Fransisko wa Paola

Fransisko wa Paola (kwa Kiitalia Francesco da Paola; 27 Machi 14162 Aprili 1507) alikuwa mtawa nchini Italia.

Franziskus von Paola.jpg

Ametambuliwa na Kanisa Katoliki chini ya Papa Leo X kuwa mtakatifu kuanzia mwaka 1519.

Tarehe ya kifo chake, yaani 2 Aprili, pia ni sikukuu yake[1].

MaishaEdit

Fransisko alizaliwa kwa muujiza katika mji wa Paola, mkoa wa Calabria, Italia, mwaka 1416. Wazazi wake walikuwa wamefikia uzee bila ya kuweza kuzaa, lakini walimuomba Fransisko wa Asizi na kuweka nadhiri kuwa mtoto wao ataitwa Fransisko. Ndipo walipojaliwa kuzaa.

Tangu utotoni alishika maisha magumu ya sala na toba upwekeni.

Alianzisha shirika la watawa wakaa-pweke, ambalo baadaye likawa Utawa wa Wadogo Kabisa, likapata kibali kutoka kwa Papa mwaka 1506. Pamoja na kuahidi mashauri ya Kiinjili matatu ya kawaida, wanaahidi pia kuishi daima kwa toba kama wakati wa Kwaresima.

Kanuni yake ni ya pekee, ingawa inafuata kwa jumla ile ya Ndugu Wadogo ikiiongezea malipizi makali ya mababu wa jangwani.

Kaulimbiu yake ilikuwa neno "caritas" (kwa Kilatini, "upendo").

Fransisko alikufa mwaka 1507 huko Tours, Ufaransa alipokuwa ametumwa na Papa.

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

MarejeoEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.