Yohane Mbatizaji wa Rossi

Yohane Mbatizaji wa Rossi (Voltaggio, Piemonte, 22 Februari 1698Roma, Lazio, 23 Mei 1764) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki nchini Italia.

Papa Pius IX alimtangaza mwenye heri tarehe 13 Mei 1860, halafu Papa Leo XIII akamtangaza mtakatifu tarehe 8 Desemba 1881[1].

Sikukuu yake huadhimishwa katika tarehe ya kifo chake[2].

MaishaEdit

Mtoto wa maskini, alikwenda Roma kwa masomo[3] akapewa upadrisho ingawa aliugua kifafa.

Tangu hapo alijitosa kuhudumia wanawake fukara pamoja na wagonjwa, wafungwa, wafanyakazi na hasa kuadhimisha sakramenti ya upatanisho kwa wengi.

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

Viungo vya njeEdit

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.