Papa Adeodato I (pia aliitwa Deusdedit) alikuwa Papa kuanzia tarehe 19 Oktoba 615 hadi kifo chake tarehe 8 Novemba 618[1]. Alitokea Roma, Italia[2]. Jina la baba yake lilikuwa Stephanus, ambaye alikuwa shemasi mdogo.

Papa Adeodato I.

Alimfuata Papa Bonifasi IV akafuatwa na Papa Bonifasi V.

Kabla ya kuchaguliwa, alitoa huduma ya kipadri kwa miaka 40[3]. Baadaye alikuza idadi ya mapadri na kuwapa nafasi zilizokuwa zimeshikwa na wamonaki kadiri ya sera ya Papa Gregori I na Papa Bonifasi IV[4][3] .

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu[5].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[6].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  1. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  2. https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
  3. 3.0 3.1 Attwater, Aubrey (1939). A Dictionary of Popes: From Peter to Pius XII, 66. ISBN 0199295816. 
  4. Jeffrey Richards, The Popes and the Papacy in the Early Middle Ages (London: Routledge and Kegan Paul, 1979), p. 262
  5. Philips, Fr Andrew. The Holy Orthodox Popes of Rome.
  6. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Adeodato I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.