Mfalme Edmund (841/842 - Thetford, Uingereza, 20 Novemba 869/870) alikuwa mfalme wa Waangli wa Mashariki (leo Norfolk na Suffolk) katika kipindi kigumu cha karne ya 9, nchi iliposumbuliwa sana na Waviking.

Mchoro mdogo wa karne za kati wa kifodini cha Edmund.

Anaheshimiwa tangu kale kama mtakatifu mfiadini, msimamizi wa Uingereza.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1].

Maisha

hariri

Edmund alipambana na Wadani waliozoea kushambulia Britania, halafu kudai pesa nyingi ili kujiondokea salama.

Kumbe mwaka 869 Edmund alikataa kulipa, lakini alishindwa vitani na kutekwa.

Edmund aliahidiwa ataachiwa uhai na ufalme akikanusha imani yake na kukubali himaya ya Wadani. Hata hivyo alikataa mara mbili mpaka akachomwa kwa mishale[2].

Amezikwa Beadoricesworth, leo Bury St. Edmund, kilometa 50 kutoka Cambridge.

Kifo chake kikawa pia mwisho wa ufalme wa Anglia Mashariki, lakini ushujaa wake haujasahaulika, akawa kielelezo cha wengi huko Uingereza. Kabla karne hiyo haijaisha, sarafu iliyotolewa enzi ya uhai wake ilikuwa inaitwa “penny ya Mt. Edmund”.

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.