Kifimbo
Kifimbo wa kawaida (Albula vulpes)
Kifimbo wa kawaida (Albula vulpes)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Actinopterygii
Oda: Albuliformes
Familia: Albulidae
Bleeker, 1859
Jenasi: Albula
Scopoli, 1777
Ngazi za chini

Spishi 11 zilizopo:

Vifimbo, chache, minyimbi, manyimbi, manyimbwi, mkizi waume au panya ni samaki wa baharini katika jenasi Albula ya familia Albulidae.

Kifimbo wa pwani za Afrika ya Mashariki ni mkubwa kuliko spishi zote nyingine na ana uzito wa kipeo wa kg 10.0 na urefu wa sm 104. Spishi nyingine ni sm 25-50 kwa kipeo. Rangi yao ni ya fedha kwenye mbavu na kijivu hadi kijani-zaituni mgongoni. Kijivu kwenye magamba huunda mistari myanana myembamba mara nyingi ambayo hunyumbuka urefu wa mbavu kutoka kwa matamvua mpaka mkia. Vitako vya mapezi mbavuni pengine ni njano.

Mwenendo

hariri

Spishi hizi huishi maji ya kitropiki karibu na pwani na huenda kwenye pwa-tope ili kujilisha wakati wa maji maundifu. Samaki wazima na wachanga wanaweza kuwa pamoja katika makundi, na wanaweza kupatikana kwa peke yao au kwa jozi.

Vifimbo hula nyungunyungu-bahari, samaki wachanga, gegereka na moluska. Miamba, magenge na vitalu safi vya nyasi-bahari ina mawindo madogo tele kama vile kaa na uduvi. Wanaweza kufuata shepwa ili kukamata wanyama wadogo wanaowafukuza kutoka kwenye mchanga wa sakafu.

Vifimbo na binadamu

hariri

Uvuvi wa vifimbo kwa kutumia chambo cha nzi bandia ni mchezo maarufu katika Bahamas na kusini mwa Florida. Zamani uvuvi huu ulikuwa maarufu kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki pia lakini siku hizi vifimbo wamekuwa nadra. Kwa sababu vifimbo huishi katika maji kame ya pwani, uvuvi unaweza kufanywa kwa kutembea kwenye maji au kutoka mashua yasiyoingia maji sana. Uvuvi huu unafanyika kwa ajili ya michezo kwa kawaida, kwa hivyo samaki huachwa, lakini wanaweza kuliwa pia. Mapishi ya mfano ni samaki aliyegawanyika na kukolewa na mchuzi wa pilipili na chumvi halafu kuokwa.

Spishi za Afrika

hariri

Spishi za mabara mengine

hariri

Spishi za kabla ya historia

hariri
  • Albula bartonensis
  • Albula bashiana
  • Albula campaniana
  • Albula dunklei
  • Albula eppsi
  • Albula oweni

Marejeo

hariri
  • Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
  • Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.