Anthony Banzi
Anthony Banzi (Mangoja, Parokia ya Tawa, mkoa wa Morogoro, 28 Oktoba 1946 - Dar es Salaam, 20 Desemba 2020) alikuwa askofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania.
Aliwekwa wakfu na Kardinali Polycarp Pengo mwaka 1994. Tangu mwaka huo hadi kifo chake alikuwa askofu wa Jimbo la Tanga.
Maisha
haririAlipata elimu ya msingi katika shule ya msingi ya Lukenga. Mwaka 1960 alijiunga na Seminari ndogo ya Mt. Peter, Bagamoyo, na baadaye Seminari ndogo ya Mt. Charles huko Itaga kuanzia mwaka 1965 hadi 1967.
Mwaka 1968-1969 alijiunga na Seminari Kuu ya Kibosho kwa masomo ya Falsafa na baadaye Seminari kuu ya Kipalapala kwa masomo ya Teolojia kuanzia mwaka 1970 hadi 1973.
Alipewa daraja takatifu ya upadre tarehe 29 Julai 1973.
Alifanya kazi kama paroko msaidizi katika parokia za Mlali, Msongozi, Mtombozi, Matombo na kama Paroko katika Parokia ya Maskati.
Mwaka 1976 alifanya kazi kama mhasibu mkuu wa Seminari kuu ya Ntungamo, Bukoba.
Miaka 1976 - 1981 alikwenda Austria (Ulaya) kwa masomo zaidi, ambapo alitunikiwa shahada ya udaktari (Ph.D).
Kuanzia mwaka 1981 hadi 1982 alikuwa Chaplain wa Hospitali ya Turiani na pia paroko wa parokia ya Mandera.
Miaka 1981 - 1985 alikuwa Mhasibu mkuu wa Jimbo Katoliki la Morogoro.
Miaka 1985 - 1987 alikuwa Chaplain wa Sekondari ya Bigwa, Morogoro.
Miaka 1988 - 1991 alikuwa Gombera wa Seminari kuu ya Ntungamo.
Mwaka 1992 Padre Anthony Banzi aliteuliwa kuwa Gombera wa Seminari kuu ya Kibosho, Moshi, ambapo alifanya kazi mapaka alipoteuliwa kuwa Askofu wa Jimbo katoliki la Tanga tarehe 24 Juni 1994 na kuwekwa wakfu tarehe 15 Septemba 1994.
Viungo vya nje
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |