Ulama
Ulama (pia: Ulema, kutoka Kiarabu علماء ʿulamāʾ) ni namna ya kutaja wataalamu wa dini katika Uislamu.
Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya |
Imani na ibada zake |
Umoja wa Mungu |
Waislamu muhimu |
Abu Bakr • Ali |
Maandiko na Sheria |
Qur'an • Sunnah • Hadithi |
Historia ya Uislamu |
Historia |
Tamaduni za Kiislamu |
Shule • Madrasa |
Tazama pia |
Mamlaka na uwezo wao ni tofauti katika jamii za Kiislamu kufuatana na mapokeo tofauti. Katika madhehebu ya Shia wana athira kubwa zaidi.
Kati ya Waislamu ulema huulizwa kuhusu uelewano wa sharia na vipengele vingine vya imani.
Neno "ulama" latokana katika lugha ya Kiarabu na hapa ni wingi wa aalim (ar. عالِم) inayomaanisha "mtu mwenye elimu, mtaalamu". Neno hili linaweza kutaja wataalamu wa kila fani lakini inamaanisha hasa wataalamu wa dini[1].
Matawi ya elimu
haririKimapokeo ulema hujifunza Quran, tafsir (namna ya kuelewa Qurani), Sunnah na ahadith, shariah (kanuni za imani), fiqh (namna ya kutumia sharia) na kalam (theolojia au mafundisho kuhusu imani).
Marejeo
haririMakala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |