Agnes wa Asizi
Agnes wa Asizi (Assisi, 1197 au 1198 - Assisi, 16 Novemba 1253) alikuwa mdogo wa kwanza wa Klara wa Asizi.
Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu bikira. Papa Benedikto XIV alithibitisha heshima hiyo tarehe 6 Novemba 1751, akiruhusu Wafransisko kuadhimisha sikukuu yake kila tarehe 16 Novemba.
Maisha
haririAlikuwa binti wa pili kati ya watatu wa Favarone wa Offreduccio Scifi; mama yake Ortolana alikuwa wa ukoo wa kisharifu wa Fiumi na binamu yake Rufino ni mmojawapo kati ya wenzi watatu wa Fransisko wa Asizi.
Akiwa na umri wa miaka 15 tu, alimfuata dada yake Klara wiki mbili tu baada ya huyo kukimbia nyumbani (18 Machi 1212) ili atawe nyuma ya Fransisko, mwanzilishi wa Ndugu Wadogo. Pamoja, walishinda upinzani mkali wa baba yao na ndugu wengine ili kushika kwa moyo wote ufukara mkuu walivyoelekezwa na Fransisko [1].
Ndipo Fransisko alipowahamishia kwenye kikanisa cha San Damiano nje kidogo ya Assisi ambacho alikuwa amekarabati kwa mikono yake.
Baada ya wanawake wengine kujiunga, monasteri yao ikawa asili ya Utawa wa Mt. Klara.
Mwaka 1219 Agnes aliteuliwa na Fransisko kuwa abesi wa monasteri ya Monticelli, karibu na Firenze, ambayo ikazaa monasteri nyingine Italia kaskazini, kama vile Mantova, Venezia na Padova.
Mwaka 1253 Agnes alirudishwa San Damiano wakati wa kihoro cha dada yake, akamtumikia hadi mwisho.
Mwaka huohuo, mwenyewe alifariki, tarehe 16 Novemba.
Kwa wakati huo mama yao Ortolana, na mdogo wao Beatrice, walikuwa wameshafariki katika monasteri hiyohiyo.
Masalia ya Agnes yanatunzwa katika Basilika la Mt. Klara mjini Assisi, yalipohamishiwa pamoja na yale ya Waklara wote wa kwanza.
Tazama pia
haririTanbihi
haririMarejeo
hariri- Bartoli, Marco. Chiara d'Assisi. Rome 1989: Instituto Storico dei Cappuccini.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |