Uskoti
| |||||
Wito: Nemo me impune lacessit (Kilatini: Hakuna anayenichokoza bila adhabu) | |||||
| |||||
Uskoti (kijani cheusi) katika kisiwa cha Britania (Uingereza) | |||||
Lugha | Kiingereza, Kigaeli, Kiskoti | ||||
Mji mkuu | Edinburgh | ||||
Mji mkubwa | Glasgow | ||||
Waziri Mkuu | Nicola Sturgeon | ||||
Eneo - Total - % water |
78,782 km² 1.9% | ||||
Wakazi - Jumla (2001) - msongamano |
5,062,011 64/km² | ||||
GDP (PPP) • Total • Per capita |
2002 est. $130 Billioni $25,546 | ||||
Pesa | Pound sterling (£) (GBP) | ||||
Time zone - Summer (DST) |
GMT (UTC+0) BST (UTC+1) | ||||
Internet TLD | .uk | ||||
Calling Code | 44 |
Uskoti ni nchi ya Ulaya. Iko kaskazini mwa kisiwa cha Britania Kuu ikiwa sehemu ya Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini.
Jiografia
haririUskoti ni theluthi ya kaskazini ya kisiwa cha Britania. Eneo lake ni km² 78,772. Upande wa kusini Uskoti umepakana na Uingereza wenyewe.
Upande wa mashariki kuna Bahari ya Kaskazini, upande wa kaskazini na magharibi ile ya Atlantiki pamoja na bahari ya Eire.
Ndani ya nchi kuna kanda tatu:
- Nyanda za Juu
- tambarare za chini
- vilima vya Kusini
Mlima mkubwa wa Uskoti ni Mlima Nevis karibu na Fort William wenye kimo cha mita 1,344.
Mbali ya bara Uskoti ina visiwa 790. Upande wa magharibi wa Uskoti bara liko funguvisiwa la Hebridi. Upande wa kaskazini kuna visiwa vya Orkney na vya Shetland.
Historia
haririKihistoria Uskoti uliwahi kuwa nchi ya pekee, mpaka ikaunganishwa chini ya Ufalme wa Uingereza tangu mwaka 1603 BK.
Tangu mwaka 1707 Uskoti haukuwa tena na bunge la pekee lakini ulikuwa na wawakilishi katika bunge la London. Bunge la Uskoti lilirudishwa tena mwaka 1999 nalo linasimamia mambo ya ndani.
Mnamo Septemba 2014, wananchi walipiga kura kuhusu uhuru wa nchi yao, lakini wengi waliamua kudumisha Ufalme wa Muungano. Hata hivyo, baada ya Ufalme huo kujitoa katika Umoja wa Ulaya, kuna mpango wa kupiga tena kura mwaka 2023.
Miji kumi mikubwa ya Uskoti
haririMji | Wakazi 5 Aprili 1991 |
Wakazi 29 Aprili 2001 |
---|---|---|
Glasgow (Glaschu) | 658.379 | 629.501 |
Edinburgh (Dùn Èideann) | 400.632 | 430.082 |
Aberdeen (Obar Dhèathain) | 182.133 | 184.788 |
Dundee (Dùn Dè, Dùn Dèagh) | 157.808 | 154.674 |
Paisley (Paislig) | 73.925 | 74.170 |
East Kilbride (Cille Bhrìghde an Ear) | 70.579 | 73.796 |
Hamilton (Hamaltan) | 49.988 | 48.546 |
Cumbernauld (Comainn nan Allt) | 49.507 | 49.664 |
Greenock (Grianaig) | 49.267 | 45.467 |
Ayr (Àir) | 47.962 | 46.431 |
Picha za Uskoti
hariri-
Ukuta wa Adriano ni mpaka wa kale kati ya eneo la Dola la Roma (kusini) na maeeno huru ya Uskoti (kaskazini) wakati wa karne ya 2 BK.
-
Sueno's Stone ni makumbusho ya zamani za Wapikti katika Uskoti
-
Kinubi cha Kiskoti au clarsach.
-
Maghofu ya monasteri ya Melrose Abbey.
-
Boma mjini Edinburgh.
-
Boma la Stirling Castle.
-
Daraja la Reli la Forth.
Viungo vya Nje
hariri- Maps Archived 23 Novemba 2005 at the Wayback Machine. and digital collections Archived 6 Februari 2006 at the Wayback Machine. at the National Library of Scotland
- The Gazetteer for Scotland Archived 22 Januari 2007 at the Wayback Machine. - Extensive guide to the places and people of Scotland, by the Royal Scottish Geographical Society and University of Edinburgh
- SiliconGlen, Scotland - site hosting the first online guide to Scotland and the soc.culture.scottish FAQ.
- (PDF file) Scottish economic statistics 2005 Archived 7 Novemba 2006 at the Wayback Machine. - from the Scottish Executive
- Scottish Census Results On Line Archived 4 Julai 2008 at the Wayback Machine. - official government site for Scotland's census results
- Scottish Executive - official site of the Scottish Executive
- Scottish Parliament - official site of the Scottish Parliament
- Scottish Tourist Board - official site of Scotland's national tourist board, VisitScotland
- Scottish news, travel and history - from BBC Scotland
- Scottish Neighbourhood Statistics Archived 30 Novemba 2003 at the Wayback Machine. - Scottish Executive's programme of small area statistics in Scotland
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Uskoti kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |