Chuo Kikuu cha Stellenbosch
Stellenbosch University (awali Chuo Kikuu cha Stellenbosch / Universiteit van Stellenbosch) ni chuo kikuu cha umma cha utafiti katika mji wa Stellenbosch, Afrika Kusini. Vyuo vingine vilivyo karibu ni Chuo Kikuu cha Cape Town na Chuo Kikuu cha Western Cape.
Chuo Kikuu cha Stellenbosch | |
---|---|
Universiteit van Stellenbosch | |
Staff | 2,430 |
Wanafunzi | 26,243 |
Wanafunzi wa shahada ya kwanza | 15,869 |
Wanafunzi wa uzamili | 9,233 |
Mahali | {{{mji}}} |
Rangi | Maroon |
Msimbo | Maties |
Mascot | Squirrel[1] |
Affiliations | AAU, ACU, CHEC, HESA, IAU |
Faili:MatiesLogo.png |
Stellenbosch University ilisanifu na kuunda microsatellite ya kwanza barani Afrika, SUNSAT, iliyozinduliwa mwaka wa 1999.
Wanafunzi hupewa jina la msimbo Maties . Baadhi wanadai kuwa jina hili linatokana na sare yao ya mchezo wa raga yenye rangi ya maroon: tamatie ni jina la Kiafrikaans la nyanya. Inaelekea zaidi kutoka kwa lahaja ya Kiafrikaans Maat (maana yake "rafiki" au "mwenzi") lililotumiwa sana hapo awali na wanafunzi wa mtangulizi wa Chuo Kikuu cha Cape Town, Chuo cha Afrika Kusini.
Historia
haririAsili ya chuo kikuu inaweza kufuatiliwa kutoka kwa Stellenbosch Gymnasium , ambayo ilifunguliwa tarehe 1 Machi 1866, na kuwa Stellenbosch College mnamo 1881 na ambayo kwa sasa iliyo katika Idara ya Sanaa. Mwakani 1887 chuo hiki mara renamed Victoria College ; kilipopata hadhi ya chuo kikuu tarehe 2 Aprili 1918 kilibadilishwa jina tena na kuitwa Stellenbosch University .
Jina
haririMajina yote mawili Chuo Kikuu cha Stellenbosch na Stellenbosch University ni sahihi, ingawa hili la mwisho ndilo rasmi na linapaswa kutumika katika shughuli za kibiashara na mawasiliano. Hii pia inashikilia kweli katika tafsiri za Kiafrikana za jina, na Universiteit van Stellenbosch na Universiteit Stellenbosch [1] Archived 15 Novemba 2010 at the Wayback Machine. [2] Archived 16 Novemba 2010 at the Wayback Machine. Baadhi ya idara hupendelea moja juu ya lingine, kwa mfano, Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Stellenbosch , ambayo hufupishwa kuwa USB .
Daraja
haririKulingana na daraja za Chuo Kikuu cha Leiden, SU inaorodheshwa ya 454 katika vyuo vikuu 500 bora duniani kote katika masuala ya uchapishaji kimataifa na ya 415 katika suala la matokeo ya Nukuu kutoka machapisho ya kisayansi ya SU mwaka wa 2007. Hii ni mojawapo ya orodha za kuaminika zaidi katika hadhi ya utafiti lakini haipanii - na kwa sababu nzuri - kuorodhesha vyuo vikuu kwa upana [3] Archived 22 Julai 2011 at the Wayback Machine.
Shule ya Biashara ya Chuo Kikuu cha Stellenbosch(USB) ilikuwa ya 39 kati ya shule 100 za biashara zinazoongoza duniani, kulingana na utafiti wa Taasisi ya Aspen katika toleo lake mbadala Beyond Pinstripes Grey la 2009-10. USB pia ndio shule ya biashara ya pekee kutoka Afrika Kusini na pia katika bara zima iliyo katika orodha ya 100 bora. [4]
Mwaka 2009 Webometrics iliorodhesha Stellenbosch ya tatu Afrika nyuma ya Chuo Kikuu cha Cape Town na Chuo Kikuu cha Pretoria. [5] Archived 21 Februari 2010 at the Wayback Machine.
Mahali pake
haririStellenbosch, mji mkongwe zaidi nchini Afrika Kusini baada ya Cape Town, ni mji wa chuo kikuu wenye wakazi wapatao 90,000 (ukiondoa wanafunzi). Uko takriban kilomita 50 kutoka Cape Town na uko kwenye kingo za Eersterivier ( "Mto wa Kwanza") katika eneo maarufu kwa ukuzaji wa mvinyo na lililozingirwa na mandhari ya kupendeza ya milima. Mafunzo katika Chuo Kikuu cha Stellenbosch yamegawanywa kati ya kampasi kuu ya Stellenbosch, kampasi ya Tygerberg, ambapo Kitivo cha Sayansi ya Afya iliko, kampasi ya Bellville Park, ambapo Shule Hitimu ya Biashara iliko, na kampasi ya Saldanha, palipo Kitivo cha Sayansi ya Kijeshi katika Shule ya Jeshi ya Kikosi cha Ulinzi wa Taifa cha Afrika Kusini.
Lugha
haririStellenbosch University ni chuo cha kati cha Kiafrikaans, hasa katika vitengo vya shahada za kwanza na za pili. Hata hivyo, wanafunzi wanaruhusiwa kuandika na kufanya kazi zao, majaribio na mitihani katika Kiingereza na Kiafrikana. Lugha ya masomo pia inatofautiana kulingana na Kitivo, Kitivo cha Sanaa kwa mfano kikiwa na asilimia 40 Kiingereza, mafunzo mengi yakifanywa kwa lugha zote mbili na lugha ya takrima au nyenzo nyingi ikidhamiriwa na mwanafunzi.
Katika ngazi ya Uzamili lugha ya masomo hudhamiriwa kwa misingi ya mpangilio wa darasa. Nyingi ya kozi za Uzamili wa juu hufanywa kwa Kiingereza. Kulingana na hali ya sasa, asilimia 60 ya wanafunzi husema kuwa Kiafrikaans ndiyo lugha yao ya nyumbani, asilimia 32 hutumia Kiingereza kama lugha yao ya nyumbani, ilhali asilimia 1.6 tu ya wanafunzi ndio hutumia Kikhosa kama lugha yao ya nyumbani.
Sera ya lugha bado ni suala linaloendelea katika Chuo, kwa kuwa ni mojawapo ya taasisi chache za elimu ya juu katika Afrika Kusini ambazo bado zinatoa mafunzo katika lugha ya Kiafrikana. Kwa sababu hii, kinaenziwa sana katika jamii ya Waafrikana, na hata chuo hiki kuhesabiwa kama nguzo kuu katika maisha ya Kiafrikana. Nyingi ya taasisi zimetoa mafunzo kwa Kiingereza kutoka jadi au kugeuza sera na kuwa za Kiingereza tu.
Wanafunzi
haririKirangi, uwakilishi wa wanafunzi katika Stellenbosch University ni kama ifuatavyo:
Usajili Kikabila, 2009 | Asilimia | Jumla |
---|---|---|
Wazungu | 67.6% | 17.753 |
Machotara | 15.2% | 4.000 |
Weusi | 14.4% | 3.800 |
Wahindi | 1,9% | 500 |
Jumla | 100% | 26.243 |
Vitivo na shule
haririStellenbosch University ina takriban idara 150 katika vitivo 10. Pia ina zaidi ya taasisi 40 za utafiti (na nyinginezo).
Vitivo kwenye kampasi kuu ni:
- Sanaa na Sayansi za Kijamii
- Sayansi
- Elimu
- Sayansi Kilimo
- Sheria
- Thiolojia
- Sayansi za Kiuchumi na Usimamizi
- Uhandisi
Vitivo na shule ambazo haziko kwenye kampasi kuu ni:
- Sayansi ya Kijeshi - iliyoko Saldanha Bay
- Sayansi za Kiafya - iliyoko Tygerberg
- Graduate School of Business Archived 21 Desemba 2005 at the Wayback Machine. - iliyoko Bellville
Vifaa na huduma
haririMaktaba ya JS Gericke ni mashuhuri kwa kuwa chini ya ardhi, katika orofa mbili, na kusimama kwenye eneo sawa na nyanja mbili na nusu za mchezo wa raga. Maktaba hii ina mikusanyiko iliyotawanyika kote kampasi nje ya chuo kikuu, na yote imesajiliwa katika hifadhidata ya kompyuta, kwa kutumia kompyuta ya aina ya mainframe asili ya chuo kikuu, aina ya UNIVAC. Kuna maktaba nyingine kadhaa ndogo zinazoshughulikia vitivo mbalimbali, ikiwemo Maktaba ya Thiolojia, Maktaba ya Sheria na Maktaba ya Madaktari ya Tygerberg.
Chuo Kikuu cha Stellenbosch pia kina Mahafadhi pamoja na kumbi mbili za hafla. Mahafadhi hii ndio makao ya Stellenbosch University Choir ambayo imesifika sana kimataifa, pamoja na kuwa kwaya kongwe zaidi Afrika Kusini imepokea tuzo kadhaa ng'ambo [onesha uthibitisho]
Chuo kikuu pia kina ukumbi wa sanaa wenye viti 430, unaojulikana kama HB Thom Theatre na ni ukumbi wazi. Pamoja na vifaa hivi ni idara ya maigizo ya chuo kikuu, chini ya uongozi wa Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Jamii. Mara kwa mara idara hii hufanya michezo ya kuigiza, makala, kabareti na michezo nyimbo.
Langenhoven Students' Centre (Neelsie) ndio makao ya Halmashauri Wakilishi ya Wanafunzi, ukumbi wa maankuli, senema, ofisi ya posta, kituo cha manunuzi, ofisi ya ushauri na ofisi za vilabu vyote vya mwanafunzi. Bendi za wanafunzi na shughuli mbalimbali za burudani kwa kawaida hufanyika katika ukumbi wa maankuli wakati wa chakula cha mchana.
Chuo hiki kina redio yake inayojulikana kama MFM (Matie FM), iliyo na kikao chake katika Neelsie. Hupeperusha matangazo katika eneo lote la Stellenbosch katika mitabendi 92.6 FM. Hupeperusha mchanganyiko wa muziki, habari, burudani na habari za kampasi.
Chuo hiki pia husambaza machapisho kama vile Die Matie (linaloonekana kila baada ya wiki mbili), kwa ajili ya wanafunzi wake na Kampusnuus (kila mwezi) kwa wafanyakazi wake. Yearbook rasmi, Die Stellenbosch Student , huchapishwa kila mwaka na kupewa kwa wanafunzi wote waliofuzu. Matieland ni jina la gazeti rasmi la wanafunzi wa zamani. Huchapishwa mara mbili kwa mwaka na kusambazwa kwa baadhi ya wanfunzi 100,000 wa zamani na marafiki wa Chuo Kikuu.
Michezo
haririVifaa vya michezo kwa zaidi ya nyanja 30 za ushindani na burudani za michezo zinaungwa mkono na chuo kikuu pamoja na viwanja viwili vya michezo, mabwawa mawili makubwa ya kuogelea (chini ya paa moja), na DF Malan Center, ukumbi wa kusudi mbalimbali kama sherehe na michezo ya ndani, viwanja vingi vya kuchezea, kikiwemo cha Hockey, na pumzikio. Chuo kikuu hutoa michezo ifuatayo kwa wanafunzi wake:
Mwaka wa 2006 Stellenbosch ilikuwa kituo cha kujaribia mapendekezo kahdaa katika sheria za shirikisho la raga, zinazojulikana kama Sheria za Stellenbosch.
Makazi ya wanafunzi
haririChuo hiki kina makazi mbalimbali au kwa jina lingine koshuise (jina la Kiafrikana la kumbi za makazi).
Wanafunzi katika mabweni ya binafsi wanaweza kuwa wanachama wa Private Students' Organisation (PSO), inayojulikana pia kama Private Wards. Awali kulikuwa PSO 6 hadi 8 Oktoba 2008, wakati PSO nne mpya zilipofunguliwa. Wanafunzi hupewa makao mbalimbali kupitia mfumo wa mgao wa bahati nasibu. Makao ya kibinafsi huruhusu wanafunzi wote kufurahia utendaji sawa, kutoka misaada ya kitaaluma, nafasi za kimichezo, kama zinazotolewa na makao ya chuo, ilhali mwanafunzi akibakia katika makaazi ya kibinafsi.
Wanafunzi wa Zamani Mashuhuri
hariri- Andries Petrus Treurnicht, msomi wa Biblia na mwanzilishi wa Chama cha kihafidhina cha Afrika Kusini.
- Beyers Naudé, msomi wa Biblia, mwanafunzi wa HF Verwoerd na shujaa wa mapambano.
- Brian Currin wakili mashuhuri wa Haki za Binadamu.
- Billy Downer, mwendesha mashitaka ya umma.
- Casper de Vries, ni muigizaji wa Afrika Kusini, mcheshi, Mburudishaji, mtunzi, mwongozaji, mtayarishaji na mwandishi wa michoro maarufu na maonyesho ya Kiafrikana ya mtu mmoja.
- Cornelis Jacobus Langenhoven, mshairi wa Kiafrikana na mwandishi wa maneno ya Die shina .
- Cromwell Everson, mtunzi wa muziki wa aina ya classical na mtunzi wa opera ya kwanza ya Afrikaans.
- Daan du Toit, Mchungaji wa Kanisa la NG, aliyekuwa Katibu wa Chama cha NG Kerk kwa Cape Province yote, Mwanzilishi wa "Alta Du Toit School" kwa wale wenye akili punguani
- Danie Craven mchezaji maarufu wa mchezo wa Raga na msimamizi wa michezo.
- Daniel François Malan, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Afrika Kusini.
- Deon van der Walt, alikuwa mwimbaji ambaye aliimba katika Nico Malan Theatre kama Tenor.
- Edwin Cameron, ni mwanachuo wa Rhodes na Hakimu wa Mahakama.
- Elsa Joubert, riwaya yake Die swerfjare van Poppie Nongena ilitafsiriwa katika lugha 13 na kuigizwa.
- Ernst van Heerden, alikuwa mshairi mashuhuri wa Kiafrikana.
- Frederik Van Zyl Slabbert, ni mchambuzi wa kisiasa na kiongozi wa zamani wa upinzani wa Afrika Kusini.
- Friedel Sellschop, alikuwa mwanasayansi na waanzilishi katika uwanja wa fizikia ya kinuklia.
- Hein Grosskopf Archived 22 Februari 2010 at the Wayback Machine., aliyekuwa gaidi albino, sasa hakimu Botswana.
- Heinz Carl Heinrich Winckler, Mburudishaji na mwanafunzi wa zamani wa sheria.
- Hendrik Frensch Verwoerd, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Afrika Kusini.
- James Barry Munnik Hertzog mwanasheria, aliyekuwa Boer na Waziri Mkuu wa Muungano wa Afrika Kusini.
- James Leonard Brierley Smith, babake William Smith
- Jan Rupert, alisomea Uhandisi wa Kiufundi mfanyabiashara na mpwa wa Anton Rupert.
- Johann Rupert, mfanyabiashara na Mdhamini mwanzilishi wa Ufadhili wa Watoto wa Nelson Mandela.
- Jan Smuts, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Afrika Kusini, kiongozi wa kijeshi, na baba wa taifa. Mmoja wa watu muhimu waanzilishi wa Shirikisho la Mataifa na Umoja wa Mataifa.
- Johannes du Plessis Scholtz, alikuwa mwanafilolojia wa Afrika Kusini, mkusanyaji na mwanahistoria wa sanaa.
- Frederik Van Janse Johannes Rensburg, alikuwa kiongozi wa Afrika Kusini wa Ossewabrandwag.
- Jim Kroupa, wakati mwingine akijulikana kama James J Kroupa, mjenzi na mchezeshaji vibonzo ambaye amefanya miradi kadhaa ya Muppet, na muigizaji sauti katika kipindi maarufu cha Marekani watoto cha Bear in the Big Blue House.
- Lourens Wepener Hugo Ackermann, ni mmoja wa majaji wanne maalumu katika Mahakama ya Katiba ya Afrika Kusini.
- Magnus Merindol De André Malan, Waziri wa mwisho wa ulinzi wakati wa enzi iliyopita ya Apartheid.
- Martin Welz, mweledi wa uandishi pelelezi katika Afrika Kusini na Mhariri wa gazeti pelelezi la Afrika Kusini la Noseweek.
- Mark Patterson, mwekezaji wa kibinafsi katika hisa na mwanzilishi wa Global MatlinPatterson Advisors
- Mike Horn, mpenda shani wa Afrika Kusini.
- Peet Pienaar, mwanafunzi wa sanaa ambaye alifanya makumbusho ya kiwiliwili kwa kutumia mwili wake mwenyewe.
- Riaan Cruywagen, msomaji wa habari na msanii sauti ambaye amehusishwa na SABC tangu matangazo yake ya kwanza ya televisheni mwaka wa 1975.
- Rona Rupert, mwanamuziki na mwandishi wa vitabu 33 vya Kiafrikana.
- Sampie Terreblanche, aliyekuwa profesa wa Uchumi katika Stellenbosch na mwanachama mwanzilishi wa Democratic Party.
- Sandra Botha, Kiongozi wa sasa wa upinzani katika Bunge katika Democratic Alliance (Afrika Kusini).
- Stuart Abbott, mchezaji wa raga na mwanfunzi wa zamani wa uchumi.
- Uys Krige, almaarufu kama mwandishi, mshairi, Mtunga hadithi, mkalimani mchezaji raga, mwanahabari wa vita na mweledi wa mapenzi.
- Vern Poythress, mwanafalsafa za Ucalvinisti mwanachuo wa Agano Jipya
- Zanne Stapelberg, opera Soprano
Marejeo
hariri- ↑ "Meet Pokkel the Maties mascot", Matie News, 18 Februari 2009