Ghat ya Magharibi

(Elekezwa kutoka Western Ghats)

Milima ya Ghat ya Magharibi ni eneo la milima inayoenea katika urefu wa km 1,600 sambamba na pwani ya magharibi ya Bara Hindi, kupitia majimbo ya Kerala, Tamil Nadu, Karnataka, Goa, Maharashtra na Gujarat[1].

Ghat ya Magharibi (Wetsren Ghats) upande wa magahribi wa Bara Hindi

Ni eneo lililoandikishwa na UNESCO kama Urithi wa Dunia likiwa kati ya vitovu vya bioanwai[2]. Kuna idadi kubwa ya spishi za wanyama na mimea ambayo inapatikana nchini Uhindi pekee.

Jina la "ghat" katika lugha za Kihindi linamaanisha "safu ya milima". Safu hiyo ina athira kubwa kwa hali ya hewa na mwendo wa masika ya monsuni (pepo za msimu katika Bahari Hindi) yanayoonyesha kwa wingi kwenye mitelemko ya magharibi ya Ghat ilhali kiasi kinachofika upande wa mashariki ni kidogo.

Maeneo

hariri

Masafa ya milima ya Ghat huanzia kaskazini kuelekea kusini kando ya magharibi na kuacha tambarare nyembamba kwenye pwani ya magharibi.

Maeneo mengi ndani ya Ghat yametengwa kama hifadhi ya taifa au misitu inayohifadhiwa. [3]

Masafa huanza karibu na mji wa Songadh wa Gujarat, na kuishia karibu na ncha ya kusini ya Uhindi. Eneo la milima hii lina jumla ya kilomita za mraba 160,000 na kuwa eneo la kukusanya maji kwa mito inayomwagilia asilimia 40 za Uhindi. Mwinuko wa wastani ni mnamo mita 1,200 juu ya UB. [4]

Vilele

hariri

Ghat ya Magharibi huwa na milima mirefu inayofikia kimo cha zaidi ya mita 2000. Mlima Anamudi (mita 2,695) ndio mlima mrefu zaidi.

Chanzo cha mito

hariri

Mvua inayonyesha kwenye Ghat ya Magharibi unalisha mito mingi ya kudumu ya Uhindi. Mifumo mikubwa ya mito inayotokea kwenye Ghat ya Magharibi, hii ni pamoja na mito ya Godavari, Kaveri, Krishna, Thamiraparani na Tungabhadra . Mito mingi midogo zaidi yenye chanzo kwenye Ghat inajiunga na mito hiyo, na hubeba maji mengi wakati wa miezi ya masika. Mito hiyo inaelekea hasa upande wa mashariki ikifuata mtelemko wa nchi ikiishia kwenye Ghuba ya Bengali.

Mito ya Periyar, Bharathappuzha, Pamba, Netravati, Sharavathi, Mandovi na Zuari inashuka upande wa magharibi ikiishia katika Bahari Arabu. Kutokana na mtelemko mkali upande huu inashuka kwa kasi kali.

 
Maporomoko ya Jog huko Karnataka, moja ya milango ya kuvutia zaidi nchini India.
 
Mvua ya kila mwaka kando ya mkoa wa Magharibi wa Ghat.

Kanda ya Maharashtra kwa wastani hupata mvua nzito kuliko mikoa ya Karnataka, Kerala na Goa. Katika Maharashtra mvua inaenea sawasawa zaidi kwa sababu mabonde mengi yanaruhusu sehemu za mawingu kupita safu ya Ghat. Lakini Ghat huko Karnataka inaacha nafasi chache za mawingu kupita hivyo miteremko ya magharibi ya Karnataka hupokea mvua kubwa, zaidi ya sm 400, kushinda sehemu nyingine za Ghat ya Magharibi.

Mahali Eneo Kiwango cha mvua cha mwaka (milimita)[5]
Agumbe Thirthahalli, Karnataka mm 7624
Amboli Sindhudurg district, Maharashtra mm 3859
Hulikal Hosanagara, Karnataka 5316
Amagaon Khanapur, Karnataka mm 4089
Kakkalli Sirsi, Uttara Kannada district, Karnataka mm 4921
Nilkund Sirsi, Uttara Kannada district, Karnataka mm 4369
Mahabaleshwar Satara district, Maharashtra mm 5761
Devimane Sirsi, Uttara Kannada district, Karnataka mm 3981
Surli Hosanagara, Karnataka mm 4335
Lonavla Pune district, Maharashtra mm 4073
Charmadi Mudigere, Karnataka mm 4131
Samse Mudigere, Karnataka mm 3914
Kollur Udupi district, Karnataka mm 4992
Makkiyad Wayanad district, Kerala mm 3714
Kudremukh Chikmagalur district, Karnataka mm 4158
Rajamalai Idukki, Kerala mm 4785
Nyamakad Idukki, Kerala mm 3007
Sholayar Coimbatore, Tamil Nadu mm 3024
Vythiri Wayanad district, Kerala mm 4000
Pookode Wayanad district, Kerala mm 3957
Dhamanohol Mulshi taluka, Maharashtra mm 6255
Mulshi Pune district, Maharashtra mm 5100
Tamhini Ghat Mulshi taluka, Maharashtra mm 5255
Chinnakallar Coimbatore, Tamil Nadu mm 2947
Rock Rock Uttara Kannada district, Karnataka mm 5132

Mamalia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. "Western Ghats".
  2. Myers, Norman; Mittermeier, Russell A.; Mittermeier, Cristina G.; Da Fonseca, Gustavo A. B.; Kent, Jennifer (2000). "Biodiversity hotspots for conservation priorities". Nature. 403 (6772): 853–858. doi:10.1038/35002501.
  3. "Western Ghats". UNESCO. Iliwekwa mnamo 3 Januari 2013.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "The Peninsula". Asia-Pacific Mountain Network. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Agosti 2007. Iliwekwa mnamo 19 Machi 2007.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. https://en.climate-data.org

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Uhindi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ghat ya Magharibi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.