Kitigrinya
Kitigrinya ( ትግርኛ, tigriññā, pia huandikwa Tigrigna, Tigrina, Tigriña; pia: Kitigray, Kitigre, Kihabesha) ni lugha ya Kisemiti inayozungumzwa katika Ethiopia (hasa jimbo la Tigray) na Eritrea.
Maandishi yake ni kwa alfabeti ya Kiethiopia.
Wazungumzaji
haririIdadi ya wasemaji ni takriban milioni 5-6. Wazungumzaji wa lugha hii huitwa Watigray.
Nchini Ethiopia, Kitigrinya ni lugha ya tatu inayotumiwa na watu wengi (baada ya Kioromo na Kiamhari), wakati nchini Eritrea lugha hii inaongoza kuwa lugha inayotumika zaidi nchini humo. Waongeaji wengine wanaotumia lugha hii ni pamoja na wahamiaji wengi duniani ikiwa pamoja na wale wa huko Sudan, Saudi Arabia, Marekani, Ujerumani, Italia, Uingereza, Kanada na Sweden, pamoja na watu wa jamii ya Beta Israel ambao kwa sasa huishi nchini Israeli.
Historia
haririKitigrinya kimetokana na lugha ya kale ya Ge'ez iliyokuwa lugha ya nyanda za juu za Ethiopia na hadi leo ni lugha ya liturgia katika Kanisa la Kiorthodoksi la Ethiopia na la Eritrea.
Maandiko ya mwanzo kabisa ya lugha ya Kitigrinya yanafuata baada ya sheria za jadi zinazopatikana katika wilaya ya Logosarda, yaliyopo kusini mwa Eritrea tokea mwanzoni mwa karne ya 13.[1]
Lugha ya Kitigrinya, pamoja na lugha ya Kiarabu, zilikuwa kati ya lugha rasmi katika shirikisho lililodumu kwa muda mfupi la Ethiopia na baadaye nafasi yake ilichukuliwa na lugha ya Kiamhari. Tangu kupatikana kwa uhuru wa Eritrea mwaka 1991, lugha ya Kitigrinya iliendelea kama lugha inayotumika zaidi nchini humo, na kuifanya nchi hiyo kuwa nchi pekee duniani kuitambua lugha ya Kitigrinya katika ngazi ya taifa.
Katika eneo la Eritrea, wizara ya habari iliamua kuanzisha gazeti la kila wiki liandikwalo kwa lugha ya Kitigrinya lilikua likigharimu takribani senti tano na kuuza nakala zaidi ya 5,000 kila wiki. Katika kipindi hiki, gazeti hili lilifahamika kama la kipekee zaidi.[2]
Lahaja za Kitigrinya hutofautiana kimatamshi, kimaana na kimaandishi.[3] Hadi sasa, hakuna lahaja ambayo imeshakubaliwa kuwa ndiyo maalum kwa watumiaji wa lugha hii.
Lugha hii mara nyingi huchanganywa na lugha nyingine ambazo kwa namna fulani hufanana nazo hasa katika matamshi, kwa mfano lugha ya Kitigre ambayo lugha hii hutumika katika maeneo ya ukanda wa chini wa Eritrea, hasa upande wa Kaskazini na Magharibi ambapo lugha hii hutumika.
Marejeo
hariri- ↑ "UCLA Language Materials Project Language Profiles Page: Tigrinya". UCLA. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-03-02. Iliwekwa mnamo 2006-11-10.
- ↑ Ministry of Information (1944) The First to be Freed—The record of British military administration in Eritrea and Somalia, 1941-1943. London: His Majesty's Stationery Office.
- ↑ Leslau, Wolf (1941) Documents Tigrigna (Éthiopien Septentrional): Grammaire et Textes. Paris: Librairie C. Klincksieck.
Bibliografia
hariri- Amanuel Sahle (1998) Säwasäsǝw Tǝgrǝñña bǝsäfiḥ. Lawrencevill, NJ, USA: Red Sea Press. ISBN 1-56902-096-5
- Dan'el Täxlu Räda (1996, Eth. Cal.) Zäbänawi säwasəw kʷ'ankʷ'a Təgrəñña. Mäx'älä
- Rehman, Abdel. English Tigrigna Dictionary: A Dictionary of the Tigrinya Language: (Asmara) Simon Wallenberg Press. Introduction Pages to the Tigrinya Language ISBN 1-84356-006-2
- Eritrean People's Liberation Front (1985) Dictionary, English-Tigrigna-Arabic. Rome: EPLF.
- ----- (1986) Dictionary, Tigrigna-English, mesgebe qalat tigrinya englizenya. Rome: EPLF.
- Kane, Thomas L. (2000) Tigrinya-English Dictionary (2 vols). Springfield, VA: Dunwoody Press. ISBN 1-881265-68-4
- Leslau, Wolf (1941) Documents tigrigna: grammaire et textes. Paris: Libraire C. Klincksieck.
- Mason, John (Ed.) (1996) Säwasǝw Tǝgrǝñña, Tigrinya Grammar. Lawrenceville, NJ, USA: Red Sea Press. ISBN 0-932415-20-2 (ISBN 0-932415-21-0, paperback)
- Praetorius, F. (1871) Grammatik der Tigriñasprache in Abessinien. Halle. ISBN 3-487-05191-5 (1974 reprint)
- Täxästä Täxlä et al. (1989, Eth. Cal.) Mäzgäbä k'alat Təgrəñña bə-Təgrəñña. Addis Ababa: Nəgd matämiya dərəǧǧət.
- Ullendorff, E. (1985) A Tigrinya Chrestomathy. Stuttgart: F. Steiner. ISBN 3-515-04314-4
- Ze'im Girma (1983) Lǝsanä Ag’azi. Asmara: Government Printing Press.
Viungo vya nje
hariri- (en) Muhtasari kuhusu Kitigrinya kwenye Ethnologue
- lugha ya Kitigrinya kwenye Multitree
- ramani ya Kitigrinya Ilihifadhiwa 21 Juni 2010 kwenye Wayback Machine.
- Tigrinya classes for children of Tigrinya-speaking immigrants in Sweden Ilihifadhiwa 17 Agosti 2009 kwenye Wayback Machine., including teaching materials.
- Tigrigna online Ilihifadhiwa 14 Novemba 2020 kwenye Wayback Machine., includes an online English-Tigrinya dictionary.
- Sites with Tigrinya text or sound files (all require a Ge'ez Unicode font).
- Asmarino Ilihifadhiwa 13 Januari 2006 kwenye Wayback Machine.: Eritrean exile site.
- Meskerem: "Eritrean opposition" website.
- Eritrean government site with links to Haddas Ertra Ilihifadhiwa 17 Januari 2006 kwenye Wayback Machine., the daily Tigrinya newspaper in Eritrea.
- Christian recordings in Tigrinya: Global Recordings website.
- Tigrina Learning and Playing Game Board - ጸወታ ፍልጠት: It provides for playful learning of the Ge'ez script and all languages which are written with it.[1] Ilihifadhiwa 19 Januari 2021 kwenye Wayback Machine.
Jina la lugha | |||||||||||||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
ትግርኛ tigriññā | |||||||||||||||||||||||||||||||
Pronunciation | /tɨɡrɨɲa/ | ||||||||||||||||||||||||||||||
Inazungumzwa nchini | — | ||||||||||||||||||||||||||||||
Ukanda | — | ||||||||||||||||||||||||||||||
Jumla ya wazungumzaji | — | ||||||||||||||||||||||||||||||
Familia ya lugha | {{
|
Afro-asiatic | yellow = Afro-Asiatic | orange = Niger-Congo | gold = Nilo-Saharan | goldenrod = Khoisan | lawngreen = Indo-European | lightgreen = Caucasian | yellowgreen = Altaic | limegreen = Uralic | mediumspringgreen = Dravidian | Paleo-Siberian | Paleo-siberian | Palaeosiberian | Palaeo-Siberian | Palaeo-siberian = Paleosiberian | pink = Austronesian | Austro-asiatic | Austroasiatic | lightcoral = Austro-Asiatic | tomato = Sino-Tibetan | Hmong-Mien = Hmong-Mien | orchid = Australian | violet = Papuan | lavender = Tai-Kadai | lightblue = American | Na-Dené | deepskyblue = Na-Dené | Dené-Yeniseian | deepskyblue = Dené-Yeniseian | lightcyan = Eskimo-Aleut | creole = Creole | pidgin = Pidgin | mixed = Mixed | isolate | language isolate | #dddddd = language isolate | sign | sign language | silver = sign language | conlang | constructed language | black = constructed language | default | white = — |
}} | |
Mfumo wa uandikaji | Ge'ez alphabet abugida | ||||||||||||||||||||||||||||||
Hadhi rasmi | |||||||||||||||||||||||||||||||
Lugha rasmi nchini | Eritrea (working language) | ||||||||||||||||||||||||||||||
Hurekebishwa na | No official regulation | ||||||||||||||||||||||||||||||
Misimbo ya lugha | |||||||||||||||||||||||||||||||
ISO 639-1 | ti | ||||||||||||||||||||||||||||||
ISO 639-2 | tir | ||||||||||||||||||||||||||||||
ISO 639-3 | tir | ||||||||||||||||||||||||||||||
Note: This page may contain IPA phonetic symbols in Unicode. |