Santa
Santa ni neno lenye asili ya Kilatini linalotumika katika lugha nyingi kama sehemu ya majina ya watu au mahali. Maana yake ni "mtakatifu", kiasili zaidi mtakatifu wa kike. Neno mama kwa Kilatini ni "Sancta", lililoendelea katika lugha za Kirumi mbalimbali (kama Kiitalia, Kihispania, Kireno) kwa umbo la "Santa".
Miaka ya nyuma neno "santa" limejulikana hasa kama kifupi cha "Santa Claus" ambaye ni jina la mhusika katika desturi za Krismasi za Marekani akifanana na masimulizi mengine katika tamaduni za Ulaya zinazojulikana kiasi kama Baba Krismasi kwa Kiswahili, jina ambalo ni tafsiri ya Kiingereza "Father Christmas".
Vinginevyo neno "santa" ni sehemu ya majina ya miji au vijiji vilivyopokea jina kwa heshima ya mtakatifu wa kike fulani, mifano ni Santa Ana, Santa Barbara, Santa Clara, Santa Maria. "Santa" inapatikana pia kama jina linalodokeza jambo linalotazamwa kuwa takatifu kama Santa Fe (imani takatifu) kama jambo hili linaainishwa kuwa la kike kisarufi.
Angalia pia
hariri