Papa Agapeto I

Mt. Agapeto I

Papa Agapeto I alikuwa papa kuanzia mwezi wa Mei au Juni 535 hadi kifo chake tarehe 22 Aprili, 536.

Alimfuata Papa Yohane II akafuatwa na Papa Silverio.

Muda si mrefu baada ya kifo chake alianza kuheshimiwa kuwa mtakatifu.

Sikukuu yake ni 20 Septemba, tarehe alipolazwa katika kaburi la kudumu.

Alisimama imara dhidi ya Waario, pia alimwondoa madarakani Anthimus, askofu mkuu wa Trabzon (Uturuki) aliyehamishimiwa na serikali kuwa Patriarki wa Konstantinopoli kutokana na mafunzo yake yaliyoangaliwa na Kanisa Katoliki kuwa ya uzushi.

Tazama piaEdit

MarejeoEdit

Viungo vya njeEdit

Kuhusu Papa Agapeto I katika Kamusi Elezo ya Kikatoliki

  Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Agapeto I kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.