Fransisko wa Fatima

(Elekezwa kutoka Fransisko Marto)

Fransisko Marto wa Fatima (11 Juni 1908 - 4 Aprili 1919), ni jina la mmojawapo kati ya watoto watatu waliotokewa na malaika wa amani (1916), halafu na Bikira Maria (1917) kwao Fatima, Ureno, pamoja na binamu yake Lusia Santos na dada yake Yasinta Marto.

Picha halisi ya Lusia Santos (kushoto) na binamu zake Fransisco na Yasinta Marto, mwaka 1917.
Mahali pa Fatima nchini Ureno.
Sanamu iliyotiwa taji ya Bikira Maria ya Fatima katika kikanisa kilichopo mahali pa njozi.

Njozi hizo zilithibitishwa na Kanisa Katoliki kuwa za kuaminika[1], hata ikaanzishwa kumbukumbu ya Bikira Maria wa Fatima katika liturujia kila tarehe ya njozi ya kwanza, 13 Mei.

Fransisko, katika miezi iliyofuata na ugonjwa uliommaliza, aling’aa kwa maadili, kwa kuvumilia tabu, kwa imani na kwa kudumu katika sala[2].

Pamoja na dada yake mdogo Yasinta, alitangazwa na Papa Yohane Paulo II kuwa mwenye heri tarehe 13 Mei 2000, halafu na Papa Fransisko kuwa mtakatifu tarehe 13 Mei 2017, miaka 100 kamili tangu tukio la kwanza.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[3].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.