Jeshi

(Elekezwa kutoka Majeshi)

Jeshi ni kundi kubwa la watu wanaopewa mamlaka ya kutumia nguvu ya silaha kutetea nchi kwa niaba ya dola au kutekeleza maagizo ya serikali dhidi ya maadui wa nje.

Jeshi la Mahdi wa Sudan.

Neno linatumika hasa kwa kutaja jeshi la ardhi, jeshi la wanamaji na jeshi la anga.

Kazi ya jeshi

hariri

Kazi ya jeshi ni

  • kulinda nchi dhidi ya maadui wa nje
  • kutetea nchi dhidi ya mashambulizi kutoka nje au
  • pia kushambulia nchi nyingine kama hatua hii imeamriwa na serikali halali.

Kusudi hilo dhidi ya hatari ya nje ndiyo tofauti kuu na kazi ya polisi ambayo ni mkono mwingine wa serikali ya taifa wenye silaha. Hata hivyo kuna nchi ambako tofauti kati ya jeshi na polisi si wazi vile, hasa kuna nchi nyingi ambako jeshi limepewa wajibu wa ndani ya taifa au ambako wanajeshi walichukua mamlaka mikononi mwao kwa nguvu ya silaha.

Katika nchi mbalimbali kuna vikosi vinavyotekeleza shughuli ndani ya taifa lakini vina silaha sawa na sehemu za jeshi na wakati mwingine vinahesabiwa kama sehemu ya jeshi. Kwa mfano vikosi vinavyolingana na FFU ya Tanzania vinaitwa gendarmerie huko Ufaransa na nchi nyingi za Afrika Magharibi au carabinieri huko Italia na kule vinahesabiwa kama mkono wa jeshi ingawa kazi yao ni ya ndani ya nchi.

Hali ya jeshi vitani husimamiwa na sheria ya kimataifa ya vita jinsi ilivyoundwa katika mikataba mbalimbali ya kimataifa. Sheria hiyo inalenga kulinda raia wakati wa vita na pia haki za wanajeshi wakikamatwa na adui. Sheria inadai ya kwamba wanajeshi wote wanahitaji

  • kuwa na sare rasmi inayoonekana na kuwatofautisha na raia
  • kuwa chini ya mamlaka rasmi inayoeleweka na kuwajibika kwa serikali yao
  • kubeba silaha zao wazi
  • kutimiza masharti ya sheria ya kimataifa

Wanajeshi wanafuata utaratibu huo wanalindwa na sheria inayokataza pia raia kubeba na kutumia silaha na kushiriki katika mapigano. Katika vita nyingi sheria ilipuuzwa lakini kuna mifano kadhaa katika karne ya 20 ambapo jinai za vitani zilifuatiliwa kwa mfano kwenye Kesi za Nuremberg kuhusu jinai za vitani upande wa Ujerumani na kesi zilizofikishwa mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai tangu mwaka 2000.

Jeshi la ardhi

hariri

Jeshi la ardhi lina kituo ama kambi ambayo kambi hii yaweza kulinda makundi ya Jeshi, divisheni ama umma wa jeshi. Kukitokea vita, Jeshi huwa wakipeleka divisheni na makundi ya kijeshi kwa vipimo kulingana na vita na mbinu za kusukuma ama kushinda adui kwa vita. Na pia ratili ya vita ikiwapendukia, Jeshi hupeleka wanajeshi pulikiza ili kusukuma adui kabisa ama kumshinda.

Jeshi la taifa

hariri

Jeshi la Taifa ni chombo kilichoanzishwa kisheria chenye silaha na askari wenye mafunzo ya kivita amabao kazi yao ni kupambana kivita kulinda ardhi ya nchi husika dhidi ya uvamizi kutoka nje. Nchi huwa na jeshi moja la kulinda mipaka yake dhidi ya uchokozi kutoka nje, lakini pia huwa na majeshi 'Usu' kadhaaa kwaajili ya kulinda usalaama wa ndani. kwa mfano; majeshi ya nchi ni kama Jeshi la Uganda (UPDF), Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (TPDF). Majeshi Usu ni kama Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na TANAPA.

Shughuli nyingi za majeshi hutofautiana kulingana na kitengo husika cha jeshi, kwa mfano jeshi la nchi kavu,Jeshi la Anga na Jeshi la Majini, haya ndiyo matawi makuu matatu ya jeshi . Kwa historia, Jeshi la anga lilikuwa pamoja na Jeshi la ardhini, hasa kwa historia ya Uchina ama Jeshi la ukombozi wa umma wa Uchina ilichanganya (jeshi la ardhi, jeshi la majini, jeshi la anga, divisheni za makombora na usayari) kwa tawi moja.

Majeshi ya kisasa yaitwa pia huduma, ama askari watawala). Hii inaweza kuhusu pia matawi ya Vita: jeshi la nchi kavu, vifaru, makombora, na mhandisi wa jeshi, na pia Wasafirishaji wa matawi kama: mawasiliano, watambuzi, daktari, wapeleka vifaa, na Jeshi la ndege (tofauti na jeshi la anga).

Tazama pia

hariri