Kitabu cha Methali

(Elekezwa kutoka Mith)

Kitabu cha Mithali kimo katika Tanakh (Biblia ya Kiebrania), hivyo pia katika Agano la Kale la Biblia ya Kikristo ambamo ni cha kwanza kati ya vitabu vya hekima.

Kitabu cha Methali kwa Kiebrania.

Historia yake

hariri

Kweli kitabu hicho kinaonekana cha zamani kuliko vile vya hekima vinavyofuata; labda kilikamilika katika karne ya 4 KK, kisha kukusanya tafakuri za vizazi kadhaa juu ya maisha kwa mtazamo wa kibinadamu na wa imani.

Lugha yake

hariri

Kitabu kiliandikwa kwa Kiebrania na kutafsiriwa kwa mara ya kwanza katika lugha ya Kigiriki huko Misri (tafsiri maarufu kama Septuaginta).

Yaliyomo

hariri

Yaliyomo ni maadili ambayo yamuongoze mtu maishani ili awe na heri.

Ufafanuzi wake

hariri

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.


Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo * Kutoka * Walawi * Hesabu * Kumbukumbu * Yoshua * Waamuzi * Ruthu * Samueli I * Samueli II * Wafalme I * Wafalme II * Mambo ya Nyakati I * Mambo ya Nyakati II * Ezra * Nehemia * TobitiDK * YudithiDK * Esta * Wamakabayo IDK * Wamakabayo IIDK * Yobu * Zaburi * Methali * Mhubiri * Hekima DK * SiraDK * Wimbo Bora * Isaya * Yeremia * Maombolezo * BarukuDK * Ezekieli * Danieli * Hosea * Yoeli * Amosi * Obadia * Yona * Mika * Nahumu * Habakuki * Sefania * Hagai * Zekaria * Malaki

Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.

  Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitabu cha Methali kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.