Ukurasa mama: wikipedia:Wakabidhi

Ukurasa huu una michango kuanzia 2020 hadi 2023 Machi


Mabadiliko ya uongozi hariri

Ndugu, baadhi ya viongozi wa Wikipedia yetu wameacha kazi muda mrefu. Kumbe wamejitokeza wengine, tena wenyeji. Nimeona pia kwamba wanalalamikia hali ya sasa ya viongozi wengi kutokea nchi za mbali. Kwa nini tusirekebishe hali hiyo? --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:06, 25 Aprili 2020 (UTC)[jibu]

Naona wafuatao walikuwa wakabidhi lakini hawakuonekana tena muda mrefu. Ninapendekeza tukubali utaratibu ufuatao:
  • kama mtumiaji aliyekuwa mkabidhi hajahariri kwenye swwiki kwa muda wa mwaka mmoja anafutwa kama mkabidhi
  • Kufuatana na pendekezo hili wafuatao hawakuonekana muda mrefu hivyo wangefutwa kama wakabidhi: mtumiaji:Baba Tabita (tangu 26 Septemba 2018, alituaga), mtumiaji:Malangali (tangu mwaka 2015), mtumiaji:Sj (tangu Julai 2019, tangu 2015 aliingia mara 3), ;
  • mtumiaji:Ndesanjo hakuonekana tena tangu Novemba 2019 hivyo angebaki kufuatana na pendekezo la juu. Alikuwa mmoja wa waanzilishi wa swwiki, alikuwa mbali muda mrefu alirudi 2019.

Kipala (majadiliano) 09:02, 23 Julai 2020 (UTC)[jibu]

Shughuli zinazotekelezwa na wakabidhi hariri

Ifuatayo ni takwimu ya kazi ya wakabidhi kufuatana na takwimu hii. Inaonyesha kwamba wale wenye haki za ukabidhi wanatekeleza kwa viwango tofauti, na kazi nyingi zinatekelezwa na wachache mno. Napeleka hii hapa pamoja na ombi 1) waliopo humu wajitahidi kushiriki zaidi; 2) tuangalie nani anafaa kuongezwa katika idadi hiyo (pamoja na kuondoa hao ambao wameondoka).

Shughuli la ukabidhi zilizotekelezwa
Na. Mtumiaji ana haki za alitumia haki mara ngapi Futa kurasa Kubatilisha “futa” Futa kumbukumbu Rudisha Zuia mtumiaji Batilisha “zuia” Linda kurasa Batilisha “linda”
1 Riccardo Riccioni Mkabidhi (admin) 300 149 0 0 0 145 1 5 0
2 Kipala bureaucrat, mkabidhi (admin) 141 46 0 0 0 28 2 65 0
3 Jadnapac mkabidhi (admin) 6 3 0 0 0 1 0 1 1
4 Muddyb bureaucrat, mkabidhi (admin) 6 3 0 0 0 0 0 3 0
5 ChriKo mkabidhi (admin) 3 3 0 0 0 0 0 0 0

Kipala (majadiliano) 17:47, 30 Agosti 2020 (UTC)[jibu]

Kuangalia upya orodha ya Wakabidhi kwa Mwaka 2020 na utaratibu wa kupiga kura KURA IMEFUNGWA hariri

Hatujasahihisha orodha ya wakabidhi tangu 2014; wengine hawaonekani tena, na kazi inafanywa na wachache mno. Tunahitaji A) mapatano jinsi ya kuondoa wale ambao hawapo tena na B) wakabidhi wa nyongeza.

Utaratibu wa kupiga kura hariri

Utaratibu ufuatao umekubaliwa kati ya wakabidhi waliopo (tazama ukurasa wa majadiliano)

a) Mpiga kura awe aliyewahi kuandikishwa tangu mwezi 1 (hatutaki waliojiandikisha jana kwa kumpigia kura rafiki leo)
b) aliyewahi kuhariri makala 3 kwenye swwiki (nje ya ukurasa wake mwenyewe; haitoshi kutunga/kusahihisha makala 1-2 pekee)
c) aliyehariri katika miezi 12 kabla ya kura yetu

A.) Pendekezo la kuwa na wakabidhi hai KURA IMEFUNGWA hariri

Kulingana na utaratibu jinsi ilivyo katika wikipedia nyingi inapendekezwa

A) Mkabidhi ambaye hajahariri kwa miezi 12 anaondolewa haki zake za ukabidhi; akirudi anaweza kurudishwa kwa mapatano ya wakabidhi waliopo
B) Mkabidhi aliyepo na kuhariri ataendelea (linganisha orodha juu kabisa)

Ukubali au upinge pendekezo hili; bofya "hariri chanzo" upande wa "Ninakubali" au "Sikubali" na weka alama ya ~~~~ kama sahihi yako. Anzisha kila mstari mpya kwa alama ya *

Ninakubali Pendekezo A) IMEKUBALIWA (kura 11 halali, kura 1 ya mtumiaji asiye na michango ya kutosha) hariri

Sikubali Pendekezo A) hariri

B.) Pendekezo la kuchagua wakabidhi wapya KURA IMEFUNGWA. Wote waliopendekezwa wamepita, wamepokea haki za ukabidhi hariri

  • Unaweza kuangalia michango ya mtumiaji kwenye miradi yote ukiandika username hapa

*Kwa kila jina linalotajwa kuna historia fupi ya kuhariri kwake: idadi ya kuhariri katika swwiki, (katika miradi mingine), lini alichangia mara ya mwisho kabla ya tar. 1 Septemba 2020

Hapa tutaje jina la mtumiaji. Tutafakari vema kama maarifa yake na historia ya uhariri vitamsaidia kutekeleza wajibu. Andika jina lake badala ya "NN" na weka alama (sahihi) yako ya ~~~~ kwa "Nakubali". Kama huna jina la kupendekeza, angalia waliotajwa/waliopendekezwa tayari na uweke alama (sahihi) yako baada ya "Nakubali" / "Sikubali". Baada ya siku 10 (tarehe 14 Septemba 2020) zoezi la upigaji kura litafungwa na matokeo yatatangazwa.

Alihariri: swwiki mara 1,393 (commons mara 2,543), mara ya mwisho kabla ya Septemba: 31 Agosti 2020

'Nakubali:'Aneth David (majadiliano) 11:18, 4 Septemba 2020 (UTC), Kipala (majadiliano) 08:36, 4 Septemba 2020 (UTC)BrixL (majadiliano) 10:25, 4 Septemba 2020 (UTC) --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:59, 4 Septemba 2020 (UTC)--Jadnapac (majadiliano) 12:06, 4 Septemba 2020 (UTC)- Czeus25 Masele (majadiliano) 14:27, 4 Septemba 2020 (UTC)-RollarTz (majadiliano) 05:42, 5 Septemba 2020 (UTC) Ebenezer Mlay (majadiliano) 17:36, 4 Septemba 2020 (UTC) Idd ninga (majadiliano) 17:31, 4 Septemba 2020 (UTC)̠ Olimasy (majadiliano) 13:29, 5 Septemba 2020 (UTC)-manguboy (majadiliano) 23:04, 8 Septemba 2020 (UTC) -ChriKo (majadiliano) 12:34, 9 Septemba 2020 (UTC) --'Muddyb Mwanaharakati' 'Longa' 08:50, 12 Septemba 2020 (UTC) [jibu]

Sikubali:

Alihariri: swwiki mara 500 (commons mara 1,671), mara ya mwisho kabla ya Septemba: 15 Agosti 2020

Nakubali: Idd ninga (majadiliano) 06:56, 4 Septemba 2020 (UTC) --Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:59, 4 Septemba 2020 (UTC)--Jadnapac (majadiliano) 12:06, 4 Septemba 2020 (UTC) - Czeus25 Masele (majadiliano) 14:27, 4 Septemba 2020 (UTC)- Ebenezer Mlay (majadiliano) 17:36, 4 Septemba 2020 (UTC) ana maarifa pande mbalimbali, mtumiaji hai--Kipala (majadiliano) 11:21, 5 Septemba 2020 (UTC)-Olimasy (majadiliano) 13:29, 5 Septemba 2020 (UTC) -ChriKo (majadiliano) 12:34, 9 Septemba 2020 (UTC) --'Muddyb Mwanaharakati' 'Longa' 08:50, 12 Septemba 2020 (UTC) [jibu]

Sikubali:

Alihariri: swwiki mara 1,242 (commons mara 42, wikidata mara 143), mara ya mwisho kabla ya Septemba: 30 Agosti 2020

Nakubali:--Riccardo Riccioni (majadiliano) 10:59, 4 Septemba 2020 (UTC)--;Jadnapac (majadiliano) 12:06, 4 Septemba 2020 (UTC); ana maarifa mazuri, mwanawikipedia hai Kipala (majadiliano) 14:00, 4 Septemba 2020 (UTC) - Czeus25 Masele (majadiliano) 14:27, 4 Septemba 2020 (UTC) —Ebenezer Mlay (majadiliano) 17:36, 4 Septemba 2020 (UTC) Idd ninga (majadiliano) 17:25, 4 Septemba 2020 (UTC)-Olimasy (majadiliano) 13:29, 5 Septemba 2020 (UTC)-manguboy (majadiliano) 23:04, 8 Septemba 2020 (UTC) -ChriKo (majadiliano) 12:34, 9 Septemba 2020 (UTC) --'Muddyb Mwanaharakati' 'Longa' 08:50, 12 Septemba 2020 (UTC) [jibu]

Sikubali:

Alihariri: swwiki mara 827 (enwiki mara 13) , mara ya mwisho kabla ya Septemba:18 Agosti 2020

Nakubali:--Jadnapac (majadiliano) 12:06, 4 Septemba 2020 (UTC) --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:56, 4 Septemba 2020 (UTC) - Czeus25 Masele (majadiliano) 14:27, 4 Septemba 2020 (UTC) Ebenezer Mlay (majadiliano) 17:36, 4 Septemba 2020 (UTC) ana maarifa, mtumiaji haiKipala (majadiliano) 11:18, 5 Septemba 2020 (UTC)-Olimasy (majadiliano) 13:29, 5 Septemba 2020 (UTC)-manguboy (majadiliano) 23:04, 8 Septemba 2020 (UTC) -ChriKo (majadiliano) 12:34, 9 Septemba 2020 (UTC) --'Muddyb Mwanaharakati' 'Longa' 08:50, 12 Septemba 2020 (UTC) [jibu]

Sikubali:

Alihariri: swwiki mara 57 (commons mara 73), mara ya mwisho kabla ya Septemba: 16 Mei 2020

Nakubali:--Jadnapac (majadiliano) 12:06, 4 Septemba 2020 (UTC) --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:56, 4 Septemba 2020 (UTC) - Czeus25 Masele (majadiliano) 14:27, 4 Septemba 2020 (UTC) Ebenezer Mlay (majadiliano) 17:36, 4 Septemba 2020 (UTC) Idd ninga (majadiliano) 17:31, 4 Septemba 2020 (UTC)-Olimasy (majadiliano) 13:29, 5 Septemba 2020 (UTC)-manguboy (majadiliano) 23:04, 8 Septemba 2020 (UTC) --'Muddyb Mwanaharakati' 'Longa' 08:50, 12 Septemba 2020 (UTC) [jibu]


Sikubali:anaweza kufaa lkn amehariri kidogo mno pia hakuonekana miezi 3 Kipala (majadiliano) 15:11, 4 Septemba 2020 (UTC)
[jibu]

Alihariri: swwiki mara 696 (enwiki mara 38), mara ya mwisho kabla ya Septemba: 30 Mei2020

Nakubali:--Jadnapac (majadiliano) 12:06, 4 Septemba 2020 (UTC) --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:00, 4 Septemba 2020 (UTC) - Czeus25 Masele (majadiliano) 14:27, 4 Septemba 2020 (UTC)- Ebenezer Mlay (majadiliano) 17:36, 4 Septemba 2020 (UTC)-Olimasy (majadiliano) 13:29, 5 Septemba 2020 (UTC)-manguboy (majadiliano) 23:04, 8 Septemba 2020 (UTC) --'Muddyb Mwanaharakati' 'Longa' 08:50, 12 Septemba 2020 (UTC) [jibu]

Sikubali: ana maarifa lkn hajaingia tangu miezi 3 Kipala (majadiliano) 15:11, 4 Septemba 2020 (UTC) [jibu]

Mkutano wa wakabidhi tarehe 2022-09-10 hariri

Miniti za Mkutano wa Wakabidhi ulifanyika online tarehe 10 Septemba mwaka 2022

Wakabidhi waliohudhuria: Ingo (Kipala), Christiaan (ChriKo), Aneth (Asterlegorch367), Clement (Czeus25 Masele), Otto (Olimasy), Riccardo Riccioni (Riccardo Riccioni), Ebenezer (CaliBen), Idd (Idd ninga), Antoni (Jadnapac)

Wakabidhi wasiohudhuria: Emmanuel (Manguboy), Mohammed (MuddyB) Aliyekuwepo bila kuwa mkabidhi: Mtatiro (Magotech)


1.Ingo anawakaribisha wote, agenda iliyopendekezwa inakubaliwa

2.Tunatambulishana kifupi

3. Tunashauriana kuhusu editathons. Tunaona mara kwa mara kasoro nzito zifuatazo: A) tafsiri za google, B) jamii hazikupangwa ipasavyo ; C) Interwiki inasahauliwa; D) makala za enwiki huonyeshwa kama marejeo; E) Fomati ya muundo haifuatwi kama vile jina la lemma koze mwanzoni, fomati ya vichwa vidogo ndani ya matini, marejeo; F) makala mpya wakati mwingine zimefupishwa hadi kukosa maana, hasa wakitafsiri teaser pekee; G) kasoro za tahajia kama kuchanganya l/r -

Tuliwahi kuelewana kwamba editathon inayotekelezwa kwa kufundisha wageni inatakiwa kuendeshwa kwa kufuata mfumo wa Peer Review kwa utaratibu ufuatao:

(Azimio la awali) 
A) kila mmoja aunde kwanza makala zote katika nafasi yake ya mtumiaji (user space) badala ya nafasi ya makala (article namespace ) na B) kila makala ipitiliwe na mtumiaji mwingine anayeisoma na kutaja masahihisho / kasoro halafu C) makala inaweza kuhamishwa nafasi ya makala.  D. Wanawikipedia wanaoongoza editathon ni lazima kukubali na utaratibu huu

Riccardo anauliza kama uwingi wa makala ya editahons kuna uhusiano na misaada ya Wikimedia zinazotolewa kwa kuendesha editathons hizo Antoni anakubali Wikimedia inatoa misaada ya aina hiyo Ingo anaomba kwamba kundi la Jenga Wikipedia ya Kiswahili lishirikishwe katika mashauriano kama hatua yoyote kuhusu miradi ya Wikimedia katika Tanzania kama inahusu Wikipedia ya Kiswahili

Azimio
3.1. Utaratibu wa Peer review utumike kwa mazoezi ya editahons
3.2. Tunaomba Wikimedia isikubali misaada kwa warsha au editathons zinazuhusu swwiki  kama mwandalizi / Kiongozi wa warsha hajaangaliwa kama ana maarifa ya kutosha; lazima ashauriane kwanza na mtumiaji mwenye uzoefu mkubwa anayepitia naye misaada   iliyoandaliwa, makosa yanaotokea na kasoro za kawaida    

>>>(Je, nani atapeleka ombi hili Wikimedia??)

3.3.Kama mmoja wetu ana taarifa kwamba editathon inaandaliwa, alete habari kwenye kundi la Telegram kabla ya zoezi

4. Utaratibu wa ufutaji makala Tulikuwa na utaratibu huu: A) Makala zenye matusi au matangazo ya kibiashara (hasa kama ziemfichwa) zinaweza kufutwa mara moja B) kwa kawaida mmoja akiona kasoro nzito ataweka alama ya {{futa}} halafu ataandikisha makala katika Wikipedia:Makala kwa ufutaji halafu anaweza kumpa habari mtunga makala. C) Mwingine ataangalia makala na ama kuifuta au kusahihisha au kuingia katika majadiliani kama hatambui kasoro.

Tunaweza kukatibisha pia wengine wasio wakabidhi kutumia alama ya {{futa}} na kuandikisha makala katika orodha

Majadiliano: Tunahitaji kupata njia inayozingatia mawili: A)hatuwezi kukubali makala mbaya ambazo zinaharibu hadhi ya wikipedia yetu (kama hazieleweki, makosa mengi ya lugha au maudhui, bila kufuata fomati) B) hatutaki kuwakatisha tamaa wachangiaji wapya wanaoweza kujirekebisha na kuwa wachangiaji wema

Azimio:
Tunakubaliana makala ambazo ni mbaya kabisa zinaweza kufutwa mara moja. Ni lazima kumweleza mchangiaji sababu na kumkaribisha aandike upya.  
Mengine ambayo tunaona zinaweza kuboreshwa; tuweke kwenye orodha

Tunahitaji wengi zaidi wanaopitilia ukurasa wa makala kwa ufutaji na kufute / kurudisha huko >>>>(Azimio lina tatizo: nini ni makala mbaya sana? Je tunahitaji kuelewana upya au inatosha??)

5. Akaunti maradufu ya mtumiaji mmoja: Azimio: Tusikubali akaunti zaidi ya moja kama mtumiaji hakueleza sababu maalumu inayokubalika na mkabidhi

6.Mikutano ya Wakabidhi Idd anapenekeza tuwe na mikutano ya kila mwezi. Inakubaliwa.

Ingo ataita mkutano Mwezi wa Oktoba , Anethi ataanda mkutano wa zoom.

7.Mpango wa Mwaka Mpango wa mwaka kwa swwiki inapendekezwa. Tutashauriana kwenye Oktoba na kuomba mapendekezo. Mara matokeo ya sensa zitapatikana tunapata kazi kubwa kuingiza data katika makala za kata. Hii itakuwa nafasi nzuri kufanya editathon na wageni kuwapa uzoefu wa kurudia. Vilevile makala za wabunge wa 2020 bado.

8.Agenda zilizopedekezwa lakini hatujajadili: A) Utaratibu wa kuzuia watumiaji: tukumbushane kuhusu utaratibu tuliokubali , ona https://sw.wikipedia.org/wiki/Wikipedia:Kuzuia_watumiaji. Je kuna haja ya masahihisho?

B)Je tunaye anayeweza kuwasiliana na ngazi ya Meta kuhusu mambo ya settings?

Mkutano wa Wakabidhi wa swwiki tarehe 04 Januari 2023 hariri

Ona miniti hapa Kipala (majadiliano) 10:45, 10 Februari 2023 (UTC)[jibu]

Makala zenye Mashaka hariri

Kuna jumla ya makala 529 zenye tafsiri ya Kompyuta, na bado hatujaweka juhudi ama mkakati wa kuzipunguza, je tunaweza kuzipangilia muda ambao tunaweza kuzirekebisha ,ama kuziweka sawa au ikishindikana kuzifuta kabisa, ama pia tunaweza kuziwekea mpango kwamba makala yenye tafsiri ya mashaka iwe na siku kadhaa katika Wikipedia ya Kiswahili na isiporekebishwa iondolewe ili kupunguza uwingi na uwepo wa makala za aina hiyo ? Idd ninga (majadiliano) 11:57, 12 Machi 2023 (UTC)[jibu]