Jumuiya ya Nchi Huru (kwa Kirusi: Содружество Независимых Государств (СНГ), sodrushestvo nezavisimikh gosudarstv (SNG); kwa Kiingereza: Commonwealth of Independent States (CIS)) ni jina la umoja wa nchi zilizokuwa sehemu za Umoja wa Kisovyeti hadi mwaka 1991.

Bendera ya Jumuiya ya Nchi Huru.
Nchi wanachama wa Jumuiya ya Nchi Huru;
zambarau: wanachama kamili;
zambarau nyeupe: wanachama wa kushirikishwa.

Jumuiya hiyo iliundwa tarehe 8 Desemba 1991 na viongozi wa Urusi, Belarusi na Ukraine.

Makao makuu yapo Minsk, mji mkuu wa Belarusi na wabunge hukutana Sankt Peterburg.

Wanachama

+ Nchi mwanachama wa kushirikishwa

+ Nchi zilizokuwa jamhuri za Umoja wa Kisovyeti zisizoshiriki katika jumuiya

Shabaha na hali ya jumuiya

Jumuiya ilianzishwa kama njia ya kuondoa Umoja wa Kisovyeti bila kuacha ushirikiano. Tangu kuundwa nchi wanachama zilitia sahihi mikataba na mapatano mengi lakini hali halisi umuhimu wa umoja huu umerudi nyuma. Marais hawakutani pamoja tangu miaka kadhaa.

Ukraine na Georgia zinaelekea kujiunga na Ulaya na kambi la magharibi pamoja na NATO na mwelekeo huo umeshasababisha ugomvi na Urusi. Moldavia vilevile inaimarisha uhusiano wake na Romania, ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya na NATO, kwa sababu Wamoldavia wengi huongea Kiromania.

Viungo vya Nje