Open main menu

Mitume Petro na Paulo

HistoriaEdit

Tangu zamani sana sikukuu hiyo inaadhimishwa kila tarehe 29 Juni, ikiwaunganisha ingawa hawakuuawa pamoja.[1]

Kadiri ya mapokeo, mtume Petro alitangulia kuuawa kwa kusulubiwa kichwa chini miguu juu katika mtaa wa Vatikano, ambapo sasa limesimama basilika lake ambalo ni kanisa kubwa kuliko yote duniani.

Mtume Paulo aliuawa baadaye kwa kukatwa kichwa nje kidogo ya ngome ya mji. Sehemu hiyo kwa heshima yake lipo basilika lingine kubwa lililojengwa juu ya kaburi lake.

AdhimishoEdit

Kwa Wakatoliki ni sikukuu ya amri, yaani inayodai kila mwamini ashiriki Misa, ingawa Baraza la Maaskofu linaweza kusamehe amri hiyo kwa wakazi wa eneo lake kama kalenda ya serikali haiadhimishi kama sikukuu ya taifa.[2]

Katika Ukristo wa mashariki ndio mwisho wa mfungo wa Mitume.

TanbihiEdit

  1. The Catholic Encyclopedia, Volume XI (Robert Appleton Company, New York, 1911), s.v. "St. Paul", accessed 2007-06-04.
  2. Codex Iuris Canonici (1983), canon 1246.

Viungo vya njeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mitume Petro na Paulo kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.