Ngome ya Yesu (pia: Boma la Yesu; kwa Kiingereza: Fort Jesus) ni ngome ya kale mjini Mombasa (Kenya). Iko kwenye kisiwa cha Mombasa ikitazama mlango wa bandari ya kale.

Geti ya ngome
Ndani ya Fort Jesus
Uwanja ndani ya ngome

Ilijengwa mwaka 1593 na msanifu Giovanni Battista Cairato kwa niaba ya Wareno na ilikuwa kituo muhimu cha Wareno kwenye njia ya mawasiliano kati ya Ureno na Uhindi. Jahazi zao zilipita Afrika Kusini zikapumzika kidogo Msumbiji penye ngome kubwa ya Kireno halafu ziliendelea kupitia Mombasa na kuvuka bahari hadi Bara Hindi.

Historia ya ngome hariri

Mabwana wa ngome walibadilishana.

Kipindi cha Kireno hariri

 • Wareno: 1593 - 1631
 • Sultani wa Mombasa: 1631 - 1632
 • Wareno: 1632 - 1698
 • Sultani wa Omani: 1698 - 1728
 • Wareno: 1728 - 1729

Baada ya kuondolewa na Waomani Wareno walisafiri moja kwa moja kati ya Msumbiji na Goa.

Kipindi cha Kiarabu hariri

Baada ya Wareno utawala wa ngome ulipiganiwa kati ya Sultani wa Omani na maliwali wa Mombasa wa nasaba ya Mazrui waliojaribu kuendelea bila mabwana wa Omani.

 • Sultani wa Oman: 1729 - 1741
 • Liwali wa Mombasa: 1741 - 1747
 • Sultani wa Oman: 1747
 • Liwali wa Mombasa: 1747 - 1828
  • (pamoja na usaidizi wa kikosi cha wanamaji kutoka Uingereza 1824)
 • Sultani wa Oman: 1828
 • Liwali wa Mombasa: 1828 - 1837
 • Sultani wa Oman: 1837 - 1856

1856 Mombasa pamoja na Boma la Yesu ilikuwa sehemu ya usultani wa Zanzibar

 • Zanzibar: 1856 - 1895
  • Uasi wa kijeshi na kurudishwa chini ya Zanzibar kwa msaada wa Uingereza: 1875

Chini ya Uingereza na Kenya hariri

1895 mji pamoja na ngome zilikodiwa na Uingereza

 • Uingereza: 1895 - 1963
 • Kenya : 1963

Waingereza walitumia ngome kama gereza.

Tangu mwaka 1958 imekuwa makumbusho ya kitaifa. Leo hii ni sehemu ya Makumbusho ya Kitaifa ya Kenya na ya urithi wa dunia wa UNESCO.

Tazama pia hariri

Viungo vya nje hariri