Kitabu cha Yona ni kimojawapo kati ya vitabu vinavyounda Tanakh (yaani Biblia ya Kiebrania), kwa hiyo pia Agano la Kale, sehemu ya kwanza ya Biblia ya Kikristo.

Mahali pake katika Biblia

hariri

Tokea zamani kitabu hicho kimepangwa kati ya "Manabii wadogo" kwa sababu mhusika mkuu amepewa jina la nabii mmojawapo wa zamani.

Hata hivyo hakileti ujumbe wa kinabii, bali kinafanana zaidi na hadithi zenye fundisho la imani au maadili, kama vingine vilivyopangwa kati ya "vitabu vya historia".

Habari ni kwamba mtu huyo, alipopata wito wa kinabii kwa faida ya Waashuru wa mji wa Ninawi, maadui wa Israeli, alijaribu kuukwepa.

Baadaye, alipolazimika kuwatangazia adhabu ya Mwenyezi Mungu, alionyesha huzuni kali kwa kuona wametubu na kuhurumiwa na Mungu.

Lengo la kitabu

hariri

Lengo kuu la kitabu ni kupambana na utaifa wa Wayahudi uliowafanya wadhani Mungu anatakiwa kuwapenda wao tu, hata kusikitikia huruma yake kwa watu wa mataifa.

Mwangwi katika Agano Jipya

hariri

Yona anatajwa katika Injili kuhusiana na ishara yake iliyomuashiria Yesu.

Kwanza, kwa kuhubiri pasipo miujiza, alionyesha mtu anapaswa kupokea ujumbe wa Mungu bila ya kumdai ishara inayothibitisha ukweli wake.

Pili, kwa kuwemo siku tatu tumboni mwa nyangumi, alifanywa ishara ya Yesu Kristo aliyekaa hadi siku ya tatu ndani ya kaburi.

Ufafanuzi wake

hariri

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Marejeo

hariri


Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo * Kutoka * Walawi * Hesabu * Kumbukumbu * Yoshua * Waamuzi * Ruthu * Samueli I * Samueli II * Wafalme I * Wafalme II * Mambo ya Nyakati I * Mambo ya Nyakati II * Ezra * Nehemia * TobitiDK * YudithiDK * Esta * Wamakabayo IDK * Wamakabayo IIDK * Yobu * Zaburi * Methali * Mhubiri * Hekima DK * SiraDK * Wimbo Bora * Isaya * Yeremia * Maombolezo * BarukuDK * Ezekieli * Danieli * Hosea * Yoeli * Amosi * Obadia * Yona * Mika * Nahumu * Habakuki * Sefania * Hagai * Zekaria * Malaki

Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.

  Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitabu cha Yona kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.