Liberati, Bonifasi na wenzao

Liberati, Bonifasi na wenzao Servyo, Rustiko, Rogati, Setimo na Masimo (walifariki Karthago, leo nchini Tunisia, 484) walikuwa wamonaki wa Kanisa Katoliki huko Gafsa waliouawa kikatili na Wavandali, wakati wa utawala wa mfalme Huneriki aliyekuwa Mwario, kwa sababu ya kuungama imani sahihi na umoja wa ubatizo. Watesi wao, baada ya kujaribu kuwachoma moto juu ya mbao walipopigiliwa misumari, waliuawa kwa kupigwa kichwa kwa makasia.

Liberati alikuwa abati wao, Bonifasi shemasi, Servyo na Rustiko mashemasi wadogo na Masimo kijana wa miaka 15 aliyeamua kuuawa na jumuia yake ingawa angeweza kuachiliwa [1].

Tangu kale wanaheshimiwa kama watakatifu wafiadini. Papa Klementi X alithibitisha heshima hiyo tarehe 6 Juni 1671.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 2 Julai[2] [3], ila kwa Waaugustino ni 26 Agosti.

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.