Tanuri la nyuklia
Tanuri la nyuklia ni mtambo ambamo mchakato mfululizo wa nyuklia unatokea. Mwatuko wa nyuklia huzalisha joto ambalo hutumiwa kutengeneza umeme.
Kuna aina mbalimbali za matanuri lakini kwa kawaida fueli ni ama urani-235 au plutoni-239.
Kiini cha tanuri la nyuklia
haririKiini ni sehemu ya tanuri la nyuklia yenye fueli yote: mwatuko wa nyuklia unatokea hapa. Kiini ni pia mahali pa kutokea kwa joto. Kiini hutengenezwa ndani ya chumba cha pekee ambacho kina kwanza ukuta wa feleji (mara nyingi tufe) unaozungukwa na ukuta mnene wa saruji iliyoimarishwa.
Fueli imo kwa umbo la nondo za urani au plutoni. Nondo za fueli hufanywa kwa pipa la feleji linalojazwa vidonge vya urani. Hapo nyutroni zinatoka katika atomi za urani au plutoni zikigonga atomi nyingine na kuzipasua. Kila upasuaji wa atomi unaachisha nishati nyuklia inayotokea hasa kwa njia ya joto.
Kiasi cha nyutroni kinachopatikana kwa kazi hii hutawaliwa kwa kuingiza au kuondoa nondo dhibiti. Hizi nondo dhibiti hujaa vidonge vya bori au kadmi na kuzuia mwendo wa nyutroni.
Kadiri nondo dhibiti zinaingizwa kwa wingi zaidi kati ya nondo za fueli, uenezaji wa nyutroni kutoka urani au plutoni unapungua ni vivyo hivyo kadiri nondo dhibiti zinavyotolewa mwendo wa nyutroni unaongezeka, na hivyo kuongeza kiasi cha nyutroni zinazogonga na kupasua atomi nyingine - au kupungukiwa. Kuingiza na kuondoa nondo dhibiti ni njia ya kusimamia tanuri na joto lake.
Uzalishaji umeme
haririJoto kutokana na mwatuko wa nyuklia linapasha moto kwa maji yanayopitishwa kwenye tanuri na kuwa mvuke. Mwendo wa mvuke huo unasukuma rafadha inayozalisha umeme.
Matanuri ya nyuklia kadhaa hazina kazi ya kuzalisha umeme, hasa ni matanuri ya utafiti wa kisayansi au ya kutengeneza isotopi nururifu kwa matumizi ya kimatibabu, au kwa kusudi la kuwafundisha wanafunzi kwenye vyuo vikuu.
Nchi zenye nguvu ya nyuklia
hariri1. Marekani
2. U.K.
3. Ufaransa
4. Russia
5. Libya
7. Namibia
8. India
9. Pakistan
10. Korea
11. China
12. Iran
13. Kanada
14. Niger
15. Israel
Historia
haririTanuri la nyuklia la kwanza liliundwa mwaka 1942 huko Chicago na wanasayansi walioongozwa na Mwitalia Enrico Fermi.[1] Hii ilikuwa sehemu ya mradi wa Manhattan Project iliyohitaji fueli nururifu kwa kutengeneza bomu nyuklia ya kwanza.
Tanuri la kwanza la kuzalisha umeme lilijengwa Idaho, Marekani mwaka 1951. Liliweza kung'arisha balbu 1 tu.[2].
Mnamo mwaka 2011 kulikuwa na matanuri nyuklia 437 zilizozalisha nishati nyuklia iliyokuwa takriban asilimia 5 za umeme duniani.
Matanuri ya nyuklia ni mitambo ghali sana kwa sababu unururifu wa urani na plutoni ni kali, zinahitaji kufikia kiwango cha juu cha usalama.[1] Tatizo lingine ni kiasi kikubwa cha takataka ya nyuklia inayohitaji kutunzwa salama kwa miaka mia elfu kadhaa. [1]
Faida ya tanuri la nyuklia ni kwamba halichafui hewa kama kituo cha nguvu ya makaa au mafuta.
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 "Nuclear Physics (2005)". Science in the Contemporary World: An Encyclopedia. 2011 [last update]. Iliwekwa mnamo May 29, 2011.
{{cite web}}
: Check date values in:|year=
(help) - ↑ http://www.inl.gov/factsheets/ebr-1.pdf Experimental Breeder Reactor 1
Viungo vya nje
hariri- Images for nuclear reactors
- Nuclear Power Reactors Ilihifadhiwa 12 Februari 2013 kwenye Wayback Machine.
- Recent videos for nuclear reactors