Reli ya SGR ya Kenya ni mfumo mpya wa reli nchini Kenya kati ya miji wa Mombasa na Nairobi unaotumia geji sanifu (kwa Kiingereza: standard gauge). Reli hiyo ni mradi mkubwa wa miundombinu tangu uhuru mwaka 1963. Ilijengwa na kampuni ya China Road and Bridge Corporation kwa kutumia wajenzi kutoka China pamoja na Wakenya 25,000 katika muda wa miaka mitatu hadi mwaka 2016.[1]

Reli ya SGR huko Kenya

Urefu ya reli ya SGR ya Kenya ni kilomita 472 na kuna stesheni tisa.

Stesheni
Mombasa Terminus
Mariakani
Miasenyi
Voi
Mtito Andei
Kibwezi
Emali
Athi River
Nairobi Terminus

Historia

hariri

Reli ya zamani ya Kenya ilijengwa wakati wa ukoloni. Ilikuwa hasa njia ya Reli ya Kenya-Uganda. Iliporomoka tangu mwaka 2000 kwa sababu ya ukosefu wa matengenezo. Treni ya abiria ilihitaji siku nzima kutoka Mombasa hadi Nairobi badala ya saa 12 jinsi iliovyokuwa katika miaka ya 1990. Serikali ya Kenya ilikubali kukodi makandarasi ya Kichina kujenga reli ya kisasa wakati wa 2011.[2] Mradi huo umekamilishwa wakati wa mwezi Desemba mwaka 2016, takriban miezi 18 mapema zaidi.[3]


Faida za Reli ya SGR

hariri

Urahisi na haraka

hariri

Watu wanaweza kusafiri mpaka bandari ya Mombasa au hadi mji mkuu Nairobi kwa urahisi sasa kwa sababu ya reli mpya. Watahitaji kutumia saa nne na nusu tu ikilinganishwa na saa tisa kwa kutumia basi. Bila shaka, reli mpya itapunguza muda wa kusafiri. Kisha, ajali zimezidi barabarani kwa sababu ya kuongezeka kwa magari. Watu wanataka kutumia reli kwa sababu ya usalama pia.

Kuongeza nafasi za kazi

hariri

Ujenzi wa reli ya Standard Gauge ya Kenya umeongeza nafasi za kazi kwa watu elfu ishirini na tano Wakenya kulingana na mkataba kati ya serikali ya Kenya na makandarasi ya China.[4] Vijana wenyeji wengi wamepata seti mpya ya ujuzi kutokana na mradi huu. Inawezekana kwamba vijana wa Kenya wanaweza kupata kazi nzuri baada ya kukamilishwa kwa ujenzi wa reli kwa sababu ya ujuzi ambao walisoma. Reli ya kisasa itaongeza kazi, kama wahudumu katika treni, na wauzaji katika stesheni.

 
Treni ya SGR kwenye kituo cha Nairobi

Maendeleo ya uchumi

hariri

Reli ya SGR ya Kenya, bila shaka, itakuwa na manufaa ya muda mrefu kwa uchumi wa Kenya. Itaongeza usafiri wa watu na vitu kati ya miji mingi katika Kenya. Uchumi wa miji ambayo pamoja na mistari wa reli utakuwa na maendeleo. Ni muhumu zaidi kwamba reli ya SGR ya Kenya itaweza kuunganisha miji mikuu wa nchi nyingine katika Afrika mashariki.   

Upinzani

hariri

Kupunguza kazi

hariri

Hata hiyo, ingawa reli mpya inaweza kuletea Kenya maendeleo ya uchumi kwa muda mrefu, baadhi ya wafanyabiashara wameharibiwa na mradi huu. Kwa mfano, reli mpya imeathiri pakubwa biashara ya mabasi na malori.[5] Abiria zaidi wanataka kutumia reli badala ya basi. Kwa hiyo, wafanyabiashara hao wanahitaji kufikiri jinsi ya kufaa mabadiliko haya.

Athari ya reli kwa mazingira ya asili

hariri

Athari ya reli mpya kwa mazingira ya asili ya Kenya ni kwamba inapitia hifadhi ya taifa ya Tsavo.[6] Ijapokuwa mkandarasi wa China alifanya mabadiliko ya kubuni, wanyama katika mbuga ya kitaifa wanaathirika kwa mradi huu.[7]

Madeni

hariri

Watu wanasema serikali ya Kenya iliomba fedha nyingi kutoka China na itasabisha mgogoro wa madeni katika Kenya. Reli yote ilifadhiliwa kwa mikopo dola bilioni 3.2 kutoka benki ya China ya Exim katika kipindi cha miaka 2015. Kuwepo kwa milima na mabonde ilisababisha gharama ya juu ya mradi huo kulingana na serikali ya Kenya.[8]

  1. "Funds for SGR phase II to be in by January 2016, assures state". The Star (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-04-15.
  2. Kithinji, Michael Mwenda (2016), "Education System and University Curriculum in Kenya: Contentions, Dysfunctionality, and Reforms since Independence", Kenya After 50, Palgrave Macmillan US, ku. 21–40, ISBN 9781349564583, iliwekwa mnamo 2019-04-15
  3. Maafisa washtakiwa kwa madai ya ulaghai yaliokumba reli mpya Kenya (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2018-08-13, iliwekwa mnamo 2019-04-15
  4. 刘明. "Chinese-built Kenya railway on track - World - Chinadaily.com.cn". www.chinadaily.com.cn. Iliwekwa mnamo 2019-04-15.
  5. Nene, John (2018-11-09), Raha na karaha ya treni ya SGR (kwa Kiingereza (Uingereza)), iliwekwa mnamo 2019-04-15
  6. Maafisa washtakiwa kwa madai ya ulaghai yaliokumba reli mpya Kenya (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2018-08-13, iliwekwa mnamo 2019-04-15
  7. Built by Buffalo. "Bull Elephants Killed By Train". Sheldrick Wildlife Trust (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-04-15.
  8. Reli mpya ya kisasa itaifaa Kenya? (kwa Kiingereza (Uingereza)), 2017-06-26, iliwekwa mnamo 2019-04-15