Yasinta wa Fatima

(Elekezwa kutoka Yasinta Marto)

Yasinta Marto wa Fatima (5 Machi 1910 - 20 Februari 1920)[1], ni jina la mmojawapo kati ya watoto watatu waliotokewa na malaika wa amani (1916), halafu na Bikira Maria (1917) kwao Fatima, Ureno, pamoja na binamu yake Lusia Santos na kaka yake Fransisko Marto.

Picha halisi ya Lusia Santos (kushoto) na binamu zake Fransisco na Yasinta Marto, mwaka 1917.
Mahali pa Fatima nchini Ureno.
Sanamu iliyotiwa taji ya Bikira Maria ya Fatima katika kikanisa kilichopo mahali pa njozi.

Njozi hizo zilithibitishwa na Kanisa Katoliki kuwa za kuaminika[2], hata ikaanzishwa kumbukumbu ya Bikira Maria wa Fatima katika liturujia kila tarehe ya njozi ya kwanza, 13 Mei.

Katika umri wake mdogo, Yasinta alivumilia kishujaa mateso ya ugonjwa wake na kushuhudia heshima yake ya pekee kwa Bikira Maria.

Pamoja na kaka yake Fransisko, alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mwenye heri tarehe 13 Mei 2000, halafu na Papa Fransisko kuwa mtakatifu tarehe 13 Mei 2017, miaka 100 kamili tangu tukio la kwanza, akiwa mdogo kuliko watakatifu wote wasio wafiadini.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  1. "Shrine of Fatima | Today marks the anniversary of Saint Jacinta Marto's birth". Santuário de Fátima (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-03-07.
  2. Papa Pius XII, Papa Paulo VI, Papa Yohane Paulo II, Papa Benedikto XVI na Papa Fransisko walikubali asili ya Kimungu ya njozi za Fatima.
  3. Martyrologium Romanum

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.