Bustani ya Edeni (kwa Kiebrania: גַּן־עֵדֶן gan-'Ēḏen) inatajwa katika Kitabu cha Mwanzo cha Biblia kama bustani nzuri iliyopandwa na Mungu alipowaweka Adamu na Hawa baada ya uumbaji wa hao watu wa kwanza.

Bustani ya Edeni na Anguko la Binadamu, taswira ya Jan Brueghel Mzee na Pieter Paul Rubens, c. 1615

Katika tafsiri ya Kigiriki ya Biblia jina hilo lilitajwa kama "Paradiso" (παράδεισος paradeisos) kutoka neno la Kiajemi cha Kale parādaiĵah) lililomaanisha eneo lililozungushwa kwa ukuta [1]. Katika lugha ya Kiajemi inaposemwa "Paradiso" kuwa na maana ya "Eneo lililozungushwa ukuta" dhana hiyo kimsingi humaanisha "Eneo la bustani" fulani ambapo iliyozungukwa na kingo za bustani kubwa ambayo kwa lugha ya Kisemitiki katika lahaja ya Kiebrania iliitwa "Edeni" ikiwa na maana ya bustani ya asili isiyolimwa na binadamu, yaani "Nyika". [2]

Inaelezwa katika Biblia kwenye vitabu vya Mwanzo 2-3 na Ezekieli 28 na 31. [3]

Hivyo basi, kimsingi Bustani ya Edeni ni eneo halisi la kijiografia, si hadithi tu kama idhaniwavyo na watu wengi wa kizazi cha sasa.

Mahali

hariri

Mahali pa Edeni panaelezewa katika Kitabu cha Mwanzo kama chanzo cha mito minne.

Maelezo ya Mwa. 2, 10-13 yanasema: 10 Ukatoka mto katika Edeni wa kuitilia bustani maji, na kutokea hapo ukagawanyika kuwa vichwa vinne. 11 Jina la wa kwanza ni Pishoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Havila, ambako kuna dhahabu; 12na dhahabu ya nchi ile ni njema; huko kuna bedola, na vito shoham. 13 Na jina la mto wa pili ni Gihoni; ndio unaozunguka nchi yote ya Kushi. 14 Na jina la mto wa tatu ni Hidekeli; ndio unaopita mbele ya Ashuru. Na mto wa nne ni Frati.

Lakini haiwezekani kutaja mahali maalum kwa maana, mbali na mito ya Frati na Hidekeli, mingine haijulikani, ila Gihoni inahisiwa kuwa Naili kwa kuwa inasemwa kwamba inazunguka nchi yote ya Kushi. Majaribio mbalimbali yamefanywa na wataalamu mbalimbali ila bila mapatano[4].

Makazi ya Adamu na Hawa

hariri

Biblia ya Kiebrania inawaonyesha Adamu na Hawa wakitembea kuzunguka bustani ya Edeni uchi kwa sababu ya kutokuwa na ubaya wa dhambi.

Edeni inatajwa pia katika sehemu nyingine za Biblia kama vile Mwanzo, [5] katika Isaya 51:3, [6] Ezekieli 36:35, [7] na Yoeli 2:3; [8] Zekaria 14 na Ezekieli 47 hutumia taswira ya paradiso bila kulitaja jina la Edeni.

Sehemu ya pili ya simulizi la uumbaji kwenye Biblia inaanza katika Mwanzo 2:4-3:24. Hapa YHWH - Elohim (inayotafsiriwa "BWANA Mungu") anamwumba mtu wa kwanza (Adamu) na kumweka katika bustani aliyoipanda “mashariki mwa Edeni”. "BWANA Mungu akachipusha katika ardhi kila mti unaotamanika kwa macho na kufaa kwa kuliwa; na mti wa uzima katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya." [9]

Mtu alikuwa huru kula matunda ya mti wowote wa bustani isipokuwa mti wa uzima na mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Mwisho wa yote, Mungu alimuumba mwanamke (Hawa) kutoka kwa ubavu wa mwanamume ili awe mwandamani wa mwanamume. Katika sura ya tatu, mwanamume na mwanamke walishawishiwa na nyoka kula matunda yaliyokatazwa, na walifukuzwa kutoka bustani ili kuwazuia kula matunda ya mti wa uzima, na hivyo kuishi milele. Makerubi waliwekwa mashariki mwa bustani, "na upanga wa moto uliogeuka huku na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima." [10]

Mtazamo wa Kiislamu

hariri

Katika Kurani, mahali wanapokwenda hao watakaokubaliwa na Allah huitwa "jannat" (جنات) yaani bustani. "Bustani" inatajwa mara kadhaa katika Kurani [11]. Katika mawazo ya Kiislamu hiyo bustani huwa na matabaka saba. Hapa majina ya Kiblia hutumiwa kwa namna tofauti kidogo.

Tabaka la saba na la juu ni "Firdausi" (فردوس) ambayo ni matamshi ya Kiarabu ya neno Paradiso[12]. Jina la Edeni linatumiwa kwa ajili ya "jannat adni" (جنات عدن)[13] ambayo ni tabaka la nne tu[14]. [15]

Marejeo

hariri
  1. Katika nchi yabisi za Mashariki ya Kati, hadi leo bustani ni eneo lililoviringishwa na ukuta kwa kusudi la kulinda mimea, matunda na maji dhidi ya wanyamapori na wezi. Linganisha Moynihan, Elizabeth; Paradise as a garden: in Persia and Mughal India, uk. 1; New York 1979 ISBN 9780807609316
  2. Atlasi Ya Ikolojia Na Utamaduni Wa Edeni Na Bustani Ya Edeni Katika Tanzania ISBN:978-9912-40-425-0
  3. Metzger, Bruce Manning; Coogan, Michael D (2004). The Oxford Guide To People And Places Of The Bible. Oxford University Press. uk. 62. ISBN 978-0-19-517610-0. Iliwekwa mnamo 22 Desemba 2012.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. Wilensky-Lanford, Brook (2012). Paradise Lust: Searching for the Garden of Eden. Grove Press. ISBN 9780802145840. paradise lust.
  5. Genesis 13:10:HE
  6. Isaiah 51:3:HE
  7. Ezekiel 36:35:HE
  8. Joel 2:3:HE
  9. Bible, Genesis 2:9:HE
  10. Bible Genesis 3:24:{{{3}}}
  11. Qur'an, 2:35, 7:19, 20:117, 61:12
  12. Kurani 23:11: " Ambao watairithi Pepo ya Firdausi, wadumu humo"
  13. Tafsiri ya Kurani kwa Kiswahili ya Sheikh Ali Muhsin Al Barwani haitumii neno "adn"; anatafsiri mara nyingi "bustani za milele" (Kurani 13:23, 18:31, 19:61 ) au "bustani za kudumu" (9:72), bustani za daima (98:8); Tarjuma ya "Al Muntakhab" katika tafsiri ya QUR'ANI TUKUFU imetafsiriwa Kiswahili na Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani]
  14. Jannat al-ʿadn
  15. Wheeler, Brannon Mecca and Eden: ritual, relics, and territory in Islam k. 16, 2006

Kujisomea

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.