Aten (pia Aton) ni jina la Jua lililoabudiwa kama mmoja kati ya miungu mingi nchini Misri, hasa wakati wa Farao Akhenaten. Mungu aliyeabudiwa kwa umbo la Jua nchini Misri tangu kale alikuwa Ra. Kiasili Aten alikuwa duara ya Jua tu inayoonekana angani, ikachukuliwa kama ishara ya Ra au sura yake mojawapo. Aten aliitwa mwanzoni "jicho la Ra" na baadaye "kiti cha Ra". Aten alichorwa kama duara pamoja na miale iliyoishia katika mikono.

Farao Akhenaten na malkia Nefertiti wakiabudu Aten.
Aten.

Polepole wakati ibada za Aten yenyewe zilipoanza na chini ya Farao Amenhotep III (1386 KK hadi 1349 KK) Aten aliabudiwa akionyeshwa kama binadamu mwenye kichwa cha ndege kozi, sawa na picha za Ra. Mwanawe Amenhotep IV, aliyebadilisha jina lake baadaye kuwa Akhenaten, alikuwa mungu pekee aliyeabudiwa na mfalme na kwa niaba ya serikali yake. Akhenaten alibadilisha pia namna ya kumwonyesha akitumia duara yenye miale pekee.

Kuna shairi lililotambuliwa katika kaburi moja la nyakati zile ambamo Akhenaten anamsifu Aten kama muumbaji, na asili ya uhai.

Ibada ya Aten ilifutwa na Farao Horemheb.

Marejeo

hariri

Viungo vya Nje

hariri