Kasanga (Kalambo)
Kasanga ni mji mdogo kwenye Wilaya ya Kalambo, upande wa Kusini-Magharibi wa Tanzania, mwambaoni kwa Ziwa Tanganyika. Ilikuwa na jina la Bismarckburg wakati wa ukoloni wa Wajerumani.
Kasanga (Bismarckburg) |
|
Mahali pa Kasanga katika Tanzania |
|
Majiranukta: 8°27′21″S 31°8′12″E / 8.45583°S 31.13667°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Rukwa |
Wilaya | Wilaya ya Kalambo |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 13,281 |
Wakazi
haririKatika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 13,281 [1]. Kata ya Kasanga kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 ilikuwa na jumla ya watu 18,527 ikiwa na vijiji saba ambavyo ni Samazi watu 4,286, Kipanga watu 2,454, Kipwa watu 1,432, Kapare watu 1,659, Kilewani watu 3,342, Muzi watu 2,051 na kijiji cha Kasanga chenye watu 3,303. [2]
Mawasiliano
haririKasanga iko umbali wa kilomita 67 kutoka makao makuu ya Wilaya ya Kalambo ambayo yanajengwa katika mji mdogo wa Matai.
Kuna mpango wa kuunganisha Mkoa wa Rukwa - Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na hivyo serikali ya Tanzania inajenga barabara ya lami kuelekea Kasanga na kuna mpango pia wa kupanua bandari ya Kasanga ili kuwezesha meli kubwa kufanya safari zake kati ya DRC na Tanzania.
Mpango huo unaikuza Kasanga katika nyanja za ukuaji kimji na kuboresha biashara ya samaki ambayo ndiyo biashara kubwa kwa uchumi wa Kasanga na maeneo ya jirani ya vijiji vya Muzi, Kawala na Kapozwa.
Biashara
haririKasanga pia inakuwa mlango wa kukuza utalii kwa Bismarck na maporomoko ya Kalambo yaliyoko Kapozwa (Kisumba) umbali wa kilomita 36 kwa barabara kutoka Kasanga. Maporomoko ya Kalambo yamekuwa maarufu sana kwa upande wa Zambia na hivi sasa kuna mpango thabiti kuyafanya yafikike na kutangazwa kwa upande wa Tanzania.
Kwa hivi sasa Kasanga kumejengwa soko la samaki ambalo kwa lugha ya waliogharimia ujenzi huo linaitwa soko la kimataifa la samaki Kasanga. Kuna mpango wa kufunga vyumba baridi vya kuhifadhia samaki. Kasanga na Muzi vijiji vilivyo jirani vitanufaika sana na mpango wa kuunganisha DRC na Tanzania kwa njia ya bandari na mizigo mingi itapita njia hii. Uchumi wa eneo hili utakua kwa kasi kutokana na kufunguka kwa biashara kati ya nchi hizi mbili.
Historia
haririWakati wa koloni la Afrika ya Mashariki ya Kijerumani Kasanga ilikuwa makao makuu ya utawala wa Wajerumani kusini mwa Ziwa Tanganyika. Mnamo mwaka 1898 kapteni von Prittwitz aliunda hapa kituo cha kijeshi kilichopokea jina la "Bismarcksburg" (kwa heshima ya chansela Mjerumani Otto von Bismarck) mnamo 1899. Sehemu ya kombania ya 6 ya jeshi la Schutztruppe ilikaa hapa na kituo hiki kilikuwa boma muhimu kati ya Ujiji na Neu-Langenburg (Tukuyu)[3]. Tangu 1907 ilikuwa ofisi ndogo (jer. Bezirksnebenstelle) ya Mkoa wa Ujiji. 1913 Bismarckburg ilipandishwa cheo kuwa makao makuu ya mkoa wa 12 wa koloni ikawa mji mkuu wa mkoa uliokuwa mkubwa wa pili katika Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Mkoa wa Bismarckburg ulijumlisha maeneo ya Ufipa, Ukonongo, Ugala na Uwende.
Baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia jina la Kijerumani lilibadilishwa na Waingereza kuwa Kasanga.
Marejeo
hariri- ↑ https://www.nbs.go.tz, uk 149
- ↑ Sensa ya 2012, Rukwa – Kalambo District Council
- ↑ F.T. Krell: BISMARCKBURG - TWO FAMOUS COLLECTING LOCALITIES IN AFRICA, ENTOMOLOGIST'S MONTHLY MAGAZINE, 1994/03/31, imeangaliwa via researchgate.net
Kata za Wilaya ya Kalambo - Mkoa wa Rukwa - Tanzania | ||
---|---|---|
Kanyezi | Kasanga | Katazi | Katete | Kilesha | Kisumba | Legezamwendo | Lyowa | Mambwekenya | Mambwe Nkoswe | Matai | Mbuluma | Mkali | Mkowe | Mnamba | Mpombwe | Msanzi | Mwazye | Mwimbi | Samazi | Sopa | Sundu | Ulumi |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Rukwa bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Kasanga (Kalambo) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |