Raphael
Raffaello Sanzio (kwa Kiitalia huitwa pia Raffaello da Urbino; kwa Kiingereza anajulikana kama Raffael au Raphael) (6 Aprili 1483 - 6 Aprili 1520) alikuwa mchoraji na mjenzi kutoka Italia.
Pamoja na Leonardo da Vinci na Michelangelo huhesabiwa kati ya wasanii muhimu wa zama ya mwamko ya Italia.
Maisha
haririRaphael alizaliwa mjini Urbino kama mtoto wa mchoraji Giovanni Santi aliyefanya kazi katika utumishi wa mkabaila Federiko III wa Montefeltro.
Katika umri wa miaka 15 alikuwa mwanafunzi katika karakana ya mchoraji Pietro Perugino aliyeshiriki katika kazi za kupamba Kikanisa cha Sistina kwenye Vatikano.
Raphael alijifunza haraka na tangu mwaka 1500, alipokuwa na umri wa miaka 17, alipewa kazi za kwanza za kujitegemea.
Alianza kuchora picha katika makanisa ya miji mbalimbali ya Italia.
Alipenda kutembelea Firenze akitazama michoro ya walimu wa kale.
Tangu alipohamia Roma, alikoitwa na Papa Julius II, kazi kubwa aliyopewa ilikuwa picha za ukutani kwenye vyumba vya Papa mwenyewe.
Raphael aliaga dunia mapema katika umri wa miaka 37. Hakuoa wala hakuna watoto waliojulikana.
Upande wa dini, alikuwa Mkristo wa Kanisa Katoliki, tena mwanachama wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko.
Michoro yake
hariri-
Mt. Sebastiano
-
Maria na mtoto Yesu
-
Maria na mtoto Yesu (mnamo 1507)
-
Mwanamke aliyeitwa "La Muta", Galleria Nazionale delle Marche mjini Urbino
Viungo vya nje
hariri- (Kifaransa) Picha kadhaa za Rapahel Archived 19 Machi 2008 at the Wayback Machine.
- (Kifaransa) Tovuti ya kibiashara inayoonyesha picha 275 za Raffaello Santi Archived 4 Agosti 2021 at the Wayback Machine.
- (Kiingereza) Raphael kwenye Artcyclopedia
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Raphael kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |