Amarna
Eneo la Amarna (hujulikana zaidi kama el-Amarna au mara nyingine hukosewa na kuitwa Tel el-Amarna; kwa Kiarabu: العمارنة al-‘amārnah) lipo katika kingo za Mto Nile katika Misri ya sasa katika mkoa wa Minya. Lipo kiasi cha kilomita 5858 kusini mwa mji wa al-Minya na kilomita 312 au kiasi cha maili 194 kusini mwa mji mkuu wa Misri Cairo na km 402 kaskazini mwa Luxor.[1] Eneo la Amarna linajumuisha vijiji kadhaa vya kisasa kama vile el-Till kwa upande wa kaskazini na el-Hagg Qandil kwa upande wa kusini.
Amarna | |
Location in Egypt |
|
Majiranukta: 27°39′42″N 30°54′20″E / 27.66167°N 30.90556°E | |
Country | Egypt |
---|---|
Governorate | Minya Governorate |
EST | (UTC+2) |
- Summer (DST) | +3 (UTC) |
Katika eneo hili pia kuna makumbusho makubwa ya Misri ambayo yanajumuisha mabaki ya mji mkuu wa zamani, uliojengwa upya na Farao Akhenaten wa kipindi cha nasaba ya kumi na nane (1353 hivi) na kuachwa muda mfupi baadae. Akhenaten alijenga mji huo alipojaribu kubadilisha dini ya Misri kuelekea ibada ya mungu mmoja tu aliyekuwa Aten au Jua.[2] Jina la mji huo lililotungwa na Wamisri linaandikwa hivi, Akhetaten (or Akhetaton – tafsiri inabadilika katika lugha mbalimbali, katika lugha ya Kiingereza, tafsiri ya Akhetaten inamaanisha "Horizon ya Aten."[3]
Eneo hili pia limeshawahi kukaliwa na Wakristu kutoka Roma na wengineo na katika kipindi cha kuhama eneo hili, waliacha masalia mbalimbali.[4]
Jiji la Akhentaten
haririEneo la mji huu, halijawahi kuhamiwa na watu wengi, na ndio mji ambao Akhenaten aliuelezea kama Aten
"..sehemu ya kwanza, ambayo aliifanya akijua kuwa atakuja kukaa hapo,"
Inawezekana kuwa, familia ya kifalme ililipenda eneo hili, na pia kuamini kuwa, hili ndilo sehemu ya kuishi na kuanzisha mji katika eneo hili.
Mji huo ulijengwa kama mji mpya wa Farao Akhenaten, na kuutoa kwa ajili ya dini na imani yake mpya ya Aten. Ujenzi ulianza kiasi cha miaka mitano ya uongozi wake (1346 KK) na unadhaniwa ulimalizika baada ya miaka tisa (1341 KK) japokuwa ulikua mji miaka miwili kabla. Kurahisisha ujenzi, majengo mengi katika mji huu, yamejengwa kwa kutumia miti na matope na kupakwa rangi nyeupe, wakati majengo yaliyokuwa ya muhimu yalijengwa kwa kutumia mawe.[5]
Huu ni mji pekee nchini Misri unaotunza sehemu kubwa ya michoro yake ya ndani kwa sehemu kubwa, hii inawezekana ni kutokana na mji huu kutelekezwa baada ya kifo cha Akhenaten. Mji huu unaonekana ulibakia imara kwa kipindi cha karne moja au zaidi hata baada ya kifo chake,[6] baada ya mji huu kutelekezwa ulibaki bila kuhamiwa na mtu hadi Wakristo kutoka Roma walipokuja na kuanzisha makazi yao [4] karibu katika maeneo ya pembezoni mwa Mto Nile.
Sehemu na Kupanga
haririUkiwa katika kingo za Mto nile, kwa upande wa Mashariki, mabaki ya mji huu yapo katika sehemu mbalimbali, kaskazini na Kusini hususani katika barabara za kifalme. Ambayo hivi sasa yanaitwa 'Sikhet es-Sultan'.[7][8] The Royal residences are generally to the north, in what is known as the North City, na kuwa na kituo cha utawala na shughuli za kidini, na katika upande wa kusini mwa mji huu, kuna makazi ya watu.
Mji wa Kaskazini
haririEneo la kaskazini mwa mji ni sehemu yenye nyumba na mahekalu ya kifalme, na ndio makazi kwa familia za kifalme. Wakati upande wa kasakazini uaendelea kupungua ukubwa na wingi kwa nyumba nzuri. Hii ikiwa ni kulingana na mji wenyewe ulivyo.[8]
Katikati ya Mji
haririMajengo muhimu ya sherehe na utawala yapo katika eneo la katikati ya mji. Hekalu la Aten na hekalu dogo la Aten, yalikuwa yanatumika kwa ajili ya shughuli za kidini, na kati ya hekalu la Great Royal Palace na Royal Residence yalikuwa yakitumika kwa shughuli za sherehe kwa ajili ya familia za kifalme naitajiri na zilikuwa zikiunganishwa na daraja..[9] [10]
Hili pengine ndili eneo la kwanza kuwahi kumalizika na lilijengwa kwa awamu mbili.[7]
Kando ya kiunga cha Kusini
haririEneo la kusini, lilikuwa ni eneoe ambalo hii leo linajulikana kama, Southern Suburbs' yaani viunga vya kando upande wa kusini. Eneo hili lina nyumba kubwa kwa ajili ya makazi ya familia tajiri. Kama vie. Nahkt (waziri mkuu, ), Renefer (General), Panehesy (High Priest of the Aten) and Ramose (Master of Horses). This area also aliyekuwa akimiliki studia ya kuchongea michoro katika mawe. Thutmose, ambapo michoro yenye umbo la moyo ilipatikana iliyokuwa ikimilikiwa na hii ikiwa ni mwaka 1912.[11]
Kwa upande wa Kusini kwenda mbele katika mji huu, kulikuwa na eneo la Kom el-Nana, eneo lililofungiwa na lililikuwa likijulikana kama sun-shade, na pengine lilijengwa kama vile hakalu la sun-temple.[12], na pia Maru-Aten, ilikuwa ndilo hekalu mbalo asili yake lilidhaniwa kutengenezwa kwa ajili ya malkia wa Akhenaten aliyeitwa Kiya,lakini baada ya kifo chake, jina na picha zake vilibadilishwa nay ale ya motto wake wa Meritaten,.[13].
Sanaa ya Amarna
haririSanaa ya eneo la Amarna ni ya kipekee katika sanaa nyingi zinazopatina katika ncgi ya Misri . Hii ni kutokana na uwezo wao mkubwa wa kuchora kwa kuonesha uhalisia wa hali halisi ya michoro. Hii ikiwa ni pamoja na kuonesha hali halisi ya michoro mbalimbali kama vile ya familia za Kifalme wakiwa na watoto wao.Japokuwa imani katika eneo la Aten iliwahi kuangushwa kabisa lakini sanaa katika eneo hili bado inaonesha kuwa na nguvu sana. Hii ikiwa ni pamoja na kuonesha picha halisi za wanawake zikiwa zenye kung’aa kuliko za wanaume. Sanaa hii pia hujuisha uchoraji wa katuni.
Kugunduliwa mara ya pili
haririKwa mara ya kwanza, jina hili lilitajwa mwaka 1714, na Claude Sicard, mfaransa aliyekuwa mafausi wa Yesu, abaye alikuwa akisafiri katika fukwe za Mto Nile na bonde la Mto huo, katika mipaka ya Stela kutokea katika eneo la Amarna. Na kutokana na watu wengi kutembelea katika nchi ya Misri pia watu kadhaa walikuwa wakitembelea katika eneo hili,. Vikosi vya Napoleon, mwaka 1798. 1799 walitengeneza ramani ya kwanza ya Armana ambayo baadae ilikuja kuchaishwa na kati ya mwaka 1821 na 1830.[14]
Mwaka 1887, mwanamke wa kijijini alikua akilima na kugundua kugae chenye umri wa zaidi ya miaka 300[15]
Mwaka 1891 na 1892, Alessandro Barsanti aligumndua kaburi la Mfalme (japo lilikuwa likijulikana na wakazi wa eneo hilo tangu mwaka 1880).[16]
Kuna wakati kipindi cha Sir Flinders Petrie aliwahi kufanya kazi katika eneo kwa kipindi kimoja t Amarna, alifanya kazi yeye binafsi katika eneo Egypt Exploration Fund. Alianzia katika machimbo ya ya katika ya mji, akijaribu kupeleleza kuhusu hekalu kubwa zaidi la Aten, na nyumba mbalimbali za kifalme ikiwa ni pamoja na makazi ya Farao.Katika hatua mbalimbali alikuwa akifanikiwa kupata mabaki vya vigae na vyombo mbalimbali vya ndaniref name="grundon9091"/> Baada ya kuchapa matokeo ya tafiti zake, Petrie aliweza kuhamasisha watu zaidi kujiunga katika kufanya pelelezi katika maeneo mbalimbali.
Tanbihi
hariri- ↑ "Google Maps Satellite image". Google. Iliwekwa mnamo 2008-10-01.
- ↑ "The Official Website of the Amarna Project". Iliwekwa mnamo 2008-10-01.
- ↑ David (1998), p.125
- ↑ 4.0 4.1 "Middle Egypt Survey Project 2006". Amarna Project. 2006. Iliwekwa mnamo 2007-06-06.
- ↑ Grundon (2007), p.89
- ↑ "Excavating Amarna". Archaeology.org. 2006-09-27. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-07-11. Iliwekwa mnamo 2007-06-06.
- ↑ 7.0 7.1 Waterson (1999), p.81
- ↑ 8.0 8.1 Grundon (2007), p.92
- ↑ Waterson (1999), p.82
- ↑ Moran (1992), p.xiv
- ↑ Waterson (1999), p.138
- ↑ "Kom El-Nana". Iliwekwa mnamo 2008-10-04.
- ↑ Eyma (2003), p.53
- ↑ "Mapping Amarna". Iliwekwa mnamo 2008-10-01.
- ↑ "Wallis Budge describes the discovery of the Amarna tablets". Iliwekwa mnamo 2008-10-01.
- ↑ "Royal Tomb". The Amarna Project. Iliwekwa mnamo 2008-10-01.
Marejeo
hariri- Redford, Donald (1984). Akhenaten : The Heretic King. Princeton.
- David, Rosalie (1998). Handbook to Life in Ancient Egypt. Facts on File Inc.
- Moran, William L. (1992). The Amarna Letters. Baltimore: Johns Hopkins University Press. ISBN 0-8018-4251-4.
- Aldred, Cyril (1988). Akhenaten, King of Egypt. Thames & Hudson.
- Grundon, Imogen (2007). The Rash Adventurer, A Life of John Pendlebury. London: Libri.
- de Garis Davies, Norman (1903–1908). The Rock Tombs of El Amarna. Part 1-6. London: EES.
{{cite book}}
: CS1 maint: date format (link) - Martin, G.T. (1974, 1989). The Royal Tomb at el-'Amarna, 2 vols. London: EES.
{{cite book}}
: Check date values in:|year=
(help) - Aayko Eyma ed., A Delta-Man in Yebu, Universal-Publishers. 2003
- Waterson, Barbara (1999). Amarna: Ancient Egypt's Age of Revolution.
Viungo vya nje
hariri- The University of Cambridge's Amarna Project
- Amarna Art Gallery Shows just a few, but stunning, examples of the art of the Amarna period.
- M.A. Mansoor Amarna Collection