Mboo au mboro (pia: uume) ni kiungo cha uzazi cha kiume ambacho hupitisha shahawa yenye mbegu kutoka mapumbu kupitia kifuko cha akiba kwa kuingizwa katika kuma.

Mboo pia hutumika kupitisha mkojo.

Muundo wa uume ni misuli aina ya sifongo yenye neva nyingi. Kukiwa na msisimko damu inajaa nafasi zilizomo na kusababisha uume utanuke na kusimama imara na wima.

Mabadiliko ya ubalehe

Ingawa kila mtu ni mwanamume au mwanamke tangu atungwe (kadiri alivyo na kromosomu Y au la), kabla ya kubalehe tofauti hazionekani sana, isipokuwa katika viungo vya uzazi. Baadaye muda hufika wa watoto kuanza kukomaa kijinsia: na tofauti hujitokeza wazi.

Kutoka utotoni kuingia utu uzima kuna mabadiliko ya haraka katika viungo, hisia na roho. Kama ilivyo kwa viumbe hai wote, ustawi huo unaweza ukawahi au kuchelewa, lakini kwa kawaida unatokea kati ya umri wa miaka 12 na 16. Wasichana wanawahi kuliko wavulana, na Wazungu kuliko Waafrika, lakini mabadiliko ni yaleyale, nayo yanafanyika hatua kwa hatua.

Katika hayo, mengine yanamfurahisha kijana, lakini mengine hayampendezi, anayonea aibu hata kuyafadhaikia hasa asipoyaelewa. Bila ya shaka anahitaji msaada wa walezi aweze kukabili hayo yote bila ya kuvurugika kiasi cha kupotoka.

Kwanza mvulana anajikuta akirefuka haraka na kupata misuli mikubwa; kifua kinapanuka. Papo hapo sauti yake inaanza kupasuka na kuwa nzito, ndevu zinaweza zikaota, na vilevile malaika sehemu za siri, kwapani na pengine kifuani. Hali ya ngozi inakuwa ikikwaruzakwaruza hasa usoni, na chunusi hujitokeza.

Katika hatua ya mbele mabadiliko yanahusu zaidi viungo vya uzazi vinavyokua na kuanza kazi ambayo kwa kawaida itaendelea moja kwa moja, kumbe kwa msichana itakoma kati ya miaka 40 na 50.

Mabadiliko ya mwili yanaendana na mengine ya nafsi yanayofanya tabia iwe tofauti na ile ya awali. Hisia zinabadilika kadiri mwili unavyozidi kutengeneza chachu (homoni) zinazomfanya kijana aelekee namna ya baba au mama zake.

Mvulana anajikuta akivutiwa na uzuri wa wasichana, na kupenda kuwajua zaidi, kuongea nao n.k. Anapenda kuwagombeza na kuwaonea ili aonyeshe uwezo na nguvu alivyonavyo. Katika hatua hiyo anakuwa mvivu na mzito katika kutembea na mara nyingi hajali unadhifu. Kumbe msichana anazidi kupenda sifa na kujiremba.

Akili pia inapevuka na kumfanya kijana apende kuwa na maoni maalumu kuhusu mambo mbalimbali, hata kubishana na wengine. Pia apende mabadiliko, ujuzi mpya n.k. Ndiyo sababu kijana si mwepesi kupokea mashauri na maoni ya wakubwa, asije akajisikia tena mtoto huku akipenda kutambulika amekuwa mtu mzima. Kwa ajili hiyo anatamani kufanya yale wanayoyafanya wakubwa (kuvuta sigara, kurudi nyumbani usiku n.k.), kushirikiana na rika lake na hata kujiunga na makundi ya wanaomzidi katika shughuli zao (genge, timu n.k.) ingawa pengine hazifai (uhuni, bangi n.k.).

Hatimaye kuna mabadiliko upande wa roho: kati ya mawazo mengine, kijana anajitafutia msimamo mpya kuhusu maswali makuu ya maisha: anataka kuwa na falsafa na dini yake. Shida ni kwamba usahihi wa majibu unategemea sana uadilifu wa maisha: kijana akifuata anasa, akili inapofuka na imani inapotea.

Mabadiliko ya viungo vya uzazi

Uume (mboo) wa mvulana unakua, lakini kwa kiasi tofauti kati ya mtu na mtu. Ni muhimu kila mmoja ajipokee alivyo hata katika kiungo hicho, bila ya kuhangaika wala kuona aibu kwa sababu, eti ni kidogo. Hata hivyo uume unaweza kukarabatiwa ili kuzidisha urefu au upana kwa njia tofautitofauti ikiwemo kufanyiwa operesheni, pampu za kuvuta[1], kundungwa sindano[2][3] na hata kutumia dawa za kumeza kama tembe au kupaka,[4] ingawa ukarabati huu umeibua hisia tofauti.

Kusimika kwa uume si jambo jipya kwa kuwa utotoni limeshatokea kawaida kutokana na kibofu kujaa mkojo. Ila sasa linaweza kutokea kwa sababu mpya, yaani jinsia.

Kusimika kunajitokeza na kupotea haraka kutegemeana na hali iliyopo. Hali hiyo inaweza kutokea bila ya mtu kutaka, kwa mfano usiku au pia mchana kati ya watu ikimfanya aone haya.

Kukosa kusimika kunaweza kuwa ishara ya ukosefu wa nguvu za kiume. Hali hii inaweza kusababishwa na mambo mengi ikiwemo maradhi, majeraha, utumizi wa dawa za kulevya, wingi wa mafuta mwilini, shinikizo la damu, tiba ya magonjwa kama vile saratani ya tezi kibofu na mengine mengi.[5] Ukosefu wa nguvu za kiume unaweza kutibiwa kwa njia tofauti kama vile kwa kutumia dawa mbalimbali za kuongeza nguvu za kiume.[6][7][8]

Upande wa maadili pengine tunahimizwa tusisababishe hali ya kusimika bila ya lengo jema, kama vile kumtibu mgonjwa, kutoa ushauri nasaha au kujielimisha kuhusu jinsia. Kwa hiyo tukwepe kwa kawaida yale yote yanayoweza kusisimua, kama vile mawazo, maneno, masomo, mitazamo na vitendo mbalimbali kuhusu jinsia. Mvulana anahitaji kujifunza nidhamu ya namna hiyo.

Mashauri mengine ni kutovaa kaptura wala suruali zinazobana, na kuficha kwa adabu hali hiyo ikitokea, lakini bila ya kuiogopa wala kudhani ni dhambi.

Mapumbu yanaanza kutengeneza mbegu za kibinadamu kwa wingi sana: hizo ni ndogondogo na zina umbo kama la viluwiluwi vya chura, yaani vina vichwa na mikia tu.

Vichwa ndivyo vinavyoleta viini vya urithi wa baba. Mikia kazi yake ni kusaidia tu kusukuma mbegu ndani ya tumbo la uzazi mpaka zikutane na kijiyai cha mama, halafu inapotea ndani ya kijiyai. Mbegu zikiwa tayari zinahifadhiwa kwanza katika kifuko cha akiba, karibu na kibofu, zikisubiri msisimko wa kijinsia ili zitoke kwa njia ya uume na kuanza mashindano ya kutafuta kijiyai, zikisaidiwa na majimaji ambayo yanaitwa shahawa na kutengenezwa ndani ya kifuko. Shahawa inafuata mshipa wa mkojo bila ya kuchanganyikana nao.

Shahawa inaweza ikatoka hata nje ya tumbo la uzazi la mke, lililo shabaha yake, kwa kuwa inalenga uzazi hasa. Inaweza ikatokea k.mf. kutokana na ndoto za usiku, bila ya mtu kukusudia; huyo anaweza akazinduka mara au kutambua asubuhi tu kilichotokea. Kwa vyovyote asihangaike kwa kuwa hilo ni jambo la kawaida lililopangwa na Mungu ili kumsaidia mwanamume asiye na mwenzi. Maana mbegu zake kadiri zinavyoongezeka katika kifuko cha akiba zinataka kutoka, hivyo zinamuelekeza kwenye matendo ya kijinsia. Basi, kwa ndoto hizo mbegu zinapungua bila ya dhambi, na vishawishi vinakosa ukali wake. Ni suala la kusubiri tu na kuwa na hakika kwamba havitadumu muda mrefu kwa nguvu ileile.

Mvulana anapotokwa na shahawa kwa mara ya kwanza ni dalili ya kuwa si mtoto tena, bali ana uwezo wa kuzaa: kwa hiyo awajibike kama mtu mzima kuhusu uwezo mpya aliojaliwa. Hasa azingatie kuwa uwezo wake huo bado ni mbichi: ingawa unaweza kusababisha mimba, mimba hiyo itaendelea kwa shida au kufa kabisa.

Ubichi ni mkubwa zaidi upande wa nafsi, kwa kuwa mvulana hajawa tayari kubeba mzigo wa familia mpya. Ndiyo sababu asichezee uwezo huo, bali ajiandae kuwa baba safi siku za mbele: ajipatie elimu au ufundi fulani, akomae kiutu na kutunza afya yake ya mwili na ya nafsi.

Kumbe akijiingiza mapema katika masuala ya ngono, anahatarisha heshima yake pamoja na afya, kwa kuambukizwa maradhi yanayoweza yakasababisha utasa au kwa kuzaa kwa shida kabla ya wakati wa kufaa.

Matatizo

Ugonjwa wa kufanya anasa isiyofaa mara nyingi hujidhihirisha ndani ya muda mfupi na uume unapungua kadiri miaka inavyosonga mbele: pengine inasababishwa na punyeto, lakini wengine huzaliwa na kupatikana kuwa hivyo.

Upungufu wa nguvu za kiume, yaani kutokuwa na nguvu ya kutimiza wajibu wa wanandoa, ni jambo ambalo mtu anataka lakini ngono inakataa kuwajibika (si kudanganywa au hata kudanganywa kwa muda na kuanguka). Ni shida sana kwa mwanamume kwa sababu husababisha kujiona mbovu, na kupata dharau kutoka kwa mtu anayefanya kazi.

Kupoteza uume ambapo unapata shida ukiona dume limeanguka na halijamwaga.

Kumwaga shahawa kabla ya wakati wa kufanya ngono nzuri na unataka kufanya ngono, lakini shahawa inatoka katika muda mfupi mno.

Tanbihi

  1. "Do Penis Pumps Really Work? (Aug 2018) | 5 Best Penis Enlargement Pump". Penetric (kwa American English). 2016-07-11. Iliwekwa mnamo 2018-09-03.
  2. Alessandro, Littara. "Penoplasty, Glans Augmentation Using Fillers (Non- Surgical Augmentation of the Glans)". www.laserpenoplasty.com. Iliwekwa mnamo 2018-09-03.
  3. "Glans Enhancement – Penis Head Augmentation | Small Penis Enlargement 2018". www.smallpenisenlargement.net (kwa American English). 2018-09-01. Iliwekwa mnamo 2018-09-03.
  4. Tim Jewell (2018-04-02). Debra Rose Wilson (mhr.). "Is There Really an Oil or Herb for Penis Enlargement?". Health Line (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2018-09-03.
  5. Mayo Clinic. "Erectile dysfunction - Symptoms and causes". Mayo Clinic (kwa American English). Mayo Foundation for Medical Education and Research (MFMER). Iliwekwa mnamo 2018-09-26.
  6. Fletcher, Jenna (2017-03-10), "Natural remedies for treating erectile dysfunction", Medical News Today (kwa Kiingereza), Healthline Media UK Ltd, iliwekwa mnamo 2018-09-26
  7. "Erectile Dysfunction: Treatment & Care", WebMD (kwa American English), iliwekwa mnamo 2018-09-26
  8. Anon. "Generic Tadalafil – Effective Solution for Several Male Health Problems". Apcalis SX (kwa en - US). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-09-12. Iliwekwa mnamo 2018-09-26.{{cite web}}: CS1 maint: unrecognized language (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mboo kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.