Wamisionari wa Afrika

(Elekezwa kutoka Mapadre Weupe)

Wamisionari wa Afrika (kirefu Wamisionari wa Bibi Yetu wa Afrika, kifupi zaidi M. Afr.) ni jina rasmi la shirika la kimisionari la Kanisa Katoliki linalojulikana kwa Kiingereza kama "White Fathers" (kwa Kifaransa "Pères Blancs"), kutokana na rangi ya kanzu yao.

Kardinali Lavigerie, mwanzilishi wa shirika la kimisionari la White Fathers.

Lilianzisha mwaka 1868 na Charles Martial Lavigerie (1825-1892), askofu mkuu wa kwanza wa Algiers, Aljeria, ambaye baadaye akawa kardinali.

Lengo lilikuwa hasa uinjilishaji wa bara la Afrika, na kweli wanashirika walijitosa kufanya kazi kubwa ambayo inaendelea hata leo, ambapo lina mapadri kama 1,500.

Kisheria leo ni shirika la maisha ya kitume. Wanashirika hawaweki nadhiri kama watawa, ila kiapo cha kufanya umisionari kwa Waafrika hadi kifo chao.

Kwa agizo la mwanzilishi wao wanatakiwa kuishi katika jumuia yenye wamisionari kutoka nchi mbalimbali na kutumia hata kati yao lugha ya wenyeji.

Barua ya Lavigerie ya mwaka 1886 kwa Papa Leo XIII inasema: "Wao wanataka utawala, utaalamu na uchumi. Sisi basi, tujitahidi kuleta Ukristo na uhuru wa kweli. Afrika iwe nchi ya Waafrika, nao Waafrika wasigeuzwe kuwa Wazungu weusi." [1].

Tanbihi

hariri
  1. Kanisa katika Tanzania, V2, Kitabu cha Mwalimu, Ndanda Mission Press, 1975, uk.17.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wamisionari wa Afrika kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.