Rosa wa Lima

Mt. Rosa wa Lima
alivyochorwa na Claudio Coello (16421693), Prado, Madrid, Hispania.

Rosa wa Lima ni jina lililoenea la Isabel Flores y de Oliva (20 Aprili 158624 Agosti 1617), binti wa Wahispania waliohamia Lima, Peru.

Alipata umaarufu kwa juhudi zake katika maisha ya kiroho na kwa huduma zake za huruma kwa maskini wa mji wake huo.

Mlei wa Utawa wa Tatu wa Mt. Dominiko na bikira, ni Mwamerika wa kwanza kutangazwa mtakatifu katika Kanisa Katoliki. Kwanza alitangazwa mwenye heri na Papa Klementi IX tarehe 10 Mei 1667, halafu mtakatifu tarehe 12 Aprili 1671 na Papa Klementi X.

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

MarejeoEdit

  • Teodoro Hampe Martínez. "Santa Rosa de Lima y la identidad criolla en el Perú colonial" (essay of interpretation), Revista de Historia de América, No. 121 (January – December, 1996), pp. 7–26

Viungo vya njeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rosa wa Lima kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.