Samari

(Elekezwa kutoka Samarium)


Samari (Samarium) ni elementi ya kikemia yenye alama Sm na namba atomia 62, maana yake kuna protoni 62 katika atomu. Ni elementi ya kimetali yenye rangi nyeupe-kifedha inayooksidika hewani. Kwenye mfumo radidia inahesabiwa kati ya lanthanidi.

Samari
Jina la Elementi Samari
Alama Sm
Namba atomia 62
Mfululizo safu Lanthanidi
Uzani atomia 150,36
Valensi 2, 8, 18, 24, 8, 2
Densiti 7.52
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka °K 1345
Kiwango cha kuchemka °K 2173
Hali maada mango

Samari iligunduliwa mnamo 1879 na Mfaransa Paul-Emile Lecoq de Boisbaudran. Ilipokea jina lake kutokana na madini Samarskiti ya madini ambayo ilitengwa. Madini yenyewe ilipata jina lake kwa heshima ya afisa wa migodi wa eneo la Urusi ambako madini yalitambuliwa mara ya kwanza.

Madini hayo hupatikana zaidi nchini Uchina, Marekani, Brazil, India, Sri Lanka na Australia; Uchina unaongoza ulimwenguni katika uchimbaji wa madini ya samari.

Samari haipatikani katika hali safi ila iko ndani ya madini mengi. Akiba za duniani kote za samari zinakadiriwa kuwa tani milioni mbili; Uzalishaji wa kila mwaka ni karibu tani 700. [1] China ina uzalishaji mkubwa zaidi na tani 120,000 zilizochimbwa kwa mwaka; inafuatwa na Marekani (kama tani 5,000) na India (t 2,700). [2] Samari kwa kawaida huuzwa kama oksidi.[3]

Samari ni metali ya ardhi adhimu yenye ugumu na densiti ya kufanana na zinki. Ugumu na wiani sawa na ile ya zinki. Kiwango cha kuchemsha ni °C 1794.

Matumizi

hariri

Matumizi ya kibiashara ya samari yapo hasa kwenye sumaku za samari-kobalti ambazo ni sumaku za kudumu. Zina faida ya kuvumilia halijoto hadi nyuzijoto °C 700 bila kupoteza tabia zake za kisumaku.

Isotopi ya samari-149 ina uwezo wa kufyonza nyutroni na kwa hiyo inatumiwa kudhibiti mchakato ndani ya matanuri ya nyuklia.

Marejeo

hariri
  1. Emsley, John (2001). "Samarium". Nature's Building Blocks: An A–Z Guide to the Elements. Oxford, England, UK: Oxford University Press. ku. 371–374. ISBN 0-19-850340-7.
  2. "Rare Earths" (PDF). United States Geological Surves. Januari 2010. Iliwekwa mnamo 2010-12-10.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. What are their prices?, Lynas corp.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Samari kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.