Mtumiaji:Zenman/Mradi wa Afrika

Makala iliyochaguliwa

hariri

Makala iliyochaguliwa kwa Novemba 2012

hariri
 

Hifadhi ya Serengeti ni eneo kubwa la savana na misitu katika Tanzania ya kaskazini hasa katika mikoa ya Mara na Arusha ikipakana na Kenya. Eneo lake ni 14,763 km² na kijiografia inaendelea ndani ya Kenya inapoitwa Hifadhi ya Masai Mara. Kuna idadi kuba ya wanyama wa pori. Serengeti pamoja na Masai Mara inajulikana hasa kwa uhamisho wa kila mwaka wa zaidi ya milioni moja ya nyumbu wanaovuka mto Mara. Kuna pia aini nyingi nyingine za wanyama kati yao "watano wakubwa" wanaovuta watalii hasa yaani tembo, simba, chui, fisi, kifaru na nyati. Eneo la hifadhi ya Ngorongoro liliwahi kuwa sehemu ya Serengeti hadi kutengwa kama hifadhi ya pekee. Bonde la Olduvai ambako mabaki ya wanadamu wa kale kabisa yalipatikana liko ndani ya Serengeti. Mazingira ya Serengeti ni kanda ya kijiografia iko katika kaskazini-magharibi ya Tanzania na inaenea kwa kusini-magharibi mwa Kenya kati ya latitude 1 na 3 Kusini na longitude 34 na 36 Mashariki. Ina enea kiwango cha mraba kilometa 30,000 2.


Je, wajua...?

hariri


Wasifu Uliochaguliwa

hariri

Wasifu Uliochaguliwa kwa Novemba 2012

hariri
 
 
Nelson Mandela

Nelson Rolihlahla Mandela alizaliwa tarehe 18 Julai, mwaka 1918. Ni rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia nchini Afrika Kusini. Alikuwa mwanasheria na mwanachama wa ANC aliyepinga siasa ya Apartheid katika Afrika Kusini. Mandela alitumikia kifungo cha maisha kwa miaka 27 kutokana na harakati zake za kuupinga ubaguzi wa rangi. Alifungwa katika kisiwa cha Robben. Baada ya kuachiliwa huru mwaka 1990 alianzisha sera ya maridhiano. Mwaka wa 1993, pamoja na Frederik Willem de Klerk alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani.

kuchaguliwa picha kwa 2012

hariri

kuchaguliwa picha kwa Novemba 2012

hariri
 


Ngoma kutoka Rwanda.
(kupata bango)