Msalvia (mmea)
Msalvia | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Msalvia
(Salvia divinorum) | ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Msalvia (ujulikanao pia kama sage of the diviners, seer's sage, ska maría pastora, yerba de la pastora ama kwa kifupi salvia; jina la kisayansi Salvia divinorum) ni mmea ambao hufikia urefu wa kima zaidi ya mita moja na huwa na shina mraba lisilo na kitu ndani kama mimea mingine ya familia ya mnanaa Lamiaceae.
Majani yake hutumika pia kusafisha meno.
Utumizi wa majani yake kwa njia ya kutafuna, kuvuta kama sigara au kupika kama chai unasababisha namna ya ulevi [1] kwa sababu yana chembechembe aina ya opioidi zinazosababisha ukumbusho-wazimu (hallucination).[2]
Kwa vile mmea huu haujifanyiwa utafiti wa kina, madhara yake na usalama wa matumizi yake kwa muda mrefu bado havijathibitishwa.
Asili na historia
haririAsili ya mmea huu ni nchi ya Mexico na humea kiasilia katika msitu wa Sierra Mazateca ya Oaxaca kwenye vivuli vilivyo na unyevu.
Leo msalvia pia hukuzwa nyumbani na hupandwa vipandikizi vya tawi au shina lake kwa vile mmea huu hutoa mbegu kwa uchache na ugumu sana.
Sheria
haririMsalvia umeruhusiwa katika nchi nyingi lakini matumizi yake hudhibitiwa nchini Australia, Ubelgiji, Brazil, Canada, Denmark, Estonia, Finland, Ujerumani, Italia, Japan, Korea Kusini, Poland, Hispania, Uswisi, Armenia na sehemu nyingine Marekani.[3][4] Hata hivyo mmea huo umeenea sehemu tofautitofauti na miche yake huuzwa na wakulima wa miti na dawa katika nchi nyingine.
Marejeo
hariri- ↑ "Salvia divinorum". Drugs.com. 2018. Iliwekwa mnamo 22 Juni 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Butelman, Eduardo R; Kreek, Mary Jeanne (2015). "Salvinorin A, a kappa-opioid receptor agonist hallucinogen: Pharmacology and potential template for novel pharmacotherapeutic agents in neuropsychiatric disorders". Frontiers in Pharmacology. 6. doi:10.3389/fphar.2015.00190.
{{cite journal}}
: CS1 maint: unflagged free DOI (link) - ↑ Siebert (Legal status).
- ↑ Erowid (Legal status).