Visiwa vya Cook (kwa Kiingereza: Cook Islands, kwa Kimaori: Kūki 'Āirani) ni nchi huru ya Polynesia katika Pasifiki iliyopo katika hali ya ushirikiano wa hiari na Nyuzilandi.

Visiwa vya Cook
Cook Islands
Kūki 'Āirani
Bendera ya Visiwa vya Cook Nembo ya Visiwa vya Cook
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa:
Wimbo wa taifa: Te Atua Mou E
Mungu ni Ukweli
Lokeshen ya Visiwa vya Cook
Mji mkuu Avarua
21°12′ S 159°46′ W
Mji mkubwa nchini Avarua
Lugha rasmi Kiingereza
Kimaori
Serikali
Mfalme
Mwakilishi wa Mfalme
Waziri Mkuu
Ufalme wa kikatiba
Charles III wa Uingereza
Tom Marsters
Mark Brown
Uhuru
Kujitawala kwa
ushirikano wa hiari
na New Zealand


4 Agosti 1965
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
240 km² (ya 209)
--
Idadi ya watu
 - [[]] kadirio
 - 2021 sensa
 - Msongamano wa watu
 
(ya 223)
15,040
66/km² (ya 138)
Fedha Dollar ya New Zealand
(pia Dollar ya Cook Islands) (NZD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC-10)
(UTC)
Intaneti TLD .ck
Kodi ya simu +682

-


Ramani ya Visiwa vya Cook

Eneo lake ni visiwa vidogo 15 vyenye eneo la km² 240.

Mji mkuu wa Avarua uko kwenye kisiwa cha Rarotonga.

Historia hariri

Jina limetolewa kwa kumbukumbu ya mpelelezi Mwingereza James Cook aliyefika kwenye kisiwa cha Manuae mwaka 1773 na kuchora visiwa hivi mara ya kwanza kwenye ramani ya dunia.

Visiwa vilikuwa eneo lindwa la Uingereza katika karne ya 19 kufuatana na ombi la malkia wa Cook aliyeogopa uvamizi wa Ufaransa wakati ule.

Chini ya utawala wa Kiingereza viliwekwa chini ya usimamizi wa serikali ya New Zealand, zikabaki hivyo katika hatua mbalimbali za uhuru wa New Zealand.

Mwaka 1965 New Zealand ikawapa watu wa Cook nafasi ya kujiamulia kuhusu uhuru wao. Visiwa viliamua kujitawala katika ushirikiano na New Zealand. Hatua hiyo ilisimamiwa na Umoja wa Mataifa kwa azimio lake No. 1514 (XV).

Sheria huamuliwa na bunge la visiwa vya Cook. Serikali haisimamiwi na New Zealand. Wananchi wote wana uraia wa New Zealand inayoendesha pia shughuli za jeshi na siasa ya nje kwa niaba ya visiwa. Visiwa vya Cook vimebaki na nafasi ya kufanya mapatano na nchi za nje vilevile.

Watu hariri

Wakazi ni 15,040 (2021), karibu wote wenye asili ya Kimaori (78.2%) na machotara wa Kimaori (7.6%).

Lugha zinazotumika ni hasa Kiingereza (86.4%) na Kimaori (76.2%).

Upande wa dini, wengi ni Wakristo, hasa Waprotestanti (68.2%) na Wakatoliki (17%).

Uchumi hariri

Utalii ni biashara kuu visiwani.

Picha hariri

Tazama pia hariri

Viungo vya nje hariri


  Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.