Akwila na Priska
Akwila na Priska (au Akula na Prisila) walikuwa mume na mke Wayahudi wa Ponto (leo nchini Uturuki) katika karne ya 1 BK.
Ni maarufu katika vitabu 4 vya Biblia ya Kikristo kama jozi iliyopokea mikusanyiko ya Wakristo nyumbani na kufanya kazi ya umisionari katika miji na nchi mbalimbali, kama vile Korintho na Efeso, baada ya kufukuzwa na Kaisari Klaudio wakiwa pamoja na Wayahudi wote wa jiji la Roma (mwaka 49).
Wakati huo walikuwa Wakristo tayari (Mdo 18:2-3).
Huko Korintho walianza kushirikiana na Mtume Paulo (Mdo 18:18) aliyewataja kila mara kwa heshima na shukrani kubwa, pia kwa sababu walihatarisha uhai wao ili kumuokoa huko Efeso (1Kor 16:19; Rom 16:4; 2Tim 4:19)[1].
Baadaye walirudi Roma kwa muda, labda mpaka Kaisari Nero alipoanza kudhulumu Kanisa. Hapo wakarudi Efeso.
Kati ya watu walioinjilishwa nao, muhimu zaidi ni Apolo, Myahudi msomi wa Aleksandria, Misri (Mdo 18:36).
Wanaheshimiwa na madhehebu mengi kama watakatifu. Kama vile Agano Jipya linawataja daima pamoja, sikukuu yao inawaadhimisha daima kwa pamoja ingawa tarehe ni tofautitofauti, kadiri ya madhehebu. Kwa Wakatoliki ni hasa tarehe 8 Julai[2].
Tazama pia
haririTanbihi
haririViungo vya nje
hariri- Saints Aquila and Priscilla Ilihifadhiwa 28 Februari 2016 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Akwila na Priska kama habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |