Madhara ya kuvuta sigara

Mwili wa mvutaji sigara.

Madhara ya kuvuta sigara ni mengi na yamesambaa mwilini mwote. Sababu ni kuwa sigara ina kemikali zaidi ya 4,000 ambazo zina uwezo wa kudhuru afya ya binadamu. Hivyo kila sekunde nane, mtu mmoja hufariki kutokana na utumizi wa tumbaku.

Imebainika kuwa saba kati ya wavutaji sigara kumi, huanza uraibu huu wakiwa wangali watoto. Wanaoendelea kuvuta sigara kwa muda mrefu hufupisha maisha yao kwa miaka 20 hadi 25. Yafuatayo ni baadhi tu ya maradhi yatokanayo na uvutaji wa tumbaku.

Kung’oka kwa nyweleEdit

Uvutaji sigara hudhoofisha kinga ya mwili na kisha kudhuru mizizi ya nywele. Hii husababisha kung’oka kwa nywele mapema.

Magonjwa ya machoEdit

Wavutaji sigara hupata magonjwa ya macho mara nyingi kuliko wasiovuta. Sehemu ya macho inayopitisha mwangaza inaweza kufichwa kama vile wingu linavyoficha jua (yaani kwa ikimombo) na kusababisha upofu. Ugonjwa huu husababishwa kwa njia mbili. Kwanza moshi wa sigara huwasha macho na pili kemikali zilizomo ndani ya sigara hupita kwenye mishipa, damu na hatimaye kudhuru macho. Sigara pia husababisha kudhoofika kwa sehemu ya kati ya macho (retina) na hivyo kupunguza uwezo wa macho kuona vizuri na hata kutofautisha rangi (macular degeneration).

Kukunjana kwa ngoziEdit

Kemikali zinazopatikana ndani ya sigara hupunguza uwezo wa ngozi kujirekebisha hivi basi ngozi huzeeka haraka na kupoteza uwezo wa kulainika. Mvutaji wa sigara huonekana mzee kuliko umri wake haswa.

Magonjwa ya masikioEdit

Uvutaji sigara huleta magonjwa mengi ya masikio. Sababu ni kwamba uvutaji wa sigara hufanya uchafu ugande kwenye mishipa ya damu na hivyo kupunguza mwendo wa damu hadi kwenye sehemu za ndani za masikio. Moshi na kemikali za tumbaku pia hujeruhi sehemu za ndani za masikio na majeraha hayo yanaweza kuambukiza hata ubongo (menengitis). Yote haya yanaweza kusababisha uziwi.

Saratani ya ngoziEdit

Uvutaji sigara unasababisha saratani ya ngozi. Kemikali za sigara husababisha vidonda kwenye ngozi ambavyo haviponi kwa urahisi. Baada ya muda hugeuka kuwa saratani.

Magonjwa ya menoEdit

Sigara hutatiza mdomo na kuongeza uchafu unaoganda kwenye meno hivi kusababisha kuoza kwa meno, harufu mbaya mdomoni na uchafu wa meno. Sigara pia hutatiza kupona kwa vidonda, hasa baada ya kung’olewa kwa jino. Saratani ya mdomo na ulimi inapatikana zaidi kwa wavutaji sigara na watumiaji wa tumbaku za aina nyingine.

Magonjwa ya mapafuEdit

Uvutaji wa siagara ndio sababu kubwa zaidi ya saratani ya mapafu. Pia husababisha kupasuka kwa vibofu vya hewa safi na kutoa harufu mbaya mwilini. Wavutaji pia hupata saratani ya koromeo na kuziba njia ya hewa na hivyo basi inabidi kutobolewa kwa kishimo kwenye shingo ili kumwezesha mwathiriwa kupumua.

MifupaEdit

Sigara inasababisha mifupa kuwa myepesi na kupungukiwa nguvu. Sababu ni kuwa kemikali zilizomo ndani ya sigara hupunguza uwezo wa mwili kujenga mifupa iliyo na nguvu. Mifupa kama hii huvunjika kwa urahisi na kuchukua muda mrefu sana kupona (asilimia 80 zaidi ya mifupa ya kawaida).

Ugonjwa wa moyoEdit

Sigara ndiyo sababu kubwa zaidi ya magonjwa ya moyo. Inasababisha moyo kupiga kwa kasi zaidi na hivyo kuongeza msukumo wa damu mwilini (high blood pressure). Mwishowe husababisha mshtuko wa moyo na hata kifo. Kimoja kati ya vifo vitatu ulimwenguni hutokana na magonjwa ya moyo na huua zaidi ya watu milioni moja kwenye nchi za Afrika.

Vidonda vya tumboEdit

Sigara hupunguza uwezo wa mwili kujikinga dhidi ya viini vinavvyosababisha vidonda tumboni. Pia hupunguza uwezo wa tumbo kustahimili nguvu ya asidi baada ya kula. Vidonda vya mvutaji basi huwa vigumu kutibika, na mara nyingi hutokea tena baada ya kupona.

VidoleEdit

Kutu ya sigara hukusanyika na kuganda kwenye kucha na vidole vya mvutaji. Kisha hubadilisha rangi ya vidole na kucha kuwa za manjano au maji ya kunde. Ngozi ya vidole pia hukauka na kuwa ngumu sababu ya joto na kemikali za sigara.

WanawakeEdit

Sigara huongeza hatari ya kupata saratani ya mfuko wa uzazi (cancer of theuterus). Ni vigumu zaidi kwa mwanamke mvutaji sigara kupata mimba na ni rahisi sana kwake kuipoteza. (miscarrige). Uvutaji wa sigara pia humfanya mwanamke kumzaa mtoto aliyekufa (stillbirth) au aliye na uzito usiotimia wa kawaida. Watoto hao huwa na afya duni baadaye. Sababu ni kuwa kemikali za sigara hupunguza mwendo wa mtoto kukua akiwa angali mimbani. Sigara pia husababisha ugumba (menopause) kabla ya wakati wake. Sigara pia inaweza kumfanya mwanamke kuwa tasa.

WanaumeEdit

Sigara inapunguza mpigo wa damu kwenye sehemu za uume. Sigara pia huharibu mbegu za wanaume na kwa hiyo watoto wanaowazaa huwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kupata magonjwa ya saratani. Sigara pia huwafanya wanaume kuwa tasa.

Magonjwa ya ngoziEdit

Sigara huleta magonjwa mengi ya ngozi kama vile uvimbe, kuwashwawashwa na hudhoofisha hali ya ngozi.

Ugonjwa wa ‘Buerger’Edit

Huu ni ugonjwa wa uvimbe kwenye mishipa ya damu ya miguuni na mikononi. Mishipa hii huzibika na kuzuia mwendo wa damu kwenye sehemu zilizoathirika. Isipotibiwa kwa haraka, mvutaji anaweza kukatwa miguu au mikono.

SarataniEdit

Zaidi ya kemikali 40 zinazopatikana kwenye tumbaku zimethibitishwa kusababisha saratani. Ukilinganisha na asiyevuta sigara:

MapafuEdit

Mvutaji ana uwezekano wa mara 22 zaidi wa kupata saratani ya mapafu

PuaEdit

Mvutaji ana uwezekano wa mara 2 zaidi kupata saratani ya pua.

UlimiEdit

Mvutaji ana uwezekano wa mara 2 zaidi kupata saratani ya ulimi.

TumboEdit

Mvutaji ana uwezekano wa kupata saratani ya tumbo mara 3 zaidi.

FigoEdit

Mvutaji ana uwezekano wa kupata saratani ya figo mara 5 zaidi.

NyinginezoEdit

Uchunguzi unaonyesha kuwa saratani ya mdomo ni hadi mara 27, koo (mara 12), koromeo (mara 10).

Uchunguzi pia umebaini kuwa kuna uhusiano fulani kati ya uvutaji sigara na saratani ya matiti.

Tazama piaEdit

MarejeoEdit

  • The Smoker’s Body nakala ya 21 Julai-Agosti 1997.
  • Tafsiri ya National Agency for the Campaign Against Drug Abuse(NACADA)