Waraka wa pili wa Petro
Waraka wa pili wa Petro ni kimojawapo kati ya vitabu 27 vya Agano Jipya katika Biblia ya Kikristo.
Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.
Mwandishi
haririSiku hizi wataalamu wanakubaliana kukanusha barua hiyo kuwa imeandikwa kweli na Mtume Petro, wakisema ni kitabu cha mwisho kuandikwa katika Agano Jipya (labda huko Roma mwaka 100 hivi B.K.).
Kwa hakika iliandikwa baada ya waraka wa Yuda, kwa sababu inatumia maneno yake mengi.
Inawezekana mwandishi alitumia vilevile maneno ya Petro ambayo sasa yamepotea; kwa vyovyote aliandika kwa mamlaka yake kwa makanisa yote ili kuthibitisha mapokeo.
Mada
haririPamoja na kupinga uzushi, lengo la barua ni kueleza sababu gani Bwana anachelewa kurudi.
Mafundisho mengine muhimu yaliyomo yanahusu uvuvio wa Roho Mtakatifu juu ya waandishi wa Biblia (Paulo mmojawao), wito wetu wa kushiriki umungu, uwepo wa ulimwengu mpya baada ya huu wa sasa kuangamizwa (2Pet 1:3-11,19 21; 3:8-18).
Marejeo
hariri- Adams, Thomas B. "A Commentary on the Second Epistle General of Second Peter" Soli Deo Gloria Ministries, 1990. ISBN 978-1-877611-24-7
- Green, Michael. "The Second Epistle of Peter and The Epistle of Jude: An Introduction and Commentary" Wm. B. Eerdmans Publishing Company, 2007. ISBN 978-0-8308-2997-2
- Leithart, Peter J. "The Promise Of His Appearing: An Exposition Of Second Peter" Canon Press, 2004. ISBN 978-1-59128-026-2
- Lillie, John. "Lectures on the First and Second Epistles of Peter" Klock & Klock Christian Pub, 1978. ISBN 978-0-86524-116-9
- Seton, Bernard E. "Meet Pastor Peter: Studies in Peter's second epistle" Review and Herald Pub. Association, 1985. ISBN 978-0-8280-0290-5
Viungo vya nje
haririTafsiri ya Kiswahili
haririVinginevyo
hariri- Christian Classics Ethereal Library
- A sizeable article giving an overview of the problems with, and ultimately a defense of, the authenticity of 2 Peter Ilihifadhiwa 28 Machi 2007 kwenye Wayback Machine.
- "Epistles of Saint Peter". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.
Makala hii kuhusu mambo ya Agano Jipya bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Waraka wa pili wa Petro kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |