Yohane Ogilvie
John Ogilvie (Drumnakeith, Banffshire, 1579 – Glasgow Cross, 10 Machi 1615) alikuwa padri Mjesuiti kutoka Uskoti.
Mtoto wa kwanza wa Walter Ogilvie, Mkalvini tajiri, alipokuwa na umri wa miaka 12 alitumwa Ulaya bara kwa masomo.
Mwaka 1596 alijiunga na Kanisa Katoliki huko Leuven, Ubelgiji, na miaka mitatu baadaye alijiunga na Shirika la Yesu.
Alipata upadrisho huko Paris, Ufaransa, mwaka 1610. Akifanya uchungaji huko Rouen, Normandy, aliomba mara kadhaa kutumwa Glasgow (ingawa tangu mwaka 1560 huko Uskoti ilikuwa marufuku kutetea Ukatoliki).[1]
Alipokosa msaada huko, alikwenda London, Uingereza, tena Paris, na mnamo Novemba 1613 akarudi Uskoti akijidai ni mfanyabiashara na kutumia jina la John Watson. Kumbe alianza kufanya utume kwa bidii akihubiri na kusoma Misa kwa siri hadi Oktoba 1614, alipofungwa gerezani chini ya mfalme James VI.
Hatimaye alinyongwa na kukatwa vipandevipande.[2]
Alitangazwa mwenye heri mwaka 1929 na mtakatifu mwaka 1976.[3]
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ "Patron Saints Index: Saint John Ogilvie". 15 Januari 2009. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 15 Januari 2009. Iliwekwa mnamo 14 Mei 2017.
{{cite web}}
: Unknown parameter|deadurl=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - ↑ "10. mars: Den hellige John Ogilvie (~1580-1615)". 13 Machi 2010. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 Machi 2010. Iliwekwa mnamo 14 Mei 2017.
{{cite web}}
: Unknown parameter|deadurl=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - ↑ "Irondequoit Catholic Communities - - John Ogilvie". 11 Oktoba 2008. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Oktoba 2008. Iliwekwa mnamo 14 Mei 2017.
{{cite web}}
: Unknown parameter|deadurl=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - ↑ Martyrologium Romanum
Viungo vya nje
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |