Panzi-bahari

(Elekezwa kutoka Ndegemaji)
Panzi-bahari
Panzi-bahari wa Mediteranea (Cheilopogon heterurus)
Panzi-bahari wa Mediteranea (Cheilopogon heterurus)
Panzi-bahari akianza kuruka
Panzi-bahari akianza kuruka
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Actinopterygii (Samaki walio na mapezi yenye tindi)
Oda: Beloniformes (Samaki kama ngarara)
Familia: Exocoetidae (Samaki walio na mnasaba na panzi-bahari)
Risso, 1827
Ngazi za chini

Jenasi 7 na spishi 64, 27 katika Afrika:

Panzi-bahari, panzi-maji, panzimai au ndegemaji ni samaki wa baharini wa familia Exocoetidae katika oda Beloniformes ambao wanaweza kuruka juu ya maji na kwenda mbali kiasi, mpaka mamia ya mita. “Mabawa” yao ni mapeziubavu kwa kweli. Katika spishi za jenasi Cheilopogon na Cypselurus hata mapezitumbo yanatumika kama mabawa na kwa hivyo huitwa “panzi-bahari mabawa-manne”. Uwezo huu usio wa kawaida katika samaki ni utaratibu wa asili wa utetezi kuepuka mbuai. Pengine pezimgongo ni refu na huitwa tanga.

Samaki wa familia Triglidae huitwa panzi-bahari pia.

Makazi

hariri

Panzi-bahari huishi katika bahari zote, hasa katika maji vuguvugu ya tropiki na ya nusutropiki. Hupatikana katika kanda ya epipelago, tabaka la juu la bahari hadi kina cha takriban m 200. Mara nyingi hujulikana kama "kanda ya nuru ya jua" kwa sababu ni mahali ambapo nuru nyingi ipo. Karibu uzalishaji wote wa msingi, au usanidimwanga, hutokea katika kanda hii. Kwa hivyo, wengi sana wa mimea na wanyama huishi eneo hili na wanaweza kutofautiana kutoka kwa planktoni hadi papa. Ingawa kanda ya epipelago ni eneo la kipekee kwa aina mbalimbali za viumbehai, pia ina vikwazo vyake. Kutokana na unamnanamna mkubwa wa viumbehai, kuna idadi kubwa za mahusiano ya mawindo na mbuai.

Viumbehai vidogo kama vile panzi-bahari ni malengo kwa viumbe vikubwa zaidi. Huwa na wakati mgumu hasa wa kutorokea mbuai na kuishi mpaka waweze kuzaa, inayosababisha kuwa na ukakamavu wa chini. Pamoja na shida za uhusiano, visababishi vya mazingira yasiyo hai pia vinachangia. Mikondo ya bahari yenye nguvu huwafanyia samaki wadogo vigumu sana kuishi katika makazi haya. Utafiti unadokeza kwamba visababishi vigumu vya mazingira katika makazi ya panzi-bahari yamesababisha mageuko ya mapezi yaliyobadilika. Kwa matokeo ya haya, panzi-bahari wamepata uteuzi wa asili ambapo spishi hupata sifa za kipekee ili kukabiliana na mazingira yao. Wakiruka angani, panzi-bahari huwaepuka mbuai wao. Ongezeko hili la kasi na uwezo wa kugeuka haraka ni faida ya kuokoka kwa panzi-bahari ikilinganishwa na spishi nyingine katika mazingira yao. Pia imependekezwa kwamba kuruka angani siyo tu maarifa ya kuepuka mbuai, kwa sababu panzi-bahari wameonwa wakiruka kutoka kwa maji bila kuwepo kwa mbuai. Nadharia nyingine pia zimependekezwa zinazojumuisha kuokoa nishati na kuingia kwenye mazingira tajiri kwa chakula .

Panzi-bahari hula planktoni hasa. Mbuai wao wanajumuisha pomboo, jodari, sulisuli, ngisi na ndege.

Maelezo

hariri

Spishi nyingi za panzi-bahari zina umbo la dulabu na mapeziubavu yaliyopanuka na kurefuka ili kutumika kama mabawa. Zile za jenasi Cheilopogon na Cypselurus zina mwili bapa na mapezitumbo pia yamepanuka na kurefuka ili kuongeza muda wanapoendelea hewani.

Panzi-bahari wamepata mabadiliko ya kimofolojia katika historia yao na lile la kwanza ni matao ya kineva yaliyopanuka sana ambayo hutumika kama mahali pa kuingiza misuli, tishu zinazounganisha na mishipa katika kiunzi cha samaki. Matao haya mapana ni thabiti na imara zaidi, yakiumba hivyo kiungo imara kati ya uti wa mgongo na fuvu. Hatimaye hii inaruhusu uti wa mgongo mgumu na imara ambayo una manufaa katika kuruka. Kuwa na mwili mgumu wakati wa kuruka na kunyiririka hupatia panzi-bahari faida ya kupitia hewa, ikiongeza kasi yake na kuboresha lengo lake. Sifa hizi zinapatia panzi-bahari nguvu kubwa na kuwawezesha kuruka nje ya maji na kuumbia umbali wa ajabu bila kudhoofisha hewani. Mwishoni wa mruko, hukunja mapeziubavu yao ili kurudi baharini, au kuweka mkia wao ndani ya maji ili kusukuma dhidi yai maji na kujiinua kwa mruko mwingine, labda wakibadilisha mwelekeo. Umbo la mchirizo wa "bawa" unafanana na umbo la kubebwa na hewa la bawa la ndege. Samaki huweza kuongeza muda wake katika hewa wakiruka moja kwa moja ndani au kwa pembe kwa mwelekeo wa hewa inayoenda juu ambayo inayosababishwa na mchanganyiko wa mikondo ya hewa na bahari.

Uvuvi na chakula

hariri

Panzi-bahari huvuliwa kibiashara kwa wavu-matamvua huko Japani, Vietnam na Uchina, na huko Indonesia na Uhindi kwa wavu-mkononi. Mara nyingi katika upishi wa Kijapani, samaki hawa huhifadhiwa kwa kuwakausha ili kutumika kama mchuzi wa samaki kwa kutengeneza supu yadash. Ng'ofu ya Cheilopogon agoo, au panzi-bahari wa Japani, hutumika kutengeneza aina fulani za sushi na hujulikana kama tobiko. Pia ni chakula kikuu katika milo ya Watao wa Orchid Island, Taiwan. Panzi-bahari ni sehemu ya chakula cha taifa cha Barbados: cou-cou na panzi-bahari. Ladha ni karibu na ile ya dagaa.

Spishi za Afrika

hariri

Mengineyo: nyota

hariri

Kuna kundinyota kwenye angakusi lililopokea jina la Volans ( Panzimaji) kwa kumbukumbu ya samaki hao. Panzimaji inapatikana kati ya makundinyota yaliyobuniwa tangu mabaharia Wazungu kuzunguka dunia yote yaani karne ya 16 na kuona mara ya kwanza nyota za kusini. Kundinyota hili lilielezwa mara ya kwanza na baharia Mholanzi Pieter Dirkszoon Keyser.

Marejeo

hariri
  • Rashid Anam & Edoardo Mostarda (2012) Field identification guide for the living marine resources of Kenya. FAO, Rome.
  • Gabriella Bianchi (1985) Field guide to the commercial marine brackish-water species of Tanzania. FAO, Rome.

Viungo vya nje

hariri