Kinga wa Hungaria au wa Polandi (pia Kunegunda, Kunigunda, Kioga, Zinga; Esztergom, Hungaria, 5 Machi 122424 Julai 1292) alikuwa malkia, binti mfalme Bela IV wa Hungaria, na mke wa Boleslao V wa Polandi.[1]

Mt. Kinga.

Familia yake asili ilizaa watakatifu mbalimbali, yeye akiwa mmojawapo. Katika ndoa yake inasadikika kwamba waliishi kama kaka na dada, ingawa mwanzoni mumewe hakupenda[2].

Pamoja na hayo, Kinga alijitahidi sana kuwatendea kwa huruma mafukara na wagonjwa, wakiwemo wakoma.

Alipofiwa mumewe (1279), aliuza mali yake yote na kugawa mapato yote kwa maskini.

Halafu alikataa madaraka yake ya kiserikali akajiunga na monasteri ya Waklara aliyokuwa ameianzisha huko Sandec (Stary Sącz), alipoishi hadi mwisho katika sala tu, asipotaka kabisa itajwe asili yake.

Papa Aleksanda VIII alimtangaza mwenye heri mwaka 1690. Halafu Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu tarehe 16 Juni 1999.

Tangu mwaka 1695 anaheshimiwa kama msimamizi wa Polandi na Lithuania.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 24 Julai[3].

Tazama pia

hariri

Tanbihi

hariri
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.