Wikipedia:Makala kwa ufutaji/Nyaraka 7
Hii ni nyaraka ya makala Wikipedia:Makala kwa ufutaji ya mwaka 2022 hadi Machi 2023. Ina makala pekee zilizofutwa au kurekebishwa ili zibaki; zisizosahihishwa zimebaki kwenye ukurasa kuu.
Kwa nyaraka za zamani zaidi angalia hapa.
Ifutwe au kuboreshwa. Fomati haijafuatwa, haina vyanzo. Aneth 12:59 11 Novemba 2020 UTC
David cross IMEFUTWA
haririHaina vyanzo vyovyote. Iboreshwe. Aneth 13:02 11 Novemba 2020 UTC
Maandamano ya 2020 katika Marekani IMEFUTWA
haririSioni maana ya makala. Maandamano ni jambo la kawaida katika nchi ya kidemokrasia. Makala haina chanzo chochote kuthibitisha chaguo la maanadamano yaliyoteua. Kipala (majadiliano) 21:45, 13 Desemba 2020 (UTC)
Assassin's Creed Odyssey IMEFUTWA
haririSehemu ya pili haieleweki. Tafsiri ya kompyuta? Hakuna vyanzo vyovyote. Isiporekibishwa haraka, iende. Kipala (majadiliano) 21:27, 8 Machi 2021 (UTC)
- Ifutwe, Haifa Bora na mpangilio abaya Asterlegorch367 (majadiliano) 07:24, 13 Januari 2022 (UTC)
Mtumiaji:Stanley Steven IMEFUTWA
haririNi ukurasa wa mtumiaji alipoweka matangazo ya kibiashara. Nimemwonya tayari, naipeleka hapa nisisahau onyo. Kipala (majadiliano) 16:48, 13 Machi 2021 (UTC)
Makala inagusa mada muhimu katika historia lakini lugha ni mbaya mno. Nahisi ni tafsiri ya kompyuta ambayo haikuangaliwa tena. Haiwezi kubaki. Ama iandikwe upya kabisa , na kwa lemma tofaut (na sahihi), au ifutwe. Tena sijui amechukua wapi, kichwa cha Kiingereza kilikuwa kitu kama "Brussels Conference Act"; "conference act" ni maazimio ya mkutano, si "sheria". Kipala (majadiliano) 06:14, 10 Julai 2021 (UTC)
- Hie ifutwe tu, labda kma mwandishi angetaka kuboresha. Lugha na mpangilio mbaya unaweza kupotosha Asterlegorch367 (majadiliano) 07:24, 13 Januari 2022 (UTC)
Ulaya na Afrika IMEFUTWA
haririTafsiri ya kompyuta mbovu sana. Labda ieleweke kwanza. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:14, 12 Julai 2021 (UTC)
- Ifutwe, kwanza haieleweki hata inahusu nini Asterlegorch367 (majadiliano) 07:27, 13 Januari 2022 (UTC)
VVU / UKIMWI nchini Ethiopia IMEFUTWA
haririTafsiri mbaya ya kompyuta. Isahihishwe au kufutwa. Kipala (majadiliano) 10:48, 11 Agosti 2021 (UTC)
UKIMWI nchini Uganda IMEFUTWA
haririMakala jinsi ilivyo ni tokeo la google translate. Sentensi kadhaa za Kiswahili ni kinyume cha maana ya kiasili ya Kiingereza. Pamoja na hayo makala ya enwiki haileti picha halisi ya hali ya Ukimwi nchini Uganda. Ama iandikwe upya au kufutwa. Kipala (majadiliano) 07:59, 25 Agosti 2021 (UTC)
Marimar, Mi corazón es tuyo, María la del Barrio ZIMEFUTWA
haririMakala hizo ziliundwa na mtumiaji mwenye matatizo ya lugha, sehemu kubwa ya matini haieleweki, hakuna vyanzo. Sioni maana kutumia muda kusahihisha makala isiyo na maana kwa wasomaji wetu. Kipala (majadiliano) 08:33, 23 Septemba 2021 (UTC)
- Hizi zifutwe moja kwa moja. Kuboresha ni sawa na kuanza upya Asterlegorch367 (majadiliano) 07:30, 13 Januari 2022 (UTC)
Susan Headley IMEFUTWA
haririIfutwe. Chanzo ni hasa enwiki kisichokubalika, sehemu iliyotafsiriwa haina habari inayoonyehsa umuhimu wowote, inaonyesha tafsiri ya kompyuta. Kipala (majadiliano) 10:14, 5 Oktoba 2021 (UTC)
- Iwapo mwandishi aliyeianzisha hatafanya mabadiliko, ifutwe Asterlegorch367 (majadiliano) 07:32, 13 Januari 2022 (UTC)
Albert Gonzalez IMEFUTWA
haririIfutwe. Chanzo ni hasa enwiki kisichokubalika, maudhui kuna tafsiri ya kompyuta mbaya sana. Kama hakuna anayetaka kuiandika upya, iende tu. Kipala (majadiliano) 10:18, 5 Oktoba 2021 (UTC)
- Nakubaliana na were Kipala, ifutwe Asterlegorch367 (majadiliano) 07:32, 13 Januari 2022 (UTC)
Mike Gogulski IMEFUTWA
haririIfutwe. Chanzo ni hasa enwiki kisichokubalika, maudhui kuna tafsiri ya kompyuta mbaya sana. Sehemu iliyotafsiriwa haionyesha umaarufu wowote. Kipala (majadiliano) 10:20, 5 Oktoba 2021 (UTC)
- Nakubaliana na Kipala, makala ifutwe Asterlegorch367 (majadiliano) 07:22, 13 Januari 2022 (UTC)
William Genovese IMEFUTWA
haririIfutwe. Chanzo ni hasa enwiki kisichokubalika, maudhui kuna tafsiri ya kompyuta mbaya sana. Umaarufu haueleweki. Kipala (majadiliano) 10:24, 5 Oktoba 2021 (UTC)
- Napendekeza ifutwe Asterlegorch367 (majadiliano) 07:22, 13 Januari 2022 (UTC)
Eddie Davidson, Jay Cohen, Max Butler, Vitaly Borker ZIMEFUTWA
haririMakala zote nne zinatumia enwiki kama chanzo ambacho hakikubaliki, maudhui kuna tafsiri ya kompyuta mbaya sana. Sioni umaarufu kwa wote. Kipala (majadiliano) 10:32, 5 Oktoba 2021 (UTC)
Ryutaro Araga IMEFUTWA
haririMakala haifuati fomati wala haikupangwa katika jamii. Iboreshwe au kufutwa.Kipala (majadiliano) 08:40, 3 Desemba 2021 (UTC)
- Napendekeza ifutwe, labda kama mwandishi atataka kuboresha. Asterlegorch367 (majadiliano) 07:21, 13 Januari 2022 (UTC)
Joby Iblado IMEFUTWA
haririMakala haifuati fomati wala haikupangwa katika jamii. Mtu mwenyewe ni maarufu kweli? Iboreshwe au kufutwa. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:32, 5 Desemba 2021 (UTC)
- Napendiekeza ifutwe Asterlegorch367 (majadiliano) 07:20, 13 Januari 2022 (UTC)
Uongozi baada ya mtume IMEFUTWA
haririTafsiri ya kompyuta ya kutetea madhehebu fulani dhidi ya mengine. Irekebishwe au ifutwe. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:27, 16 Desemba 2021 (UTC)
- Hie ifutwe tu. Ni makala kubwa ila haini mpangilio na amefanya tafsiri ya moja kwa moja Asterlegorch367 (majadiliano) 07:20, 13 Januari 2022 (UTC)
Tanzania Tech IMEFUTWA
haririNina mashaka kuhusu mada. Kwanza lemma "Tanzania Tech" ni tofauti na link inayofunguliwa "Tech Platform". Halafu naona dalili kwamba makala ni jaribio la mhariri kujitangaza (linganisha mtumiaji:Tech Platform ). Sioni dalili ya umaarufu (link ya pekee inayodai tovuti ilijadiliwa imekufa, na inaleta IP ya mwenyewe). Halafu links zinaelekea tovuti mbili tofauti: https://www.tanzaniatech.one/ na https://techplatform6.blogspot.com/. Ile ya pili inajaa nafasi za kubofya "play" na "download" bila kuonyesha inahusu nini. Hii ni hatari. Kipala (majadiliano) 22:06, 11 Januari 2022 (UTC)
- Napendekeza makala hii ifutwe. Haina umaarufu wala vyanzo
Asterlegorch367 (majadiliano) 07:13, 13 Januari 2022 (UTC)
- Basi futa. Nimepeleka mimi, ukikubali wewe - futa!° Kipala (majadiliano) 10:33, 13 Januari 2022 (UTC)
- Nadhani hii ilibadilishwa kutoka makala halisi "Tanzania Tech" kuwa makala ya "Tech Platform" ambayo haitambuliki. Nadhani kuna haja ya kutoa nafasi kwa makala kuongezewa vyanzo ili kuendelea kuwepo kwani imekwepo tokea mwaka 2016. Amanijoseph87 (majadiliano) 17:36, 13 Januari 2022 (UTC)
- Ndugu unaongeza wasiwasi. Makala haikuwepo tangu 2016 jinsi unavyosema; wewe ulianzisha 08:01, 2 Juni 2019. Ila matini inasema tovuti ilianzishwa 2020. Halafu uliingiza sasa habari kuwa "Tanzania Tech has raised a total of $1B in funding over 1 round." Hii inamaanisha nini? Bilioni USD moja???? Haiwezekani. Nanusu fake nzito. Kipala (majadiliano) 06:59, 14 Januari 2022 (UTC)
Nina wasiwasi kuhusu makala hiyo napendekeza ifutwe. Maana sijaona orodha ya kata au vijiji penye majina yale yanayotajwa humo. Naona shule ya sekondari ya Chasasa, hakuna nyingine. Pamoja na Kiswahili kibaya na tahajia yenye makosa mengi , tufute. Kipala (majadiliano) 19:44, 3 Februari 2022 (UTC)
- Mji huo upo: [1]. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:49, 4 Februari 2022 (UTC)
Laverne cox IMEFUTWA
haririTafsiri mbovu, vyanzo visivyotakiwa. Ifutwe. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:59, 10 Februari 2022 (UTC)
Binafsi naona ifutwe tuu kwasababu huyu mwenzetu amekwisha kupewa maonyo tangu hapo awali na hajataka kutafuta msaada wa kujifunza kuandika na kuhalili makala, nimechungulia jinsi ulivokua unamkumbusha lakina bado hajatekeleza yale aliyo ambiwa. -- Olimasy (majadiliano)
Tafsiri mbaya, haieleweki, ifutwe au mtu awekeza muda wa kuboresha. Kipala (majadiliano) 07:13, 16 Februari 2022 (UTC)
Tafsiri mbaya, haieleweki, ifutwe au mtu awekeze wakati wa kuboresha. Kipala (majadiliano) 07:13, 16 Februari 2022 (UTC)
Majadiliano:Spider-Man (filamu) IMEFUTWA
haririNi dhahiri tafsiri ya kompyuta iliyosafishwa kiasi tu. Makosa yanaobaki ( "kijana mwenye akili timamu" , kuaha Kiingereza kisichotafsiriwa) yanahitaji kusafishwa tena, au makala kufutwa. Kipala (majadiliano) 07:13, 16 Februari 2022 (UTC)
Ukomavu wa kijusi IMEFUTWA
haririMakala haina maudhui, haina fomati wala vyanzo. Kipala (majadiliano) 11:29, 17 Februari 2022 (UTC)
Purificación Angue Ondo IMEFUTWA
haririHaieleweki, sioni sababu ya kuwa na makala. Kipala (majadiliano) 20:10, 17 Februari 2022 (UTC)
Kibengali (Bangla) IMEELEKEZWA UPYA
haririMakala haieleweki, naona kunahitaji maboresho zaidi, lakini pia mwanzo wa makala hiyo na makala ya Kiingereza bado kunaonekana kuna utofauti, Pia naona Kuna haja ya kuwa na Kigezo cha Makala zisizoeleweka, huenda kuna watumiaji wasio wazuri wa lugha ya Kiswahili wanaofanya tafsiriIdd ninga (majadiliano) 17:26, 21 Machi 2022 (UTC)
- Nimeelekeza ukurasa kwenda Kibengali. Siku hizi wengi wanaandika tena makala zilizopo tayari. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 07:38, 22 Machi 2022 (UTC)
Siasa za Kenya IMEFUTWA
haririMakala ni kopi kutoka BBC. Kipala (majadiliano) 08:01, 3 Aprili 2022 (UTC)
Mtandao wa matangazo IMEFUTWA
haririMakala haifuati fomati, haina vyanzo, kwa jumla haieleweki. Sijakuta kampuni yenye jina kama lemma. Kipala (majadiliano) 12:16, 3 Aprili 2022 (UTC)
Rekodi rasmi za dunia IMEFUTWA
haririMatini ni google translate. Anayependa aokoe, menginevyo ifutwe. Kipala (majadiliano) 18:43, 6 Aprili 2022 (UTC)
Kuuawa kwa Javier Ambler IMEFUTWA
haririSioni sababu ya kuwa na makala hii. Ni kifupi kiasi kwamba haieleweki historia ya tukio ilikuwaje. Kuna kasoro katika umbo la makala. Ama iboreshwe na kupanuliwa sa, au ifutwe. Kipala (majadiliano) 22:01, 18 Aprili 2022 (UTC)
Engelbert Pigal IMESAHIHISHWA
haririMatini ni google translate 1:1. Isahihishwe au kufutwa. Kipala (majadiliano) 07:56, 6 Mei 2022 (UTC)
Haki kwa mazingira yenye afya IMEFUTWA
hariri- . Makala haina chanzo kinachoweza kukubaliwa
- . Makala ni fupi mno haina kitu nje ya ufafanuzi mfupi ambao hatuhitaji kwa sababu
- . makala Haki ya kuwa na mazingira salama iko tayari.
Ilhali makala hii hapa haina habari zaidi, ifutwe tu. Kipala (majadiliano) 22:03, 16 Mei 2022 (UTC)
Mtumiaji:M Nex Nex I IMEFUTWA
haririSi kujitangaza? --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:50, 31 Mei 2022 (UTC)
- Tusikie wengine pia. Anajitangaza , lakini jinsi ilivyo sasa naona iko chini ya kiwango cha tangazo la kibiashara. Kipala (majadiliano) 20:10, 13 Juni 2022 (UTC)
Tafsiri ya google 1:1, enwiki kama chanzo Kipala (majadiliano) 16:30, 13 Juni 2022 (UTC)
Tafsiri ya google 1:1, enwiki kama chanzo Isahihishwe au kufutwa.Kipala (majadiliano) 16:36, 13 Juni 2022 (UTC)
Gari ya kulowekwa IMEFUTWA
haririTafsiri ya google 1:1 Isahihishwe au kufutwa. Kipala (majadiliano) 16:49, 13 Juni 2022 (UTC) Olimasy (majadiliano)
Makala imeundwa kwa kutumia google translate 1:1 pamoja na makosa. Isahihishwe au kufutwa. Kipala (majadiliano) 20:07, 13 Juni 2022 (UTC)
Namibian cuisine IMEFUTWA
haririHii ni google translate kutoka https://en.wikipedia.org/wiki/Namibian_cuisine, Isahihishwe kabisa au kufutwa. Kipala (majadiliano) 21:07, 13 Juni 2022 (UTC)
Koeksister IMEFUTWA
haririTafsiri ya google kutoka https://en.wikipedia.org/wiki/Koeksister. Isahihishwe kabisa au kufutwa. Kipala (majadiliano) 21:07, 13 Juni 2022 (UTC)
Tafsiri ya google kutoka https://en.wikipedia.org/wiki/Samp. Isahihishwe kabisa au kufutwa. Kipala (majadiliano) 21:07, 13 Juni 2022 (UTC)
Tafsiri ya google kutoka https://en.wikipedia.org/wiki/Kube_Cake. Isahihishe kabisa au kufutwa. Kipala (majadiliano) 21:07, 13 Juni 2022 (UTC)
.. Olimasy (majadiliano)
Tafsiri ya google kutoka https://en.wikipedia.org/wiki/Qustul iliyofupishwa na iliyosahihishwa kidogo, lakini muundo wa sentensi si Kiswahili. Isahihishe kabisa au kufutwa.Kipala (majadiliano) 21:07, 13 Juni 2022 (UTC)
Utalii nchini Rwanda IMEFUTWA
haririKama juu. Kipala (majadiliano) 21:07, 13 Juni 2022 (UTC)
CLUB PLAYERS, CLUB OFFICIALS, Bahari United Profile ZIMEFUTWA
haririMakala hazilingani hata kidogo na fomati na maudhui ya kamusi elezo. Zifutwe. Kipala (majadiliano) 10:14, 20 Juni 2022 (UTC)
Panishee Mdudu IMEREKEBISHWA; IBAKI
haririHuyo jamaa kwanza alijitungia ukurasa wake katika kamusi elezo, halafu ulipofutwa kwa sababu alitaka tu kujinadi alimuagiza mwenzake autunge tena kwa niaba yake. Sioni umaarufu wake, wala hamna vyanzo. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:33, 7 Julai 2022 (UTC)
- Hapana Sioni sidhani Kama jamaa kawatuma watu pengine mchapishaji ataweka vyanzo, Mimi binafsi namtambua ni msanii kutoka Tanzania na anafahamika
Link ya Makala iliyochapishwa na Mtandao maarufu wa muziki na burudani nchini Kenya Panishee mdudu au PANISHIT kwenye chart za muziki uliopakuliwa zaidi https://www.ghafla.com/these-are-the-top-ten-most-downloaded-songs-in-kenya/
Kuhusu Panishee Mdudu rejea pia kwenye mitandao yake ya jamii na kazi zake za kisanaa zinavyokubalika na watu wengi https://www.instagram.com/accounts/login/?next=/panisheemdudu/ sidhani Kama alichapisha mwenyewe kijinadi
Link hii nyingine ni kutoka kwenye website kubwa Tanzania https://millardayo.com/rttn/ kuhusu habari zake na kundi lake Rotten Blood
PANISHIT alifahamika zaidi baada ya kufanya wimbo aliomshirikisha Nakaay Sumari , pia alikuwa karibu na mkongwe wa hip hop , Nash Mc
Hapana ukurasa huu ni halali , Mimi nipo Tanzania ambapo msanii huyu anajulikana kwenye jamii , rejea kazi zake zilizopo mtandaoni ,Vyanzo Vimeongezwa na vinazidi kuongezeka --Hip Hop Sana Society (majadiliano) 11:24, 7 Julai 2022 (UTC)
- Naona inaweza kubaki. Hata kama ni kweli alitunga mwenyewe awali, hata hivyo ni mwimbaji halisi. Nimeondoa sehemu za matini anapojisifu na kusimulia habari za maisha zisizo na shuhuda wowote. Kipala (majadiliano) 06:21, 19 Julai 2022 (UTC)
Justin Yav Sony IMEFUTWA
haririHakuna dalili za wikipedia:umaarufu wowote, hakuna vyanzo, Kiswahili kinajaa makosa. Ifutwe. Kipala (majadiliano) 06:11, 19 Julai 2022 (UTC)
Makala hailingani na masharti ya kamusi elezo.
- inataja habari za pesa ya crypto kama "faida" tu, hakuna majadiliano kuhusu hasara. Makala haifuati Wikipedia:Msimamo wa kutopendelea upande.
- inaelekeza kwenye ukurasa wa kibiashara
- haina vyanzo
Ifutwe. Kipala (majadiliano) 07:12, 21 Julai 2022 (UTC)
Sioni maana ya makala hiyo; tukio halipo tena, liliadhimishwa kati ya wafanyakazi wa shirika chache tu, makala haieleweki vizuri. Kipala (majadiliano) 07:28, 21 Julai 2022 (UTC)
.. Olimasy (majadiliano)
Wanawake wa Tanzania IMEBORESHWA
haririMakala haina habari halisi kuhusu lemma yake. Ingawa lemma inafaa kupata makala kubwa, maudhui hii haisaidii kitu. Inaonekana mchangiaji alianza kutafsiri maneno ya kwanza ya makala ya Kiingereza (ambayo ni dhaifu) halafu alichoka. Heri tuifute. Kipala (majadiliano) 08:15, 21 Julai 2022 (UTC)
Peta Teanet IMEFUTWA
haririMakala inatumia lugha ambayo si sanifu; hakuna chanzo; hata hakuna data kuhusu mhusika hivyo napata wasiwasi kama makala inalingana na Wikipedia:umaarufu. Ama isahihishwe sana au kufutwa. Kipala (majadiliano) 12:08, 28 Julai 2022 (UTC)
2012 Bavet risasi IMEFUTWA
haririMakala ni hafifu na ina chanzo kimoja tu. Sioni pia kama ni mada inayostahili kuwepo kwenye Wikipedia. Iboreshwe au ifutwe. Asterlegorch367 (majadiliano) 10:21, 5 Agosti 2022 (UTC)
Risasi ya Danny Hansford IMEFUTWA
haririMakala ifutwe au iboreshwe, ina chanzo kimoja tu ambacho ni ukurasa mwingine wa Wikipedia. Asterlegorch367 (majadiliano) 10:21, 5 Agosti 2022 (UTC)
Toy bunduki IMEBORESHWA
haririMakala ifutwe au iboreshwe, haina chanzo hata kimoja na sidhani kama ina kigezo cha kua na ukurasa wake wa Wikipedia Asterlegorch367 (majadiliano) 10:28, 5 Agosti 2022 (UTC)
Pape sakho uosmane IMEFUTWA
haririMakala ni fupi mno, na pia haina vyanzo vyovyote Idd ninga (majadiliano) 19:59, 7 Agosti 2022 (UTC)
Ni chama cha mashoga kisichojulikana. Hakuna vyanzo. Ifutwe. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:43, 12 Agosti 2022 (UTC)
Cynthia Tse Kimberlin IMEREKEBISHWA
haririMakala ni fupi mno, pia haina vyanzo vya kutosha na kibaya zaidi imemwagwa kwenye translator kisha ikaweka kama ilivyo, napendekezwa ifutwe. si hii pekee ni karibia makala zote alizoandaa mtumiaji huyu. Olimasy (majadiliano)
Makala ni fupi mno pia haina vyanzo vya kutosha. Pia muundo wake haujakaa sawia.--- Olimasy (majadiliano)
Franco na Afro Musica IMEFUTWA
haririMakala haina vyanzo vya kutosha hivyo ni ngumu kuona kama inafikia criteria ya umaarufu Asterlegorch367 (majadiliano) 15:36, 12 Agosti 2022 (UTC)
Shule ya isimu ya Afrika IMEFUTWA
haririMakala haina chanzo hata kimoja. Pia inaonekana kama ni tafsiri ya moja kwa moja kutoka kwenye translator Asterlegorch367 (majadiliano) 15:36, 12 Agosti 2022 (UTC)
Maud Meyer VYanzo vimeongezwa, IBAKI
haririMakala haina chanzo hata kimoja na inatumia kurasa nyingine za Wikipedia kama vyanzo Asterlegorch367 (majadiliano) 15:36, 12 Agosti 2022 (UTC)
Casper Beatz IMEFUTWA
haririMakala fupi sana na haina vyanzo Asterlegorch367 (majadiliano) 15:36, 12 Agosti 2022 (UTC)
Makala haina vyanzo na muundo wake sio mzuri Asterlegorch367 (majadiliano) 15:36, 12 Agosti 2022 (UTC)
Ngoma ya Sakara IMEFUTWA
haririMakala haina vyanzo vya kutosha na muundo haujapangiliwa vizuri Asterlegorch367 (majadiliano) 15:36, 12 Agosti 2022 (UTC)
Kobe (jina lililopewa) IMEFUTWA
haririTafsiri mbovu kabisa. Hina maana. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:14, 13 Agosti 2022 (UTC)
Jabari(maumbile) IMEFUTWA
haririVilevile. Tayari kuna ukurasa jitu na ukurasa njemba zenye maana hiyohiyo. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:17, 13 Agosti 2022 (UTC)
Kuzuizi Silaha IMEFUTWA
haririMakala haieleweki, haielezi mada yake vema, haina vyanzo halisi (chanzo kinachotumika hakionyeshi uhusiano na mada), Kiswahili kina makosa. Ama iandike upya kabisa au heri ifuttwe, hasa kwa sababu lemma inayotumika ina kosa la lugha. Kipala (majadiliano) 14:21, 16 Agosti 2022 (UTC)
Malkia wa Afrika (filamu) IMEELEKEZWA UPYA
hariri1. Filamu hii ina makala tayari The African Queen, 2. Makala hii haielezi vizuri, 3. Makala hii inatumia marejeo ambayo ni hovyo hayana uhusiano na filamu Kipala (majadiliano) 19:44, 2 Septemba 2022 (UTC)
Mitandao ya kijamii na saikolojia IMEFUTWA
haririMatini ni tafsiri ya google iliyobadilishwa kidogo sana, bado haieleweki, tena dhana imefupishwa hadi kutoeleweka. Fomati haifuatwi. Kipala (majadiliano) 22:42, 7 Septemba 2022 (UTC)
Matini ni tafsiri ya google 1:1, masahihisho madogo, makosa ya tafsiri. Kipala (majadiliano) 16:13, 8 Septemba 2022 (UTC)
- Imefutwa
Makala haina marejeo, hakuna dalili ya umaarufu wowote ili awe na makala, ifutwe.Kipala (majadiliano) 17:36, 9 Septemba 2022 (UTC)
- Imefutwa
Mike Anderson IMEREKEBISHWA
haririMakala haina marejeo, hakuna dalili ya umaarufu wowote ili awe na makala, ifutwe.Kipala (majadiliano) 17:36, 9 Septemba 2022 (UTC)
Holocaust na mitandao ya kijamii IMEFUTWA
haririMatini ni tafsiri ya google 1:1, lakini fupi mno, hakuna maudhui haitoshi kama mbegu. Iandikwe upya au kufutwa. Kipala (majadiliano) 16:13, 8 Septemba 2022 (UTC)
Ugaidi na mitandao ya kijamii IMEFUTWA
haririMatini ni tafsiri ya google 1:1, masahihisho madogo, kisehemu bila kuelewa chanzo, yenye makosa. Kipala (majadiliano) 16:13, 8 Septemba 2022 (UTC)
- Imefutwa
Matini ni tafsiri ya google 1:1, masahihisho madogo, makosa ya tafsiri. Kipala (majadiliano) 16:13, 8 Septemba 2022 (UTC)
- Imefutwa
Ni tafsiri ya kompyuta, sehemu hazieleweki, enwiki inatumiwa kama chanzo. Kipala (majadiliano) 07:34, 10 Septemba 2022 (UTC)
Ni tafsiri ya kompyuta, sehemu hazieleweki, enwiki inatumiwa kama chanzo. Kipala (majadiliano) 07:34, 10 Septemba 2022 (UTC)
Giditraffic IMEFUTWA
haririNi tafsiri ya kompyuta, sehemu hazieleweki, enwiki inatumiwa kama chanzo. Kipala (majadiliano) 07:34, 10 Septemba 2022 (UTC)
Hofu ya kukosa IMEFUTWA
haririNi tafsiri ya kompyuta, sehemu hazieleweki, enwiki inatumiwa kama chanzo. Kipala (majadiliano) 07:34, 10 Septemba 2022 (UTC)
Mbwa kwenye vituo vya kupigia kura IMEFUTWA
haririNi tafsiri ya kompyuta, sehemu hazieleweki, enwiki inatumiwa kama chanzo. Kipala (majadiliano) 07:34, 10 Septemba 2022 (UTC)
Ni tafsiri ya kompyuta, sehemu hazieleweki ("mitandao ya neva"!), enwiki inatumiwa kama chanzo. Kipala (majadiliano) 07:34, 10 Septemba 2022 (UTC)
Urembo wa mtandao IMEFUTWA
haririNi tafsiri ya kompyuta, sehemu hazieleweki, enwiki inatumiwa kama chanzo. Kipala (majadiliano) 07:37, 10 Septemba 2022 (UTC)
Miundo ya mashairi IMEFUTWA
haririMakala inakosa fomati, interwiki, vyanzo, jamii. Isiporekebishwa ifutwe. Kipala (majadiliano) 13:04, 16 Septemba 2022 (UTC)
- Nakubaliana na wewe, imefutwa
Grady Booch IMEREKEBISHWA
haririMAkala inakosa fomati, lugha na misamiati sahihi haijazingatiwa, imetafsiliwa bila marekebisho yoyote kutoka google translate. -- Olimasy (majadiliano)
Maryana Iskander IMEFUTWA
haririMakala ni tafsiri mbaya ya google; ningeifuta mara moja kama isingemhusu mtu muhimu katika harakati ya wikimedia. Isahihishwe - au kufutwa (na kutungwa upya siku moja).Kipala (majadiliano) 12:28, 4 Oktoba 2022 (UTC)
Monmouthpedia IMEFUTWA
haririmakala ni tafsiri mbaya ya google. Ningeifuta mara moja lakini mafa inafaa kuwa na makala, ni mfano mzuri wa matumizi ya Wikipedia. Iboreshwa au kufutwa na kuandikwa upya siku moja. Kipala (majadiliano) 12:31, 4 Oktoba 2022 (UTC)
Tasnifu za Wikipedia IMEFUTWA
haririNi jaribio la kutafsiri en:Plagiarism from Wikipedia. Nahisi alianza na google akajitahidi kutotumia maneno ya google lakioni bado inaonekana katika muundo wa sentensi. Pamoja na hayo haieleweki, hata lemma yake. Ilhali hata makala ya kiasili ya enwiki ni dhaifu - heri ifutwe au kuandikwa upya. Kipala (majadiliano) 12:49, 4 Oktoba 2022 (UTC)
Harakati za Wikimedia IMEFUTWA
haririTafsiri mbaya kabisa- Haieleweki. Iandikwe upya (mada ina maana) au kufutwa. Kipala (majadiliano) 17:03, 4 Oktoba 2022 (UTC)
Climate change in Kenya IMEFUTWA
haririMAkala ni tafsiri ya sehemu ndogo mno ya makala ya Kiingereza. Jinsi ilivyotafsiriwa kwa kiasi kidogo tu, matini haina habari kuhusu Kenya, maana yote ni kweli kwa kila mahali duniani. Pia ni tafsiri ya google iliyonyoshwa kidogo sana. Sioni sababu ya kuendelea na makala hii kama haina habafri juu ya mada yake (Kenya!) na hata jina halikutafsiriwa. Ama iandikwe upya au kufutwa. Kipala (majadiliano) 18:58, 11 Oktoba 2022 (UTC)
Frank Tarloff IMEFUTWA
haririMakala imetafsiriwa kwa translate tool lakini haikusahihishwa. Sehemu hazieleweki (mfano jinsi alivyotafsiri "blacklisted" na maana yake...). Iboreshwe au kufutwa. Kipala (majadiliano) 16:50, 1 Novemba 2022 (UTC)
Kimbunga cha iyan IMEFUTWA MARA TATU
haririMakala haifomati fomati yoyote, tahajia inajaa makosa mno - iandikwe upya au kufutwa. Kipala (majadiliano) 20:26, 3 Novemba 2022 (UTC)
Makala haijajitoshereza kabisa, haina fomati kabisa
Makala ni mbovu kupindukia, imechukuliwa tuu kutoka google translate ikamwagwa hapo. font type na size sijui kazitoa wapi. kiufupi ni mbovu. --Olimasy (majadiliano)
Patricia Kombo IMEFUTWA
haririGogle translate; mada inaweza kufaa, na hii ni sababu nimeipeleka hapa badala ya kufuta moja kwa moja. Kipala (majadiliano) 20:13, 9 Januari 2023 (UTC)
Abdalla Alshamsi IMEFUTWA
haririSiku hizi tunapata mara kwa mara makala juu ya wafanyabiashara kutoka Uhindi na sasa pia UAE ambao si maarufu kweli na makala hizi zinasifu wahusika badala ya kutoa taarifa tu. Makala hii haifuati kanuni ya kutopendelea upande. Nina wasiwasi kuhusu umaarufu wake hata kama ametajwa kweli kwenye magazeti hayo ya huko. Sijui tunapata hapa watu wanaolipiwa kutangaza watu? Nashauri tutumie kama mwongozo wa umaarufu wa mtu nje ya Afrika kama kuna makala katika enwiki au la. Kwa watu katika Afrika iwe tofauti. Tufute hii. Kipala (majadiliano) 10:14, 22 Januari 2023 (UTC)
- Naona makala bado ipo japo imeandikwa kwamba imefutwa. Ni vigumu sana kujiridhisha na umaarufu wa watu wa nje lakini pia uandishi wake sio mzuri. Napendekeza ifutwe pia
Mohiuddin Roni IMEFUTWA
haririSalaam, Makala hii inakasoro kwenye uwandishi wa lugha na mtu huyo si maarufu, natumai wakuu mtaichunguza kwa makini. Amani iwe kwetu sote. Ayo9 (majadiliano) 09:25, 11 Februari 2023 (UTC)
Cameron Lacroix IMEFUTWA
haririMakala ni fupi mno, lakini pia bado haionekani umuhimu wa makala hii kuwepo ,haina maelezo ya kutosha,Idd ninga (majadiliano) 12:45, 1 Machi 2023 (UTC)
Augusta-Priolo IMEFUTWA
haririMakala ni fupi mno,haieleweki, hakuna vyanzo ndani yake, na bado inaonekana haina nguvu kuendelea kuwepo, labda hadi ifanyiwe maboresho,Idd ninga (majadiliano) 18:01, 8 Machi 2023 (UTC)
Ugonjwa wa mwanamke aliyepigwa IMEREKEBISHWA
haririMbali ya kuwa ni makala ndefu, lakini ina dalili ya kuwepo kwa tafsiri ya mshine, maneno mengi hayapo katika kiswahili kinachoeleweka sana, inaweza kufanyiwa marekebisho zaidi, Idd ninga (majadiliano) 11:51, 12 Machi 2023 (UTC)
Ujana miaka ya 1980 IMEFUTWA
haririMakala haikufuata miiko na miundo wa kiswahili fasaha. Aidha marejeo yaliyotolewa hayakuwa na taarifa za kutosha. MagoTech Tanzania (majadiliano) 22:18, 12 Machi 2023 (UTC)
- Nakubaliana na wewe, umefutwa Asterlegorch367 (majadiliano) 11:12, 15 Machi 2023 (UTC)
Mtumiaji:Benforty/ Dinozo IMEFUTWA
haririMakala iliandikwa kw kurudiwa (Repeat). Tazama Dinosauri. MagoTech Tanzania (majadiliano) 22:59, 12 Machi 2023 (UTC)
Makala iliandikwa kw kurudiwa (Repeat). Tazama Black Panther: Wakanda Forever. MagoTech Tanzania (majadiliano) 00:17, 14 Machi 2023 (UTC)
- Hizi filamu zipi mbili, ya kwanza ni Black Panther (filamu) na hii ya hapa ni filamu ya mwaka 2022,Mtumiaji Denis bado anaonekana kama alikuwa anafanya mazoezi ya kuandika, japo karudi vile vile kama ilivyoandikwa katika makala ya kwanza, Amani sana Idd ninga (majadiliano) 11:46, 15 Machi 2023 (UTC)
Makala iliandikwa kw kurudiwa (Repeat). Tazama Uwezeshaji wa vijana MagoTech Tanzania (majadiliano) 23:02, 14 Machi 2023 (UTC)
Mtumiaji:Elisha Andrews/Utu uzima IMEFUTWA
haririMakala iliandikwa kw kurudiwa (Repeat). Tazama Utu uzima MagoTech Tanzania (majadiliano) 00:38, 15 Machi 2023 (UTC)
Elonis dhidi ya Marekani IMEFUTWA
haririMakala imeandiwka vibaya, inaonekana ni tafsiri ya mtandao na haina vyanzo vya kutosha. Michango minginge ya mtumiaji inafanana hivi na amefungiwa. Ifutwe Asterlegorch367 (majadiliano) 11:25, 15 Machi 2023 (UTC)
FutureMedia IMEFUTWA
haririMakala inaonekana ya kutafsiri moja kwa moja kutoka kwenye mtandao na haina vyanzo. Makala zote za mtumiaji zipo hivi. Ifutwe Asterlegorch367 (majadiliano) 11:30, 15 Machi 2023 (UTC)
Shughuli zinazoendeshwa na riba IMEFUTWA
haririMakala imeandaliwa vibaya, inaonekana ya kutafsiri moja kwa moja kutoka
kwenye mtandao na haina vyanzo. Makala zote za mtumiaji zipo hivi na amefungiwa. Ifutwe