Kurani
Kurani (kwa Kiarabu: القرآن, Qur'an) ni kitabu kitukufu cha Uislamu ambacho kinaaminiwa na Waislamu kuwa ni "Neno la Allah (Mwenyezi Mungu)". Kitabu hicho kwao ni tofauti kabisa na maandiko ya dini nyingine kwa maana hicho kinaaminika kwamba kimeandikwa moja kwa moja na Mwenyezi Mungu, kupitia mtume wake wa mwisho, Muhammad.
Sehemu ya mfululizo wa makala juu ya |
Imani na ibada zake |
Umoja wa Mungu |
Waislamu muhimu |
Abu Bakr • Ali |
Maandiko na Sheria |
Qur'an • Sunnah • Hadithi |
Historia ya Uislamu |
Historia |
Tamaduni za Kiislamu |
Shule • Madrasa |
Tazama pia |
Kadiri ya Qurani (42:8), Mungu alimuambia Muhammad: "Na namna hivi tumekufunulia Qurani kwa Kiarabu ili uwaonye watu wa Makka na walio pembeni mwake"
Kurani imeandikwa na kusomwa kwa lugha ya Kiarabu pekee kwa zaidi ya miaka 1,445.
Lakini, kwa vile leo Waislamu walio wengi ulimwenguni hawajui Kiarabu, maana halisi ya Qur'an hutolewa kwa lugha nyingine, hivyo kupelekea wasomaji kuelewa vyema yale maneno ya Kiarabu kwenye Qur'an yana maana gani. Vitabu hivyo ni kama kamusi kwa ajili ya Qur'an - hawavisomi hivi kama moja ya sehemu ya Quran na Waislamu, ili kuwa badala ya Quran ya Kiarabu.
Waislamu wengi wanaamini kwamba tafsiri ile si ya Qur'an tukufu wala si ya kweli; ni nakala ya Kiarabu tu iliyotolewa kwenye Qur'an ya kweli.[1]
Waarabu wa kabla ya Uislamu waliunda hadithi na hadithi juu ya miti, visima na milima, na waliunda ibada zinazohusiana na miamba na milima huko Safa, Marwa, Abu Kubeys, Arafat, Mina na Muzdalifah. Ingawa Qur'ani ilifuta ibada nyingine, haikupingana na maandiko ya Kiarabu yenye mizizi, badala yake, iliendeleza sana ibada hizo.[2] Wakati mwingine inakuwa vigumu kuelewa Qur'ani bila kujua mazoea ya zamani; kihistoria, wanadamu hawakutumia kipimo cha wakati kikubwa kuliko mwezi. Hivyo, mtu ambaye alisema, "Nina umri wa miaka 200." alikuwa akihesabu miezi, sio miaka. Kwa kweli alikuwa na umri wa miaka 16.[3] "Tulimpeleka Nuhu kwa watu wake na akakaa kati yao kwa miaka elfu, isipokuwa miaka hamsini." (Ankebut: 14)
Kwa kuongezea vyanzo vilivyoandikwa, masomo mengi na mashujaa, ambayo mengine ni tu katika utamaduni wa hadithi za Kiarabu, yamefunikwa kwa kifupi katika lugha ya Kurani, na marejeo madogo yanafanywa. Hadithi za Yusuf na Züleyha, İsa, Musa, İskender / Zülkarneyn ni hadithi ndefu zaidi. Hadithi za uumbaji na mafuriko, ibada ya Ibrahimu na Dhabihu, hadithi za manabii wa Kiebrania, imani ya Kiyahudi na historia, kama vile kutoka kwa Waisraeli kutoka Misri, zinachukua nafasi kubwa katika Kurani.
Historia
haririWaislamu wanaamini kwamba Qur'an mtume Muhammad alipewa na malaika Jibrīl kwenye pango la mlima Hira, kwa kipindi cha zaidi ya miaka ishirini na tatu hadi mauti yake ilipomfikia.
Qur'an haikuwa kitabu cha maandiko wakati wa uhai wa mtume Muhammad; iliwekwa kwa mawasiliano ya kimdomo tu. Bimaana, watu walihifadhi kichwani.
Mtume labda hakuwa anajua kusoma wala kuandika, lakini kwa mujibu wa Waislamu, swahaba wake Abu Bekr alikuwa akiandika maandiko yale juu ya kitu fulani wakati huo mtume Muhammad yu hai. Pale Abu Bekr alipokuja kuwa khalifa, ameileta Qur'an na kuwa kitabu kitakatifu.
Uthman, ambaye ni khalifa wa tatu, ameondoa vipengele ambavyo vilikuwa havihusiani na Qur'an tukufu.
Elementi, Sura, Mistari, Aya
haririKuna sehemu 30 katika Qur'an, ambayo inafanya kuwa na sura 114. Kila sura ina namba tofauti ya mistari.
Kwa mujibu wa mafunzo ya Kiislam, sura 86 kati ya hizi zimeshuka mjini Makka, sura 24 kati ya hizi zimeshuka mjini Madina.
Miongoni mwa sura zilizoshushwa mjini Medina ni pamoja na Al-Baqara, Al Imran, Al-Anfal, Al-Ahzab, Al-Ma'ida, An-Nisa, Al-Mumtahina, Az-Zalzala, Al-Hadid, Muhammad , Ar-Ra'd, Ar-Rahman, At-Talaq, Al-Bayyina, Al-Hashr, An-Nasr, An-Nur, Al-Hajj, Al-Munafiqun, Al-Mujadila, Al-Hujraat, At-Tahrim, At-Taghabun, Al-Jumua, As-Saff, Al-Fath, At-Tawba, Al-Insan.
Mahusiano baina ya Qur'an na Biblia
haririKatika Qu'ran , inasomwa kwamba Wayahudi na Wakristo pia huamini Mungu wa kweli. Dini hizo pamoja na Uislamu huitwa Dini za Abrahamu kwa sababu ya mahusiano hayo.
Kuna baadhi ya kurasa za Qu'ran zinazoelezea habari za mambo ya watu wa katika Biblia. Kwa mfano watu wa katika Biblia waliotajwa kwenye Qu'ran ni pamoja na Adamu, Nuhu, Abrahamu, Lutu, Ismaili, Yakobo, Yosefu, Haruni, Musa, mfalme Daudi, Solomoni, Elisha, Yona, Ayubu, Zekaria, Yohane Mbatizaji, Bikira Maria na Yesu.
Hata hivyo, kuna tofauti za muhimu kabisa baina ya Uislamu na toleo la Biblia katika kuelezea habari za aina moja. Kwa mfano, Qu'ran inaelezea kwamba Yesu Kristo si Mwana wa Mungu, kama jinsi Wakristo wanavyoamini; kwa Waislamu, alikuwa nabii tu, anayeheshimiwa kwa jina la Isa bin Mariamu.
Uislamu unafundisha kwamba haya yanatokea kwa sababu maandiko ya awali ya Biblia yamepotea na hivyo kuna baadhi ya watu wameyabadilisha. Lakini nje ya Qu'ran hakuna uthibitisho wa fundisho hilo.
Kurani na ulimwengu wa leo
haririSheria zinazotegemea matamshi na ufafanuzi wa Kurani ni shida leo kuzilinganisha na haki za binadamu, usawa wa kijinsia na dini ya binafsi na uhuru wa kusema.[11]
Tazama pia
haririTanbihi
hariri- ↑ Qur'an, Encyclopedia Britannica, retrieved on 8 Januari 2009
- ↑ https://www.researchgate.net/publication/317604040_Cahiliye_Arap_Hac_Rituellerinin_Kur'an'daki_Menasikle_Diyalektik_Iliskisi/link/5e20c19d458515ba208de0a1/download
- ↑ https://evrimagaci.org/zamani-olcmek-gun-hafta-ay-yil-kavramlari-nasil-olustu-7715
- ↑ Dan Gibson: Qur'ānic geography: a survey and evaluation of the geographical references in the qurãn with suggested solutions for various problems and issues. Independent Scholars Press, Surrey (BC) 2011, ISBN 978-0-9733642-8-6
- ↑ https://www.mdpi.com/2077-1444/11/3/102/htm
- ↑ https://dergipark.org.tr/tr/download/article-file/592002
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-07-01. Iliwekwa mnamo 2021-07-09.
- ↑ https://dergipark.org.tr/tr/download/article-file/557354
- ↑ https://www.icr.org/article/noah-flood-gilgamesh
- ↑ Leirvik 2010, pp. 33–34.
- ↑ https://www.iusinitinere.it/clash-between-sharia-law-and-human-rights-in-light-of-pace-resolution-2253-23827
Marejeo
hariri- Al-Quran (Qurani) online Ilihifadhiwa 29 Januari 2009 kwenye Wayback Machine. kwa Kiarabu na tafsiri zaidi ya 100 katika lugha 20 pamoja na Kiswahili
- Quran.com
- Swahili Quran Tasfir by Sheikh Abdullah Saleh Al-Farsy,
- Tarjuma ya Quran Tukufu kwa kiswahili ya Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani
Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kurani kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |