Guinea Mpya
Guinea Mpya ni kisiwa kikubwa katika Pasifiki upande wa kaskazini wa Australia. Ni kisiwa kikubwa cha pili duniani baada ya Greenland.
Eneo la kisiwa limegawiwa kati ya mataifa mawili:
- upande wa magharibi ni mikoa ya Indonesia ya Papua na Papua Magharibi.
- upande wa mashariki ni nchi huru ya Papua Guinea Mpya
Jiografia
haririEneo lote la kisiwa ni km² 829,200 na jumla ya wakazi ni milioni 5.2 (2004).
Kuna milima mirefu; upande wa Indonesia ni milima ya Maoke (Puncak Jaya, mita 4,884 juu ya UB) na upande wa Papua Guinea Mpya ni milima ya Bismarck (Mount Wilhelm, mita 4,509 juu ya UB).
Historia
haririKisiwa kimekaliwa tangu milenia kadhaa na wenyeji Wapapua. Kati yao wanatumia zaidi ya lugha 1,000 tofauti. Waliishi katika jamii ndogo za pekee. Jiografia ya nchi inayofunikwa na misitu minene na kugawiwa na safu za milima na mabonde ilisaidia tofauti nyingi kati ya wakazi wake. Maeneo machache ya pwani kwenye magharibi yalikuwa na mawasiliano na sultani wa visiwa vya Indonesia. Wakati Wazungu walipoanza kuingia ndani ya kisiwa walikuta bado jamii nyingi zilizotumia teknolojia ya zama za mawe.
Mnamo mwaka 1545 mpelelezi Mhispania Ortiz de Retez alipita pwani Ya kisiwa akabuni jina la "Guinea Mpya" kwa sababu machoni pake wenyeji walifanana na watu aliowahi kuwaona kwenye pwani Ya Guinea katika Afrika ya Magharibi. Wakati wa karne ya 19 Uholanzi kutoka upande wa Uhindi ya Kiholanzi (Indonesia) na Uingereza kutoka upande wa Australia walianza kuunda vituo na kudai utawala juu ya sehemu za kisiwa. Ujerumani ilifuata mwaka 1884. Hivyo kisiwa kiligawiwa katika magharibi ya Kiholanzi, mashariki-kaskazini ya Kijerumani na mashariki-kusini ya Australia. Hali halisi wakoloni walitawala tu sehemu ndogo maana ukosefu wa barabara ulibana watawala kwenye bandari pwani. Baadaye matumizi ya eropleni ilirahisisha safari.
Katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Ujerumani ilishindwa na mashariki yote ilikabidhiwa kwa Australia.
Wakati wa Vita Kuu ya Pili, Japani ilivamia kisiwa kilichoona mapigano. Baada ya mwaka 1949, wakati Uholanzi ilikubali kuondoka katika Indonesia, iliamua kubaki katika Guinea Mpya ilipoanzisha Guinea Mpya ya Kiholanzi kama koloni la pekee, dhidi ya upinzani wa Indonesia iliyodai utawala juu ya sehemu ya Kiholanzi.
Ilhali Uholanzi iliandaa uhuru wa sehemu yake, Indonesia ilivamia kijeshi mwaka 1962 na Waholanzi waliondoka. Katika mapatano kabla ya kuchukua madaraka, Indonesia iliahidi kufanya kura ya wananchi wote kuhusu swali la uhuru hadi 1969. Kura hiyo ilikuwa bandia, jeshi la Indonesia liliteua watu 1,025 pekee ambao walipaswa kupiga kura hadharani; wote walikubali kubaki Indonesia. Sehemu hiyo ilitawaliwa kwa jina la "Irian Jaya".
Katika mashariki Australia iliipa uhuru kamili nchi mpya ya Papua New Guinea.
Kwenye magharibi Irian Jaya ilibadilishwa jina kuwa "Papua" ikakawiwa baadaye kuwa Mkoa wa Papua na Mkoa wa Papua Magharibi.
Marejeo
haririViungo vya Nje
haririNew Guinea travel guide kutoka Wikisafiri
- Facsimile of material from "The Discovery of New Guinea" by George Collingridge
- Scientists hail discovery of hundreds of new species in remote New Guinea
- PapuaWeb official website Ilihifadhiwa 16 Januari 2021 kwenye Wayback Machine.
- detailed map of New Guinea
- Kigezo:Cite NSRW
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Guinea Mpya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |