Udhu
Udhu katika lugha ya Waislamu inamaanisha uzuri na usafi.
Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya |
Imani na ibada zake |
Umoja wa Mungu |
Waislamu muhimu |
Abu Bakr • Ali |
Maandiko na Sheria |
Qur'an • Sunnah • Hadithi |
Historia ya Uislamu |
Historia |
Tamaduni za Kiislamu |
Shule • Madrasa |
Tazama pia |
Sheria inawadai kutumia maji kwenye viungo maalumu kwa nia ya kujitwahirisha.
Ufafanuzi
haririKutawadha ama ni lazima ama inapendekezwa.
a. Ni lazima kutawadha kwa mambo matatu:
1. Kuswali: Katika Kurani Mwenyezi Mungu anasema: "Enyi Mlioamini! Mnaposimama kwa ajili ya swala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni" [5: 6]
2. Kutufu Alkaba: Kwa kauli yake Mtume Mohamed kumwambia mwanamke aliye katika hedhi: "Usitufu mpaka utwahirike" (imepokewa na Bukhari).
3. Kushika Msahafu: Kwa neno lake Mwenyezi Mungu: "Hawaigusi isipokuwa wale waliotwahiriwa" [56: 79]
b. Kutawadha kunasuniwa katika mambo mengine yasiyokuwa hayo:
Kwa neno lake Mtume alisema: "Hajilazimishi na udhu isipokuwa mwenye imani" (imepokewa na Ahmad).
Kunapendekezwa zaidi kutawadha wakati wa kujadidisha udhu kwa kila swala, kutawadha kwa kumtaja Mwenyezi Mungu na kuomba, wakati wa kusoma Qur’ani, kabla ya kulala, kabla ya kuoga, na kutokana na kumbeba maiti na baada ya kila tukio la kutangua udhu, hata kama hataki kuswali.
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |