Papa Zephyrinus
Papa Zephyrinus alikuwa papa kuanzia takriban 198 hadi kifo chake tarehe 20 Desemba 217/218[1]. Alitokea Roma, Italia.
Alimfuata Papa Vikta I akafuatwa na Papa Kalisto I.
Alipambana na aina mbalimbali za uzushi kutetea umungu wa Yesu Kristo[2].
Pia alitegemeza Wakristo katika dhuluma ya kaisari Setimio Severo (193-211)[3] na kumuagiza shemasi wake Kalisto, mwandamizi wake, atengeneze shamba la Mungu la Kanisa la Roma kwenye barabara Appia[4].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Tazama pia
haririMaandishi yake
haririTanbihi
hariri- ↑ https://www.vatican.va/content/vatican/en/holy-father.index.html#holy-father
- ↑ Optatus, De Schismate 1,1
- ↑ A. Butler, Lives of the Saints Vol VIII, 1866
- ↑ https://www.santiebeati.it/dettaglio/67700
- ↑ "Calendarium Romanum" (Libreria Editrice Vaticana, 1969), p. 136
- ↑ "Martyrologium Romanum" (Libreria Editrice Vaticana, 2001 ISBN 88-209-7210-7)
Marejeo
hariri- Rendina, Claudio, The Popes' Histories and Secrets (2002)
Viungo vya nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
- Kuhusu Papa Zephyrinus katika Kamusi Elezo ya Kikatoliki
- Fontes Latinae de papis usque ad annum 530 (Papa Felix IV)
- Liber pontificalis
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Papa Zephyrinus kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |