Kitabu cha Mhubiri

wa ishirini ya kwanza kitabu Biblia, mchanganyiko 12 sura ya

Mhubiri (pia: Koheleti) ni kimojawapo kati ya vitabu vya hekima vilivyomo katika Tanakh (Biblia ya Kiebrania) na hivyo pia katika Agano la Kale la Biblia ya Kikristo. Kwa sababu hiyo kilidhaniwa kimeandikwa na mfalme Solomoni, kielelezo cha hekima katika Biblia.

Kitabu hicho kina sura kumi na mbili na kwa kiasi kikubwa kimeandikwa kwa njia ya ushairi.

JinaEdit

Katika lugha ya Kiebrania jina lake ni קֹהֶלֶת (Qohelet), maana yake "Mhadhiri": ndivyo anavyojiita mwandishi, ambaye hajulikani kwa jina.

MadaEdit

Yeye anakabili masuala ya maisha kwa kuzingatia upande chanya na upande hasi wa kila moja ili kufikia hekima.

Hasa anajiuliza juu ya maana ya maadili wakati ufunuo wa Mungu ulikuwa haujafikia hatua ya kufundisha uzima wa milele na maisha yalikuwa yanaonyesha mara nyingi ustawi wa waovu na hali ngumu ya waadilifu.

Mbele ya utovu wa haki duniani, Mhubiri alikariri, "Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili" (1:2).

Hata hivyo, hatimaye akajumlisha mawazo yake kwa kuhimiza kwa imani, "Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya" (12:13-14).

UfafanuziEdit

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Maendeleo hayo yataweka wazi kwamba hukumu itafanyika baada ya kifo, na kwamba tuzo na [[]]adhabu vitatolewa kwa haki katika uzima wa milele.

TanbihiEdit

MarejeoEdit

Marejeo mengineEdit

  • Ranston, Harry (1925). Ecclesiastes and the Early Greek Wisdom Literature. First ed. Epworth Press.
  • Shapiro, Rabbi Rami Translation & Annotation, Foreword by Rev. Barbara Cawthrone Crafton (2010). Ecclesiastes Annotated & Explained. Skylight Paths Publishing

Viungo vya njeEdit

Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Tafsiri za Kiingereza
  Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitabu cha Mhubiri kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.